Kitu cha kufanya kama unataka kupata matokeo ya tofauti


Moja ya kitu ambacho watu huwa wanapenda kwenye maisha ni kupata maisha ya tofauti na maisha mazurri. Sasa leo nataka nikuoneshe ni kitu gani haswa unapaswa kufanya kama unataka kupata matokeo ya tofauti kulinganisha na vile ambavyo umekuwa unapata siku zote.

Kwanza kabisa kama unataka kupata matokeo ya tofauti unapaswa kuwa mtu wa tofauti. Hapa maana yake matendo yako na hata maneno yako ambayo umekuwa unatumia siku zote vipaswa kubadilika ili uweze kuendana na haya matokeo mapya ambayo unayataka. Huwezi kupata matokeo ya tofauti kwa kuendelea kufanya vitu vilevile kila siku, ambavyo umekuwa unafanya siku zote.

Albert Einstein aliwahi kunukuliwa akisema kwamba ujinga ni kufanya vitu vilevile huku ukitegemea kupata matokeo ya tofauti. Kumbe kama unataka kupata matokeo ya tofauti rafiki yangu sharti uwe tayari kufanya vitu vya tofauti kuliko ambavyo umekuwa ukifanya siku zote. Labda utakuwa unajiuliza hivi hivi vitu vya tofaut ambavyo ninapaswa kufanya ni vitu gani.  Ninachotaka kukwambia ni kuwa kama hujui ni kitu gani cha tofauti ambacho unaweza kufanya, basi fanya kazi kwa bidii kwenye kazi yako kuliko ambavyo umekuwa unafanya na kuliko mtu mwingine yeyote.

Kama hujui kitu cha tofauti cha kufanya, basi soma vitabu mbalimbali kuhusiana na fedha, malengo na maendeleao binafsi, kisha fanyi kazi kile unachojifunza kutoka kwenye vile vitu unavyojifunza.

Kwa jinsi hiyo utakuwa umeanza kufanya kitu cha tofauti.

Tumia muda wako vizuri, badala ya kutumia muda wako kufanya vitu ambavyo siyo sahihi, tumia muda wako vizur kufanya kitu ambnacho ni sahihi kwako mara zote.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X