WEWE UBADILIKE PIA…


Umewahi kuona hili …

Watu wengi huwa wanapenda sana kuzungumzia mabadiliko ila ni wachache sana ambao huwa wapo tayari kuweka kazi ili kuhakikisha kwamba wanapata mabadliko ambayo wao wenyewe wanataka!

Kwenye kila uchaguzi viongozi ambao huwa wanaahidi kuleta mabadiliko ndio ambao huwa wanapigiwa makofi yanguvu.

Nataka nikwambie kitu rafiki yangu. na kitu hiki ni kwamba wewe pia unapaswa kuwa sehemu ya mabadiliko ambayo unapenda kuyaona. Usiishie tu kushangilia kuwa unataka kuona mabadiliko bali usababishe mabadiliko.

Linapokuja suala zima la mabadiliko kuna vitabu vitano ambavyo ningependa kukushauri usome

Kitabu cha kwanza ni kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA

Hiki ni kitabu ambacho nimeandika mimi mwenyewe. Kitabu hiki kimeeleza ni kwa namna gani unaweza kufanya makubwa kwa kuanza na kidogo.

Nashauri sana usome kitabu hiki ikiwezekana sasa hivi. nakala ngumu yakitabu ni 20,000/- Nakala laini na audiobook pia zipo.

Kitabu cha pili ni JONATHAN LIVINGSTONE SEAGULL.

Hii ni hadithi inayoeleza kwa namna gani watu waliokuzunguka kwenye jamii yako wanaweza kukuzuia wewe kufanya mabadiliko. Niliwahi kueleza kidogo kuhusu hii hadithi hapa

Kitabu cha tatu ni kitabu cha WHO MOVED MY CHEESE

Ndani ya hiki kitabu unaenda kuona ni kwa namna gani watu wanaongelea mabadiliko ila hawachukui hatua. Lakini pia utajifunza kuona kuwa muda mwingine mabadiliko siyo kwamba yanakuja kama ajali, bali kuna viashiria fulani ambavyo vinakuja ila sasa tatizo la watu wengi ni kuwa huwa hawaviangalii hivi viashiria. Ni hadithi fupi tu ya kawaida ila yenye mafunzo makubwa

Kitabu cha nne ni kitabu cha MAKE YOUR BED

Mwandishi wa kitabu hiki kaongea ukweli kwa lugha rahisi sana. anasema kwamba kama unataka kubadili dunia. Basi anza kwa kuhakikisha kitanda chako kimetandikwa. Hilo tu!

Si kama kitu cha kijinga ee! Yaani, wewe una mpango wa kufanya mabadiliko makubwa hapa duniani, halafu eti mtu anakwambia anza kwa kutengeneza kitanda chako. Siyo kweli!

Mwandishi anasema kwamba ukitoka nyumbani kwako umetandika kitanda chako, hata ukienda kufanya majukumu mengina yasipofanikiwa, bado utakuw ana uhakika wa kitu kimoja na kitu hicho ni kwamba kitanda chako nyumbani kwako kipo safi.

Hapa mwandishi anatusisitiza kuwa walau kwenye maisha yako ya kila siku, chagua kitu hata kama ni kidogo. Jijengee utaratibu wa kukifanya kila siku. Mambo mengine yote hapa duniani yanaweza kukwama, ila utakuwa na uhakika kuwa hicho tu umekikamilisha na kipo sawa. Ni hilo tu.

Sasa sijui wewe kitu gani kidogo ambacho unaenda kujijengea utaratibu wa kukifanyia kazi kila siku bila ya kuacha.

Rafiki yangu, hivyo ndivyo vitabu vinne ambavyo kwa leo naweza kukushauri usome. Vina mambo makubwa kuhusiana na mabadiliko na jinsi gani ambavyo wew eunaweza kufanya makubwa kwa kuanzia hapo hapo ulipo.

Kama utapenda kupata audiobook za hivyo vitabu vyote, karibu. AUDIOBOOK ya kitabu cha kwanza ni 10,000/- na audiobooks za kitabu namba mbili mpaka nne pia utazipata kwa kuchangia vochatu.

Karibu sana.

Kama bado hujasoma kitabu changu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA nashauri sana usome kitabu hiki.

Unaweza kupata vitabu hivi kwa kuwasiliana na 0755848391

Fanya hivyo sasa hivi.

Umekuwa nami

Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz

Kwa maswali, maoni au booking: songambele.smb@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X