Business to Business (B2B) Ni Nini?


Business to business ni mfumo wa BIASHARA unaofanyika kati ya Kampuni na Kampuni au kati ya BIASHARA moja na nyingine.

Yaani, Kampuni inatengeneza bidhaa kwa ajili ya kuuza kwa Kampuni nyingine na siyo kwa walaji wa mwisho.

Kampuni nyingine zinaweza kuwa na bidhaa za aina mbili. Bidhaa moja ya kuuza kwa walaji wa mwisho na bidhaa nyingine kwa kampuni nyinginezo.

Au bidhaa moja inaweza kuuzwa kwa watu kwa bei tofauti. Walaji wa mwisho wakauziwa kwa bei ya juu kidogo wakati biashara au kampuni ikiiuziwa kwa bei ya chini.

Mfano bidhaa ya inayouzwa elfu ishirini kwa walaji wa mwisho inaweza kuuzwa elfu kumi na tano au chini kwa biashara nyingine.

Hiyo ndiyo business to business (B2B)


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X