Unawezaje Kujiajiri kwa Mtaji Kidogo?


Ebu fikiria kwamba ungekuwa wewe. Una mtaji kidogo na hutaki kuajiriwa ila una ndoto kubwa za kufanya makubwa hapa duniani. Una ndoto za kujenga biashara ambayo itakuwa kubwa na kukuingizia kipato kuliko hata kile ambacho ungepata kama mwajiriwa. Ungefanyaje kama ungekuwa na mtaji kidogo?

Kuna watu ambao huwa wanasema kwamba ngoja nikaajiriwe kwanza, baadaye nikikuza mtaji wangu nitarudi kujiajiri na kuanzisha biashara. Lakini hii njia huwa haifanyi kazi. kama unadhani nakudanganya, angalia kwenye jamii yako. Ni waajiriwa wangapi wametoka ajirani kwa ajili ya kuja kuajiriwa.

Wengi unawaona wameajiriwa, wakati wanaajiriwa walikuwa wanasema kwamba wanaenda ajirani kutafuta mtaji. Ila sasa imeshapita miaka kumi na bado wanasema kwamba wanatafuta mtaji. Sasa sijui wanatafuta mtaji wa bilioni ngapi ili waanze?

Kumbe kama una mtaji kidogo kusema kwamba, uende kutafuta mtaji ili uje uajiajiri inaweza isiwe njia nzuri.

Kwa hiyo unafanyaje sasa unapokuwa na mtaji kidogo na unataka kujiajiri?

Au labda unapaswa kuoa au kuolewa na mwenye hela ili upate mtaji? Hahahah

Kwa kuanza kujadili hii mada, tuanze kwa kujiuliza hivi kwani mtaji kidogo maana yake nini?

Ngoja kwanza hilo swali pia litatushinda kiulijibu maana hapa pia kuna kitu bado hatujakiweka sawa. Kwa hiyo tuanze kwanza kwa kujiuliza mtaji maana yake nini? ili baada ya hapo tuweze kujibu mtaji kidogo maana yake nini?

Mtaji maana yake nini?

Kwa mantiki ya makala hii naomba tukubaliane kuwa Mtaji ni fedha ambayo inayohitajika ili kuanzisha biashara. Kumbuka nimesema kwa mantiki ya makala hii. Kwa sababu mtaji ni zaidi ya hapo.

Kumbe basi swali letu hapo juu tungeweza kuligeuza na kusema kwamba unafanyaje unapokuwa na fedha kidogo ya kuanzisha biashara? Haya lakini ili tusipotee tujikunbushe tena swali letu.

Ni hili hapa mtaji kidogo maana yake nini? kiukweli udogo au ukubwa wa mtaji utategemea na aina ya biashara ambayo mtu anataka kuanzisha. Kwa wengi ukizungumzia mtaji. Maana yake unakuwa unaongelea mamilioni kwa mamilioni ya fedha. Mara kwa mara nimekuwa napokea simu au jumbe za watu ambao wanasema kwamba wana mtaji kidogo, ila ukimdadisi huyo mtu, utakuta kwamba mtaji wake siyo kidogo kama anavyosema.

Ndio, unaweza kukuta mtu anakwambia nina mtaji kidogo wa milioni tano, nina mtaji kidogo wa milioni kumi. Kuna siku mtu alinipigia simu ananiuliza biashara gani afanye. Huyo mtu aliendelea kuniambia kuwa ana mtaji kidogo wa milioni ishirini. Sasa unabaki kujiuliza hivi mtaji mkubwa sasa unaanzisha shilingi ngapi?

Hivi kwa mfano nikikuuliza wewe mtaji mkubwa unaanzisha shilingi ngapi na mtaji kidogo ni shilingi ngapi?

Enhee tulia hapohapo na jibu lako hilo. Ebu muulize rafiki yako swali hilohilo. Mwombe akwambie yeye anaelewa nini linapokuja suala zima la mtaji na mtaji mkubwa unaanzia shilingi ngapi? (majibu yako ya mtaji mkubwa na majibu ya rafiki yako, tuwekee kwenye eneo la comment mwisho wa makala hii)

Lakini nina hakika, majibu unayoenda kupata kutoka kwa rafiki yako, yatakuwa tofauti kabisa na ya kwako.

Wewe unaweza kusema mtaji mkubwa ni kuanzia milioni moja. rafiki yako akakwambia mtaji mkubwa ni kuanzia milioni kumi na mwingine akakwambia milioni mia moja.

Kulingana na jinsi ambavyo nimekuwa nikifanya kazi na watu mbalimbali, nimekuja kugundua kitu kimoja ambacho vijana wengi wameshikilia kwenye akili zao ni kwamba mtu anapoongelea mtaji, basi anakuwa anaongelea kuanzia milioni hamsini. milioni mia moja au milioni mia mbili!

