Umuhimu wa kuwa na pesa ya dharula


Chukulia kwamba unaenda Bukoba, umepanda Basi la umma. Ila unapofika Nyakanazi au Biharamulo gari linakata Moto. Katika hali ya kawaida kitakachofuata Ni wewe kutafuta Usafiri mwingine, hapa kama hauna fedha ya dharula, Ni wazi kuwa utaingia choo ambacho siyo sahihi.

Tena bora safari yako iwe inaishia Biharamuro, Ila kama unaenda Bukoba mjini, Karagwe-Kaisho, hapo safari yako itakuwa bado sana. Ni kweli utakuwa umeshaingia ndani ya manispaa ya Bukoba ila kwa upande mwingine utakuwa bado hujaweza kufika mbali

Fedha ya dharula Ni Nini?
Fedha ya dharula Ni Ile fedha ambayo unakuwa nayo kama akiba kwa ajili Jambo lolote ambalo hukutuzamia kutokea. Endapo litatokea hili Jambo ambalo hukutuzamia litatokea, Basi hiyo fedha ya dharula itatumika.

Mfano unaweza kuwa unatazamia safari itachukua saa nne. Lakini safari ikachukua saa mara mbili zaidi ya kile ulichotazamia. Kunaweza kusiwe na gharama za ziada kwa upande wa  usafiri, lakini ukakuta zipo gharama zaidi upande wa chakula, vinywaji n. K.

Na hii gharama ya ziada ndiyo itafanya kazi.

Je, kuwa na fedha ya dharula si kufikiri hasi?
Unaweza kuwa unajiuliza, hivi nikiwa na fedha ya dharula si nitakuwa nafikiria hasi wakati Mimi napaswa kuwa nafikiri chanya mara zote?

Kuwa na fedha siyo kufikiri hasi. Bali Ni kufikiri katika uwekezekano (possibility thinking).
Hizi dharula huwa zinatokea katika biashara, hizi dharula zipo hivyo, ni jukumu lako wewe  kuhakikisha unajiandaa nazo.

Kutojiandaa na dharula ni sawa na kukwepa ngumi ya uso kwa kufumba macho.

Dharula hutokea maishani
Dharula huwa zinatokea maishani. Inaweza kuwa ni mfanyakazi unayemtegemea vizuri sana kuacha kazi au kuumwa na hivyo wewe kwa upande mwingine ukakwama.

Inaweza kuwa ni kifaa unachokitegemea kuzima ghafla. Mfano mimi Ni Mwandishi, na huwa natumia kompyuta kwenye uandishi. Lakini changamoto ambayo huwa nakutana nayo kwenye uandishi Ni kuwa Kuna wakati kompyuta inaweza kukuchezea na kukataa kuwaka. Au siku hiyo simu ikawa kama imeingiwa na pepo wachafu.

Sasa katika mazingira kama haya kama hauna kifaa kingine cha dharula. Ni wazi kuwa utakwama Sana.

Umuhimu wa fedha za dharula
1. Inakusaidia kukamilisha Jambo lako Kama ulivyopanga bila kukwama.
Kama ulikuwa unajenga na umepiga bajeti ya nyumba Ni milioni 50, Ni muhimu uwe na milioni walau tano za ziada ambazo zinaweza kukupiga tafu pale Ambapo Mambo yanaenda ndivyo sivyo.

2. Inakusaidia kuacha kuwasumbua watu hovyohovyo
Ngoja nikurudishe kwenye mfano wetu wa awali wa wewe kwenda Bukoba na gari likashindwa kuendelea na safari baada ya wewe kufika Biharamuro.

Ni wazi kuwa Kama hutakuwa na fedha ya dharula, utakwama. Hapa utaanza kuwapigia simu watu wengine ili wakusaidie.

Ila ukiwa na fedha ya dharula wewe mwenyewe, utajikinga mwenyewe na Mambo yako yataendelea bila kuwasumbua watu.

3. Fedha ya dharula itakupunguzia msongo
Hutakaa na kuanza kuwaza, sijui mjomba atatuma fedha au hatatuma. Atatuma kwa wakati au atachelewa. Utakachofanya, utachukua hela yako na Kuendelea na safari yako.

4. Hutamwambia kila mtu shida zako. Kama hauna fedha ya dharula, utapaswa kujieleza kwa kila MTU ukiomba msaada, hata yule ambaye ulikuwa hutazamii kumweleza changamoto zako, utalazimika kufanya hivyo.

5. Utakuwa na uhakika wa maisha. Utakuwa hauishi kwa kubahatisha.

Rafiki yangu, ni muhimu Sana uwe na fedha ya dharula. Hii fedha itakusaidia katika maeneo mengi ya maisha.
Inashauriwa walau uwe na fedha ya miezi sita mpaka mpaka mwaka mzima, hii ni fedha ya dharula ambayo Unaweza kufikia muda wowote. Hivyo basi rafiki yangu changamka, usiache kuweka akiba. Fedha ya dharula ni muhimu sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X