Sababu tano kwa nini utahitaji kutoa kitabu chako kwa njia ya mtandao kwanza kabla ya kukitoa kwa njia ya nakala ngumu


Unapozungumzia kutoa kiytabu chako kwa mfumo wanakala laini, basi swali ala kwanza ambalo watu huwa wananiuliza ni kuwa vipi kuhusu hakimiliki? Hili huwa ni swali kubwa sana ambalo watu huwa wanauliza. Kwenye makala ya leo ningependa kuongelea kwa nini unapaswa kutoa kitabu chko kwa mfumo wa nakala laini kwanza kabla ya kutoa kitabu hicho kwa nakala ngumu.

Hata hivyo, ushauri huu haumfai kila mtu. Siyo kila mtu anapaswa kutoa kitabu kwa nakala laini kwanza, ila kama utaweza unaweza kuanza kutoa nakala laini halafu baadaye ukatoa nakala ngumu.

Moja ni kwa sababu ni bei rahisi kutoa nakala laini kuliko ilivyo kutoa nakala ngumu

Utoaji wa vitabu kwa mfumo wa nakala laini umerahisisha mambo mengi sana. zamani ilikuwa kwamba ili utoe kitabu chako basi ulipaswa kuwa chini ya taasisi au kampuni ya uchapishaji. Kampuni hii ilipaswa kupitia kitabu chako. Kama kampuni hiyo ingependa kitabu chako na aina ya uandishi wako basi ulikuwa na bahati, kitabu chako kilikuwa kinachapwa. Kama kampuni ilikuwa haitami kitabu chako, basi ulikuwa unaenda maji. Maana yake kitabu chako kisingechapwa. Ndio maana ukifuatilia historia nyingi za waandishi wakubwa zinhusisha kukatawaliwa mara nyingi kabla ya kucha vitabu vyao.

Lakini hii tafsiri yake nyingine ni kuwa kwa kila mwandishi mkubwa unayemwona, kuna waandishi wengine wengi ambao hawakuweza kabisa kuchapa vitabu na vitabu vyao leo hii havipo kwenye mfumo wowote ule. Hii ni kutokana na mfumo wa uchapaji iwa vitabu wa wakati huo ulivyokuwa. Kama kampuni au taasisi ya uchapaji wa vitabu ilikukataa, basi ulipaswa kwenda kutafuta kampuni au taasisi nyingine na kama zingekataa zote, basi ndoto yako ilikuwa imefikia mwisho.

Ila sasa siku hizi mambo yamebadilika. Yamebadilika kabisaa, yaani, unawez kuandika kitabu chako na kukiachapa kwa njia ya mtadao. Bila kuhitaji hizi kampuni kubwa ambazo zilikuwa zinaweka kiwingu kwa miaka mingi na kuzuia watu kufikia ndoto zao za uandishi.

Kwa hiyo, badala yaw we kushindwa kuchapa kitabu kwa sababu ya hizi kampuni, unaweza kuchapa kitabu chako kwa njia ya mtandao na kuanza kufikisha ujumbe wako kwa jamii.

Pili ni kwa sababu hauhangaiki kusambaza vitabu kwa watu

Ukichapisha vitabu kwa mfumo wa kawaida, unakuwa unahitajika usambaze vitabu hivi, kwa watu. na mbaya zaidi ni pale unapokuwa umechapisha wewe mwenyewe. Maana wewe unahitajika usimamie ubora wa uchapaji wa kazi yako, unahitaji uhakikishe kuwa unasafirisha vitabu kutoka kwa mchapaji mpaka kwako, unatakiwa kutangaza vitabu vyako. Unatakiwa utume vitabu mpaka kwa mteja, endapo vitabu vitapotea njiani basi utatakiwakutuma vitabu vingine ili viweze kumfikia.

Ila ukichapa kitabu chako kwa njia ya mtandao basi unakuwa hizo kadhia zote ambazo zinaweza kukupata.

aMaana yake mtu atakinunua kwa njia ya mtandao, na wewe utakuwa umemaliza mchezo.

Tatu ni kwa sababu unakuwa unatest mitambo

Kuna wakati mwandishi unaweza kuandika kitabu ila ukawa huna uhakika kama kitabu hicho kitakubalika miongoni mwa wasomaji wako au la! Ununuaji wa kitabu kwa njia ya mtandao unakupa picha ya namna kitabu hicho kitakavyonunulika kwa njia ya kawaida.

Na hiki hata kampuni na taasisi zinazofanya uchapishaji kwa njia ya asili zinakifanyia kazi sasa hivi. kuna kampuni sasa hivi hazichapishi kitabu chako, mpaka kitabu chako kiwe kimeuza nakala kadhaa kwa njia ya mtandao.

Usihofu, kampuni hizi hazipo hapa Tanzania, zipo nje ya nchi.s

Nne, ni njia nzuri ya mwandishi yeyote mchanga kuanza na baadaye kukuza jina lake kuwa jina kubwa

Ksms wewe unayesoma ni rais Samia Suluhu, au ni waziri mkuu Kassim basi njia hii haikufahi, maana najua tu hata kabla hujamaliza kitabu chako, kampuni nyingi za uchapaji zinakuwa zimeshakufuata kwa kuutaka mswada wako. Ila kama wewe ndio kwanza unaanza na hauna mtaji wa kuchapa vitabu vyako mwenyewe, basi  hapa, basi hapa utapaswa kuandika na kutoa kitabu chako kwa njia ya mtandao. Gharam ayake ni kidogo au hakuna kabisa.

Lkwa hiyo hiki kitu kinakufanya, unaanza kutoa ujuzi, kutumia kipaji chako au kufanya kitu unachopenda bila ya kuhitaji kuweka gharama ya ziada.

Tano, sababu unaandika vitabu vingi ambavyo huwezi kuchapa kw wakati mmoja.

Mimi karibia kila mwezi huwa naandika na kutoa kitabu kimoja. Sasa kutoa nakala za hivi vitabu kwa njia ya mtandao ni rahisi kuliko ilivyo kuhakikisha kwamba unachapa na kutoa nakala ngumu kila mwezi.

Kama na wewe una spidi kkubwa ya uchapaji wa vitabu karibia kila mwezi, basi maana yake unaweza kuamua kuchapa baadhi ya vitabu kw anjia ya mtandao kwanza, halafu baada ya hapo vitabu vingine utachapa kwa njia ya kawaida.

Rafiki yangu, hizo ndizo sababu tano kwa nini na wewe unahitaji kuchapa vitabu vyako kwa njia ya mtandao. Naomba nijue maoni yako hapa chini kuhusu hii mada ya leo ni yapi.

Karibu sana.

Makala hii imeandikwa name,

Godius Rweyongeza

Unaweza kunipata kupitia 0755848391

Kama umependa makala hii, ni wazi kuwa utapenda mafunzo yangu ambayo huwa natoa kupitia kwenye channel yangu ya youtube. Hakikishaumesubsceibe leo hii kwenye channel hii nzuri kwa ajili yako.

Kupata vitabu vyangu ambavyo nimeandika kwa njia ya mtandao, basi bonyeza hapa ili uchague kimoja, halafu unipigie uniambie kipi ungependa kupata ili nikutumie.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X