Kama kila mtu akishikilia hiki kitu kichwani mwake, nadhani kwa wengi itakuwa vigumu kufanya biashara yoyote maishani. Na hiki ndicho kinawafanya wafanyakazi wengi washindwe kufanya biashara kwa sababu tu wanasubiri wawe na mtaji mkubwa.

Kwa nini watu wanafikiri kuwa mtaji unapaswa kuwa ni fedha nyingi?

Kujibu swali hili cha tuanze kwa kuangalia biashara  yoyote ambayo inafanya vizuri.

Ukiingia kwa mfano kwenye ofisi za kampuni ya VODACOM, TIGO, HALOTEL, AIRTEL si ofisi zao zinavutia ee! Kiyoyozi, viti vya kunesa, komputa za kutosha, simu ya mezani, samani za maana na mambo mengine.

Sasa vijana wengi wanaanza biashara kwa fikra kama hiyo. Ndio maana kwa wengi linapokuja suala zima la mtaji, basi wanadhani wanapaswa kuwa na hayo mamilioni ya hela kwa sababu  picha waliyonayo kwanza kichwani mwao ni kutengeneza ofisi yenye vifaa na thamani kama hiyo.

Najua utasema, Songambele mbona hujibu swali sasa? Badala ya kujibu swali unahubihubiri tu hapa?

Ok sawa, ngoja sasa tukimbushe tena swali..swali letu la leo linasema unaweza kujiajiri ukiwa na mtaji kidogo?

JIBU ni ndio. Unaweza.

Unawezeje?

Kwanza unapaswa kujua aina ya biashara ambayo unapaswa kufanya.

Pili unapaswa unapaswa kujua kiasi Cha fedha ulichonacho. Japo ni kweli kuwa unaweza kujiajiri kwa kuanza na mtaji kidogo ila siyo kila biashara inaweza kuanzishwa na mtaji wako huo ulionao.

Kwa mfano kama una mtaji wa milioni moja, kuna biashara kadha wa kadha ambazo unaweza kuanzisha, lakini pia kuna biashara ambazo huwezi kuanzisha. Kwa mfano kama unaanzisha bishara ya kuuza matunda na una milioni moja, milioni moja ni mtaji mkubwa sana! kama unaanzish mgahawa na milioni moja, unaweza kuanza hata kwa kupikia nyumbani kwako na ukafanya delivery badala ya kuanza kwa kukodi chumba.

Kumbe kujua gharama zinazohitajika kwenye aina ya biashara ambayo unataka kuanzisha, kunakusaidia wewe kuweza kujua pia namna ambavyo unaweza kuanza biashara yako.

Tatu, kama biashara unayotaka kuanzisha inahitaji mtaji mkubwa kulinganisha na kiasi ulichonacho, basi unaweza kuanza biashara nyingine tofauti na ile unayofikiria kwa sasa hivi, ukakusanya mtaji ili baadaye uje uingie kwenye hiyo biashra unayotaka.

Mfano, tuseme kwamba unataka kufanya biashara inayohusiana na afya, kufungua maabara, pharmacy, dispensari na vitu vya aina hiyo. ni vigumu kwako kufungua bishara kwa mtaji wa milioni moja.

Kama ndoto yako na malengo yako ni kufanya hii biashara ila mtaji wako ulionao ni kidogo, iweke pembeni kwanza. Kisha chagua biashara nyingine ambayo unaweza kuanza kwa mtaji ulionao sasa hivi.

Halafu, kuza hiyo biashara. Baadaye ukishakuwa na fedha zako sasa utahamia kwenye biashara yako uipendayako.

Nadhani upande wa kujiajiri kwa mtaji kidogo tumeumaliza. Kilichobaki sasa ni kuchukua hatua kuhakikisha kwamba kweli unaanzisha biashara.

Changamoto kubwa ambayo Bado ipo mbele yetu ni kujua namna gani unaweza kujikimu?

Ujue ukiajiriwa ni rahisi Sana. Kila mwisho wa mwezi una uhakika kuwa Kuna fedha ambayo lazima tu itaingia. Na kwa kutumia fedha hiyo, utaweza kufanya maamuzi ya kujikimu. Lakini unapojiairi stori ni tofauti kabisa.

Kuna mwezi unaweza kuingiza kiasi kikubwa na wakati huohuo Kuna mwezi utaingiza kidogo. Sasa unafanyaje ili ujikimu?

Sijajua ni biashara gani unaanzisha Ila nina uhakika na kitu kimoja tu. Ukiongeza mauzo kwenye biashara yako, maana yake utaongeza mapato ya biashara na mapato yakiongezeka basi utakuwa na uwezo wa kuiendesha biashara lakini pia utaweza Kupata mshahara mzuri!

