Kitu kimoja ambacho watu hawajui kuhusu uwekezaji


Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy)

Rafiki yangu, najua Kuna aina mbalimbali za uwekezaji. Uwekezaji kwenye ardhi na NYUMBA (real estate), mali zisizo hamishika, uwekezaji kwenye kilimo cha miti, hisa, hatifungani na vipande  na uwekezaji mwingine.

Hata hivyo kitu kimoja ambacho watu hawajui Ni kuwa, uwekezaji kwenye hisa, hatifungani na vipande ni uwekezaji ambao unaweza kuanza kuifanya hata kama huna mtaji mkubwa.

Kwa mfano, ili uwe mwekezaji kwenye ardhi na nyumba tena ukiwa mjini, unakuta inakugharim mpaka milioni 50 na zaidi.

Lakini kwa upande mwingine, uwekezaji kwenye hisa Ni tofauti. Ili uwekeze kwenye hisa, kiwango Cha chini Cha kuwekeza kwenye HISA Ni hisa kumi tu.
Ambapo kiasi konachohitajika kwa pamoja kitategemea na Bei ya hisa kwa wakati husika.
Mfano, Leo hii ninapoandika hapa. Mojawapo ya kampuni kwenye soko la hisa Bei yake ni 120. Hii ndio kusema kuwa Kama unanunua hisa kumi unatakiwa kuwa na shilingi 1200/-. Ukiongeza gharama nyingine za madalali maana yake inafika karibia 2300/-

Kwa hiyo, ukiwa na 2300/- unaanza kuwa mwekezaji. Na bado unaweza kuendelea kuwekeza zaidi kadiri siku zinavyoendelea.

Hakuna uwekezaji kwenye ardhi unaoweza kuufanya kwa  2300/-

Na hata ukiangalia ukiangalia hisa zenye Bei kubwa. Nikiangalia Bei za mwisho Jana wakati soko la hisa linafanyika . Hisa za Bei ya juu zilikuwa ziliuzwa kwa 16,200/-
Ili ununue hisa kumi maana yake unapaswa kuwa na 162,000/- ambapo ukiongeza na gharama nyingine za madalali inafikia 163,100/-

Bado kwenye ardhi hiki kiwango Ni kidogo Sana kukufanya ufanye uwekezaji wa maana. Ila kwenye hisa, inawezekana.

Rafiki yangu, ninachotaka kukwambia Leo Ni kuwa, Ni rahisi sana kuwekeza kwenye HISA kuliko ilivyo kuwekeza kwenye eneo jingine. Maana kiwango Cha kawaida Cha pesa ndicho kinahitajika kuanza nacho unapowekeza

Chukua hatua uanze kuwekeza kuanzia leo. Kwa kuanzia nashauri upate nakala ya kitabu changu Cha Maajabu ya kuwekeza kwenye HISA HATIFUNGANI NA VIPANDE.

KItakupa mwongozo na kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uwekezaji kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Kupata nakala ya kitabu hiki utapaswa kulipia 5,000/- kwa ajili ya softcopy ya kitabu hiki.

Lipia Sasa kwa AIRTEL MONEY:  0684408755 jina ni GODIUS RWEYONGEZA
Au tuwasiliane kwa 0755848391.

Karibu sana

Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy0
Kitabu hiki kinapatikana kwa elfu tano tu (sotfcopy)


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X