Iambie dunia kile unachotaka kufanya, ila  kwanza kioneshe hicho kitu


Rafiki yangu, habari ya siku ya leo. Hongera sana kwa siku hii ya leo nay a kipekee sana. mimi kwa upande wangu rafiki yangu siku ya leo, nina kitu kimoja tu ambacho ningependa kukwambia. Na kitu hiki siyo kingine bali ni kwamba kama kuna kitu ambacho ungependa kuiambia dunia, basi hicho kitu unapaswa kukisema kwa dunia, ila kwanza unapaswa kuonesha kwa vitendo kwamba unaweza kukifanya hicho kitu.

Ujue hii dunia haipungukiwi na wasemaji hata kidogo, bali inapungukiwa na watendaji. Unachotakiwa kufanya ni kwamba wewe unapaswa kuwa mtendaji sana na wala siyo muongeaji sana.

Mara zote kuwa mtendaji, na onesha kile ambacho unataka kusema kwa dunia kwa vitendo na wala siyo kwa maneno.

Mara nyingi nimekuwa nikiwaambia watu waseme malengo na ndoto zao waziwazi, kisha wazifanyie kazi. Ila sasa nimegundua haya masula ya kusema malengo na ndoto zako kwa watu hivihivho tu ni upotezaji wa muda. Na mwaka huu nataka ufanye kitu kimoja tu. Malengo na ndoto zako, usiziseme kwa mtu yeyote, kabisa. wewe fanyia kazi tu malengo na ndoto zako bila kusema chochote na kwa yeyote. nina hakika rafiki yangu, kwamba mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka. matendo yako yataongea zaidi kuliko ambavyo ungeongea kwa maneno.

Ni hayo tu ambayo nilitaka kukwambia siku ya leo. Kabla sijaachana na wewe kabisa kuna kitu kimoja ambacho ningependa ufahamu. Na kitu hiki kwamba mwaka huu 2022, mwezi Juni tutakuwa na semina mkoani MOROGORO.

Semina hii itafanyika juni tarehe 24, hapahapa mkoani Morogoro.

Kwenye semina hii, unaenda kupata mafunzo ya kipekee yatayokusaidia wewe kupiga hatua na kusonga mbele kwa juhudi kubwa sana.

Semina hii ya ana kwa ana, itafanyika kwenye mojawapo ya hoteli hapa Morogoro mjini, na itakuwa semina ya siku moja tu.

Gharama ya semina hii itakuwa 50,000 tu. Malipo yote yatafanyika kwa namba 0687848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

Karibu sana.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X