Wafanyakazi na mfumuko wa Bei


hisa na nguvu ya vitu vidogo  kuelekea mfanikio makubwa
hisa na nguvu ya vitu vidogo kuelekea mfanikio makubwa

Kila tarehe 1 mwezi Mei. Macho na masikio yote ya wafanyakazi huwa yapo kwa kiongozi mkuu wa nchi kuona kama atawaongezea mshahara.

Unajua kwa nini huwa wanataka ongezeko la mshahara? Ni kwa sababu kile kipato wanachokuwa nacho mwanzoni kinakuwa hakitoshi kuwafanya wamudu mahitaji ya kila siku. Hivyo, ongezeko la mshahara likiwepo kweli, linaweza kuwa suluhisho, japo kwa kiasi fulani. Lakini kesi hii haiishii hapo, hii kesi ni kubwa na mahakama haitoshi, ndio maana tunaendelea mbele mpaka tupate suluhisho😋😋

Utakumbuka kwenye makala ya jana tuliongelea juu ya suala zima la mfumuko wa bei. Lakini mwisho wa siku tuliona ni kwa namna gani unaweza kuukwepa mfumuko huu wa bei kwa kufanya uwekezaji.

Sasa siku ya leo nataka tuone uhusiano uliopo Kati ya mshahara na mfumuko wa bei na kwa nini kila mwaka wafanyazi huwa wanaomba ongezeko la mshahara. Lakini kama  kawaida yangu, sitakuacha hivihivi, maana lengo langu siyo tu kuliongelea tatizo pekee, bali kukupa suluhisho.

Kabla sijaenda mbali zaidi. Naomba niwashukuru wale wote wanaosoma makala zangu na kunipa mrejesho. Na hasa wanaoenda mbali zaidi na kusapoti kazi zangu kwa kununua. Nyie ndio mnawezesha ujio wa makala nyingine zaidi kama hizi. Asante sana

Sasa ili tuweze kuelewa kwa kina zaidi kwa nini wafanyakazi wanakuwa wanahitaji ongezeko la mshahara, inabidi uelewe kwa kina dhana ya mfumuko wa bei kama nilivyoieleza jana.

Mfumuko wa bei huwa unatokea kila mwaka, na serikali kupitia benki kuu ya Tanzania (BoT) huwa inatangaza mfumuko wa bei kwa mwaka huo umekuwa ni kiasi gani. Ila mshahara huwa hauongezeki kila mwaka, kumbe basi kama mfumuko wa bei unaongezeka kila mwaka na mashahara hauongezeki kila mwaka, basi hapo Kuna shida sehemu……..

Jana nilisema kwamba mfumuko wa bei ni pale Ambapo uwezo wa fedha kufanya manunuzi unapungua japo fedha inabaki ileile.
Mfano kama ulikuwa na elfu moja mwanzoni mwa miaka 2000 ulikuwa na uwezo wa kununua nguo za kutokelezea mtaani. Ila leo hii elfu  huwezi kununua nguo ya kudamshi kwa elfu moja hiyohiyo😂😂.

Elfu moja imebaki ileile, Ila uwezo wake wa kufanya manunuzi umepungua.

Tuchukulie unalipwa mshahara wa laki moja. Na mwaka huu mfumuko wa bei ni asilimia 4.4 kama ulivyoripotiwa. Tazama jedwali hapo chini

Kama mwwka huu  mfumuko wa Bei ni 4.4 na wewe mshahara wako ni laki moja. Maana yake mshahara utapokea uleule Ila utakuwa umepungua uwezo wa kufanya manunuzi kwa asilimia 4.4.

Asilimia 4.4 ya mshahara wa laki moja ni 4400.

Kumbe basi, Kama mwaka jana mshahara wako wa laki moja ulikuwa unakutosha kuishi vizuri.
Mwaka huu hautakutosha kwa sababu ya mfumuko wa bei. Mshahara wako utabaki uleule ila utakuwa umepungua uwezo wa kufanya manunuzi kwa asilimia 4.4 sawa na shilingi 4400/-

Kumbe basi ndio maana wafanyakazi wanakuwa wanahitaji ongezeko la mshahara.  Ili walau like ongezeko la mshahara lifidie kile kilichopungua kutokana na mfumuko wa bei.

Kama mfanyakazi ana matumizi sawa na mshahara wake. Na mfumuko wa bei ni asilimia 4.4. anahitaji, ongezeko la mashara linaoendana na mfumuko wa bei ili asiingie kwenye mikopo ili kukidhi mahitaji yake. lakini endapo, hakutakuwa na ongezeko la mshahara, maana yake huyu mfanyakazi, atapaswa kukopa kiasi cha walau shilingi 4400/- ili kuongezea kufidia mfumuko wa bei uliotokea. Na hapo atakuwa ameanza kuingia kwenye madeni.

Hiki kitu ndicho huwa kinawafanya wafanyakazi waombe ongezeko la mshahara zaidi.

sasa mfanyakazi anaweza kufanyaje ili kuondokana na hali hii?

Kwanza ni kuhakikisha kwamba anapata elimu sahihi, kuhusu mfumuko wa bei.

Pili ni kuanza kufanya uwekezaji. maana njia pekee ya kuukwepa mfumuko wa bei ni kuwekeza sehemu ambayo inaweza kukupa mrejesho mkubwa kuliko mfumuko wa bei wenyewe.

na kwenye hili nimekua nakushauri walau kuwekeza UTT, kwenye mifuko ya uwekezaji wa pamoja. Unajiuliza, mfuko wa pamoja ni nini? UTT ni kitu gani? Naanzaje kuwekeza kwenye UTT na maswali mengine kama hayo? basi, tuwasiliane kwa 0755848391 ili uweze kupata nakala ya kitabu chako. Karibu sana.

Makala hii imeandikwa na Godius Rweyongeza.

Baadhi ya makala za Godius Rweyongeza zimechapwa kwenye magazeti makubwa nchini Tanzania likiwemo gazeti la MWANANCHI.

Kupata vitabu vya Godius Rweyongeza unaweza kwa kuwasiliana na 0755848391/ +255755848391 kwa simu au whatsap.


One response to “Wafanyakazi na mfumuko wa Bei”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X