App mbili ambazo kila mfanyabiashara anapaswa kuwa nazo


Kuna app mbili ambazo kila mfanyabiashara anapaswa Kuwa nazo.

1. Thl accounting
Hii inakusaidia kutunza hesabu zako zote za biashara. Na bidhaa ZAKO zote ulizonazo kwenye Biashara yako, itakuonesha bidhaa zinazokaribia kuisha au zilizoisha, itakusaidia kutengeneza invoice, itakusaidia kutunza hesabu za mauzo, mapato mpaka matumizi.
Hata Kama uko mbali bado unaweza kuona mwenendo wa  biashara yako. Kitu hiki Ni muhimu Sana kwako wewe mfanyabiashara.

Rafiki yangu, hii ni moja ya app ambayo nakushauri Sana uwe nayo kwenye biashara yako. Itakusaidia kufanya mengi kwa manufaa.

2. Beem
Hii inakusaidia kutuma SMS kitalaam. Yaani, unatuma sms zenye jina la biashara. Kama umewahi kuona SMS za voda, Tigo au halotel wanazotuma. Sms ambazo huwa zinakuja kwa msomaji Ila hawezi kujibuoja kwa moja. Badala yake unaweza kumwekea link au namba ya kujibu. Kama hii hapa

Hii Ni muhimu kwako mfanyabiashara.
Kwanza utafanya biashara yako ionekane kitalaamu zaidi.

Lakini pia utafanya wateja wakuamini. Kuna wateja wakiona tu kuwa unaweza kutuma jumbe za aina hiyo, watashawishika na kuona wewe unawafaa zaidi.

Unaweza kuwatumia wateja SMS za kuwajulia Hali
SMS za kuwakaribisha kununua
Ofa za sikukuu na kawaida
Mzigo mpya unaposhuka
N. K.

Hizo ndizo app mbili ambazo ni lazima kila mfanyabiashara awe nazo.

Kama ungependa kujifunza zaidi namna bora ya kuzitumia, Basi usisite kuwasiliana nami kwa 0755848391

Karibu sana.


One response to “App mbili ambazo kila mfanyabiashara anapaswa kuwa nazo”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X