Mshahara? Mambo ya mshahara yametoka wapi wakati umejiajiri?

Hapa tumeshaanza kuongea kibiashara zaidi hivyo wacha tuendelee.
Kwanza naomba nikukumbushe kuwa hapa umeshaanzisha biashara. Achana na Mambo mengine yote ya sijui una mtaji kidogo, sijui…… Achana nayo kwanza.

Sasa una biashara.
Kumbuka biashara ni yako ila unapaswa kusimama kwa kujitegemea tofauti na biashara. Yaani, jua kuwa kuna wewe na kuna biashara. Fedha ya biashara iwe ya biashara. Fedha yako iwe ya kwako. Na hapa ili utofautishe fedha yako na ya biashara, wewe unapaswa kuwa mfanyakazi namba moja kwenye biashara yako na unapaswa kijilipa mshahara!

Unaweza kijilipa kila mwisho wa mwezi au kila mwisho wa wiki au kila SIKU. Nashauri zaidi ujilipe kila wiki.

Unajilipaje sasa? Unajilipa shilingi ngapi?
Kuna namna mbili za kijilipa. Namna ya kwanza ni kujilipa kiwango fulani kila mara (siku, wiki, au mwezi). Kama ambavyo wanalipwa wengine walioajiriwa.

Unaweza kijilipa kwa kamisheni. Njia hii ya kujilipa kwa kamisheni maana yake unapata asilimia fulani kama mshahara kwenye kila mauzo utakayofanya. Labda tuseme asilimia kumi!

Kwa hiyo kila ukifanya mauzo ya milioni moja unapata asilimia kumi ambayo ni sawa na laki moja.

Ukiuza milioni tano mshahara wako unakuwa ni laki tano.

Ukiuza milioni kumi mshahara wako ni milioni moja.

Kwa njia hii unakuwa huna ukomo wa kulipwa. Juhudi zako ndizo zinakufanya ulipwe zaidi.
Na hiki ndicho kinafanya biashara inakuwa tamu 😊😊!

Ukifanya biashara kwa njia hii utajisukuma kuikuza zaidi na zaidi na hutakuwa na ukomo wa kulipwa.

ONYO: Kwa kusoma hapa inaweza kuonekana rahisi ila siyo rahisi kihivyo. Inahitajika kazi, kujitoa na kujisukuma sana. Au nikiazima maneno ya aliyekuwa waziri mkuu wa uingereza Churchill, utatoa jasho, damu na machozi.

Ila hilo lisikutishe, kwa sababu kama wengine wameweza wewe utaweza pia. Juhudi ambazo ungeweka kwa mwajiri, unaweza kuziweka kwenye biashara yako na ukanufaika pia.

SOMA ZAIDI: Kama Sio Wewe Nani? Kama Sasa Lini? INAWEZEKANA

Lakini sambamba na hilo unahitaji mwongozo, mwongozo wa kufuata ili kuikuza biashara yako kwa viwango vikubwa. Kitu ambacho nina uhakika nacho ni kwamba una ndoto ya kuiona biashara yako iking’aa. Nimekuandalia mwongozo utakaokusaidia kwenye hili na mwongozo huu ni wa kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Kitabu hiki kitakushika mkono Mpaka ufanikishe ndoto yako hiyo.

Lakini kwa vile unaanzia chini Tena kwa Mtaji kidogo, pia unahitaji kitabu cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA. Huu ni mwongozo ambao unapaswa kutembea nao popote unapokuwa. Utakushika mkono Mpaka ufanikishe ndoto zako!

Vitabu vyote hivyo vinapatikana kwa elfu 20, kwa kila kimoja. Ila fedha ambayo unatoa ni kidogo ukilinganisha na miongozo unayopata.

Hivi utajisikiaje endapo utaanzisha biashara bila ya kuwa na mwongozo na baadaye biashara yako ikafa ukashindwa kutimiza ndoto yako kwa sababu ya kukosa mwongozo!

Inauma sana! Sasa ili kuepuka haya yote! Pata nakala za vitabu Hivi leo hii.

Kumbuka kila nakala moja ni 20,000/- tu! Kwa hiyo nakala zote mbili ni sawa na 40,000/-. Ila kwa sababu ni wewe, ukilipia elfu 40,000 Leo hii nitakutumia vitabu Hivi buure kabisa. Hutaongeza Gharama za usafiri!

Changamkia Sasa. Tuma fedha kwa 0755848391 ili utumiwe vitabu leo hii bila ya kuchelewa.🤝🤝

Umekuwa nami

Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro-Tz

Kwa maswali, maoni au booking: songambele.smb@gmail.com


4 responses to “Unawezaje Kujiajiri kwa Mtaji Kidogo?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X