Faida Tatu KUBWA unazopata pale unapowekeza kwenye hisa


Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy)

Rafiki yangu, umewahi kuwaza kwamba ukiwekeza kwenye hisa utanufaika na kitu gani?

Kuna faida nyingi za kuwekeza kwenye hisa, ila kwenye hii makala ya siku ya leo ningependa kuongelea faida mbili kubwa kwa haraka

Faida ya kwanza ya kuwekeza kwenye hisa ni kupata ongezeko la thamani.  Ongezeko la thamani ni pale unaponunua hisa kwa bei ya chini na baadaye kuja kuiuza kwa bei ya juu.

Mfano mwaka, 2022 hisa za CRDB zilikuwa zinauzwa na kununuliwa kwa bei ya shilingi 150. Sasa hivi hisa hizohizo zinauzwa shilingi 380. Hii ndio kusema kwamba aliyenunua hisa kipindi hicho cha mwaka 2020 kwa shilingi 150, sasa hivi kila hisa yake ina thamani ya shilingi ya 380. Kumbe hapa kila hisa ina ongezeko la thamani la shilingi 230 na zaidi.

Na hiyo ni pesa ambayo imeongezeka bila ya wewe kutoa jasho wala kufanya kazi yoyote ile. Ulichofanya wewe ni kuwekeza fedha yako tu.

Hii ndiyo faida kubwa ambayo watu wanaomiliki hisa huwa wanaipata.

Faida nyingine ambayo utaipata kama utamiliki hisa ni  GAWIO. Gawio ni faida ambayo wanahisa wanapata. Faida huwa inapatikana kulingana na wingi wa hisa ambazo mtu anakuwa anamiliki kwenye kampuni husika. Kumbe basi, hisa ni kitegauchumi ambacho kila mtu anapaswa kuwa nacho na anapaswa kukimiliki.

3. Hisa ni kipimo cha utajiri. Leo hii dunia inamfahamu Elon Musk kama tajiri mkubwa duniani. Ila tajiri huyu siyo kwamba ana mabilini yote ya fedh mfukoni. Utajiri wake uko kwenye hisa anazomiliki kwenye makampuni ya TESLA, SPCAEX na makampuni mengine. Kumbe hisa, ni kipimo cha utajiri wa mtu husika. Na wewe tunaweza kupima utajiri wako kwa kuangalia vitegauchumi ulivyo navyo ikiwa pamoja na hisa unazomiliki..

Rafiki yangu, kama bado hujawa na kitega uchumi hiki cha kipekee basi hakikisha kwamba unakuwa nacho.

PATA KWANZA NAKALA YA KITABU CHA MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Hiki kitabu kitakupa mwongozo wewe wa kuweza kuanza kuwekeza kwenye hisa, hatifungani na vipande.

Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy)


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X