Utafanyeje Unapokuwa Na Wazo La Kufanya Biashara Ila Huna Mtaji


Rafiki yangu, leo nataka niongee na wewe na kwa namna ya kipekee sana. Najua kwamba kuna vijana wengi huko mitaani ambao wana ndoto za kufanya makubwa. Vijana ambao wana ndoto za kuanzisha biashara ila tatizo au kisingizio wanasema,ni kwamba hawana mtaji.

Je, ni kweli kwamba tatizo lako ni mtaji. Je, ni kweli kwamba hauna mtaji wa kukutosha kuanzisha biasahra?

Siku ya leo nataka nikupe mfano kidogo tu wa mnyororo wa chakula. Hiki kitu tulijifunza shule ya msingi

Kwenye mnyororo wa chakula ni kwamba mnyama aliye juu kwenye myororo wa chakula anakula mnyama aliye chini yake.

Mahindi yanaliwa na panya na panya analiwa na Bundi

Karoti zinaliwa na Sungura na sungura analiwa na mbwa mwitu na mbwa mwitu wanaliwa na simba

Sasa nataka kusema nini kwa kuonesha hivi vitu. Nataka nikwambie kwamba, kama una wazo la biashara au la kufanya kitu chochote kile ila huna mtaji, maana yake una NDOTO KUBWA.

Kitu hiki siyo kibaya maana mara zote nimekuwa nakusisitiza wewe uwe na NDOTO KUBWA kweli.

Ila sasa unataka uwe Simba wakati hujafikia hivyo viwango Unapokuwa na ndoto kubwa unapaswa kuwa tayari kuanzia chini na kupanda juu. Siyo utake kuanzia juu kwa juu.

Yaani, ni sawa na kwamba uwe SUNGURA kwenye mnyororo wa chakula halafu eti utake kumla MBWAMWITU.

Kubali kwamba kwa sasa wewe ni SUNGURA na kula majani. Baadaye ukifikia hatua ya USIMBA utakula hao mbwa mwitu bila tatizo lolote.

Hiki ni kitu ambacho unapaswa kukipokea, kwa sababu pia vijana wengi hawapendi kuanzia chini. wengi wanapenda kuanzia juu kwa juu. Unakuta kijana ana ndoto ya kuanzisha biashara na anakwambia kwamba yeye anataka kufanya biashara ya mtaji wa milioni 200. Sasa wewe unafanyaje biasahra ya mtaji wa milioni mia mbili wakati hata mtaji wa milioni moja unakushinda kuuendesha vizuri? Unafanyaje?

Kiukweli kubali kuanzia chini.kisha kubali kukua kidogokidogo, mpaka mwisho.

KILA LA KHERI

Umekuwa nami

Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE CONSULTANCY

Tuwasiliane kwa 0755848391

Morogoro-Tz

NB: Hakikisha kwamba umepata kitabu changu cha NGUVU YA WAZO NA KITABU CHA MITAJI 8 ILIYOKUZUNGUKA NA JINSI YA KUITUMIA. Vitabu hivi viwili vitakusaidia sana wewe kuweza kufika mbali kwenye kufanyia kazi wazo lako na hata kupata mtaji wa kuanzia kwenye kufanya biashara. Upo tayari nikutumie vitabu hivi viwili? Upo tayari?

TUma elfu kumi leo nikutumie ebooks zote mbili. Wahi sasa hivi.

Tuma kwa 0755848391 jina ni Godius Rweyongeza. Akhsante


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X