Kitu Kimoja Kinachopaswa Kukufanya Usome Vitabu Vya Hardcopy badala ya Softcopy


Rafiki yangu, linapokuja suala la softcopy au hardcopy watu wamekuwa wanakuwa na mtazamo tofauti. Wapo wanaopendelea hardcopy na wapo wanaopendelea softcopy na wengine wanapendelea audiobook kama huyu hapa

Kwa upendeleo wowote atakaokuwa nao mtu, hakuna ambaye anakuwa sahihi wakati mwingine akiwa hayuko sahihi. Kitu kikubwa sana ni kupata maarifa yaliyo kwenye kitabu na kuyafanyia kazi.

Ila siku ya leo ninapenda nikwambie sababu hii moja ambayo inapaswa kukusukuma wewe kupata vitabu vya nakala ngumu au audiobook na siyo softcopy.

Na sababu hii ni kwamba, kama una watoto au mtoto mdogo. Hii ni sababu kubwa kwa nini unapaswa kununua vitabu vya nakala ngumu au vitabu vilivyosomwa (audiobook).

Ili unielewe vizuri hapa naomba nieleze kwa undani kidogo, mtoto mdogo ana tabia ya kuiga kile ambacho mzazi anakuwa anafanya.

Unapokuwa unasoma kitabu kwenye simu, mtoto anakuwa hajui kama unasoma kitabu au husomi kitabu. Kitu hiki kinamfanya mtoto awe anapenda kushika simu. Ila unapokuwa unasoma kitabu cha kushikika (hardcopy), mtoto anakuwa anaona. Kitu hiki kinamfanya mwanao apendelee zaidi kushika kitabu cha nakala ngumu na hivyo kumjengea tabia ya kuanza kusoma vitabu mapema.

Hivyo, kama wewe ni mzazi, sambamba na kusoma vitabu vya nakala laini (sofcopy/ebooks), hakikisha unakuwa na nakala ngumu kadhaa pale nyumbani kwako. Pale ambapo utakuwa na mtoto,  usisome kitabu kwenye simu, badala yake soma kitabu cha nakala ngumu.

Mpe na mtoto kitabu ashike, ili aanze kuzjenga tabia ya kusoma vitabu mapema sana.

Unatakiwa pia kupenda vitabu vya kusikiliza unapokuwa na mtoto. Kwanza inasaidia kumwongezea mtoto misemo ya ziada. Na tafiti zinaonesha kwamba watoto wanaokuwa wanaojifunza misemo mingi, huwa wanajiamini mbele ya watu kuliko ambao wanakuwa na misemo kidogo. Lakini pia watoto wanaokuwa na misemo mingi huwa ni wawasilishaji wazuri wa mada. Ssa wewe hupendi mwanao awe mwasilishaji mzuri wa mada? Naamini wewe ni kama mimi, na ungependa mwanao awe gwiji wa kuongea na kuwasilisha mada mbele za watu kwa kujiamini na bila uoga wowote.

Watu wengi huwa wanapenda pale ambapo huwa wanaona  mtoto mdogo anasimama mbele ya watu na kuongea kwa kujimini. Wengi hupiga makofi na kumpongeza kwa namna ambavyo wanaweza, ikiwa ni pamoja na kutoa zawadi ya pesa.

Naamini na wewe unaweza kumlea mwanao hivyo, kwa kuanza kumjengea misingi sahihi sasa hivi.

Nakutakia siku njema

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


One response to “Kitu Kimoja Kinachopaswa Kukufanya Usome Vitabu Vya Hardcopy badala ya Softcopy”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X