Makosa ambayo watu hufanya wanapotaka KUONGEZA chanzo kingine Cha kipato


Utakuwa umegundua kuwa wiki hii nimekuwa nikikushirikiaha nakala zinazoeleza ni kwa namna gani unaweza KUONGEZA chanzo kipato Cha ziada.

Sasa Leo napenda kukwambia kuwa bado sijamaliza nilichokusudia kukwambia. Kwenye hii makala ya leo ningependa ujue makosa ambayo watu hufanya wanapotaka KUONGEZA chanzo kingine Cha kipato. Makosa yenyewe ni

Kosa la kwanza wanaanzisha chanzo kwenye eneo ambalo wenyewe hawajui.
Kisa mtu kasikia kitu fulani kinalipa au kisa kaona mtu akifanya biashara fulani na ana MAFANIKIO, Basi utakuta kwamba na yeye anakimbilia kutaka kuwekeza huko au kuanzisha biashara ya aina hiyohiyo huku akiwa haijui Kwa undani. Ninachotaka kukwambia siku ya Leo ni kuwa unapaswa kuanzisha chanzo cha kipato kwenye eneo ambalo wewe mwenyewe tayari unalijua. Ninaposema unalijua simaanishi kwamba uwe umeshahawahi kulifanyia kazi, Bali uwe umelifanyia utafiti wa kina.
Siyo kisa umesikia eti kuna crypotocurency na wewe unakimbilia huko.
Au kisa eti unasikia mavi ya tembo ni dili na wewe unakimbilia kutafuta mavi ya tembo.

Kuwa makini!

Kosa la pili ni kutojua chanzo husika kitakuwa kinaingiza kipato kwa muda gani.
Kila chanzo cha kipato huwa kinaingiza kipato kwa nyakati tofauti. Ni muhimu kwako kujua chanzo cha kipato kitakuwa kinaingiza fedha baada ya muda gani.

Hatifungani huwa zinaingiza kipato kila baada ya miezi sita
Kuna kampuni hisa zake huwa zinatoa gawio kila baada ya miezi sita na nyingine kila mwaka. Hayo yote unapaswa kuyajua.
Uwekezaji kwenye miti huwa unatoa kipato baada ya muda mrefu. Kumbe basi ni jukumu lako kujua vizuri aina ya chanzo cha kipato na kitakuwa kinagiza kipato baada ya muda gani.

Unahitaji kuwa na mchanganyiko. Vyanzo vinayoingiza kipato kila siku au kila wiki na vyanzo vinavyoingiza kila mwezi, baada ya miezi kadhaa na vile vya muda mrefu.

Kama ndio unaanza wekeza zaidi kwenye vyanzo vinavyotoa kipato kila siku au kila wiki au kila baada ya siku chache.

Kosa la tatu ni kubeti. Kuna wengi wanaofikiri kuwa kubeti ni chanzo, cha kipato. Vijana wengi wamenasa kwenye huu mtego. Hawafanyi kazi wala kujituma wakitegemea kubahatisha.

Rafiki yangu, maisha hayabahatishwi. Yana kanuni zake, zipo wazi kabisa.
Ukizifuata utafika mbali kabisa.

Ndiyo maana tunaziongelea kwenye hii blogu kila mara.

Kosa la nne ni kuanzisha chanzo Cha kipato kinachohitaji usimamizi mkubwa wenyewe wakiwa hawapo.

Kuna vyanzo ambavyo vinahitaji usimamizi mkubwa mwanzoni. Kosa ambalo watu hufanya ni kuanzisha vyanzo vinavyohitaji usimamizi mkubwa mwanzoni huku wao wakiwa wapo mbali.

Mfano mtu anaanzisha chanzo chake cha ziada kwenye kilimo biashara huku yeye akiwa mbali. Kilimo kina mambo mengi ambayo nyuma ya pazia yanahitaji kufanyiwa kazi, kumbe basi kitu kama hiki unahitaji ukianzishe ukiwa karibu ili kufanya usimamizi wa karibu.


One response to “Makosa ambayo watu hufanya wanapotaka KUONGEZA chanzo kingine Cha kipato”

  1. Asante’ kwa makala nzuri,Kuna comment km ya pili Kama sikosei kwangu Mimi Nina mtazamo tofauti kuhusu kuanzisha biashara ukiwa mbali…Cha msingi ni mfumo unaofaa kusimamia biashara usika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X