Nini mchango wa smartphone kwa mfanyabiashara?Binafsi napenda sana maswali. Napenda maswali kwa sababu maswali ndiyo yanatufanya tukue, maswali ndiyo yameifanya dunia iwe kama ilivyo leo hii. Hii ni kutokana na dhana ya wanasayansi kutaka kujua zaidi. Watu wanajiuliza hivi kitu fulani kikifanyika kwa namna fuani itakuwaje? Hivi kweli ugonjwa fulani hauwezi kupatiwa tiba? Hivi hatuwezi kufanya utaratibu wa kwenda kwenye anga na kuishi? Hayo ndiyo maswali ndio huwa yanaanzisha tafiti na mwisho wa siku watu wanakuja na majibu.

Napenda sana maswali kwa sababu maswali yanakufanya unakua. Maswali yanakufanya unajua yale uliyokuwa hujui, maswali yanakufanya mjinga kwa dakika moja ila mwisho wa siku yanakuacha ukiwa mwelevu maisha yako yote.

Na hii dhana ya kuuliza maswali kwa sisi binadamu tunazaliwa nayo. Tukiwa watoto tulikuwa tunauliza maswali sana aisee…

Leo ungeweza kuuliza maswali kuhusu Mungu? Kesho yake ukauliza maswali kuhusu kitu au mtu fulani uliyemwona na keshokutwa ungeweza kuuliza hata jinsi watoto wanavyopatikana! 😂😂, ila utoto jamani…

Sasa leo hii kuna swali nimeulizwa. Swali linasema kwamba nini mchango wa smartphone kwa mjasiriamali? Eti, nini mchango wa smartphone au simu janja kwa mjasiriamali? Kuna mchango wowote kweli kama upo?

Ili tujue umuhimu wa smartphone kwa mfanyabiashara, tunapaswa kuangalia takwimu kwanza.

Gazeti la Jamhuri la Jumanne Disemba 17-23, 2019 liliandika hivi

Ripoti ya mawasiliano ya juni 2019 ya TCRA inaonesha kuwa idadi ya watumiaji wa intaneti hapa nchini imefikia 23,142,960 na kati ya hao 22,281,727 wanatumia mtandao huo kupitia simu za mkononi.

Nayo kampuni ya GlobalData Technology ya Uingereza imesema ifikapo 2024, idadi ya simujanja itafikia milioni 30 hali inayotarajiwa kuongeza matumizi ya data mara dufu kutokana sababu zifuatazo:

 • Uwepo wa teknlojia husika ya (3G,4G&4G+).
 • Uwepo wa simu za mkononi zinazowezesha matumizi ya intaneti.
 • Uelewa wa kidigitali. Watu wanazidi kuelimika katika matumizi ya inteneti.
 • Uwepo wa majukwaa rafiki kama mitandao ya kijamii (facebook, twitter n,k).
 • Kampuni za simu kutoa vifurushi vinavyowezesha wateja kutumia intaneti kwa urahisi zaidi.
 • Maudhui sahihi.

Hizo ndizo takwimu rafiki yangu. Kiufupi ni kuwa watu zaidi milioni 23 sasa hivi unaposoma hapa wanatumia mtandao wa intaneti na idadi inazidi kuongezeka kila siku. Hizi takwimu hizi hazimhusishi rafiki yangu ambaye amenunua simujanja jana kwa mara ya kwanza! Halafu ujue nipo siriazi, kuna rafiki yangu kanunua simu janja jana na jana hiyohiyo tukaongea kwa whatsap video, chezea simu janja wewe!

Siku hizi mtu anaweka akiba maalumu kwa ajili ya kununua simujanja. Kama ambavyo mimi na wewe tunaweka akiba ya kununua kiwanja! Pengine wewe mwenyewe leo hii upo unaweka akiba kwa ajili ya kununua simu janja nyingine….

Kitu kikubwa kuhusu simujanja au smartphone ni kwamba, siku hizi huwezi kutengenisha maisha yetu ya kila siku na hizi simu. Sisi ni simu na simu ni sisi. Kila tunapoenda tunazo. Ni kama vile simu zimekuwa sehemu ya pili ya maisha. Simu zimekuwa kama nguo!

Kuna watu wanapenda simu zao kuliko hata wenza wao! Mungu anawaona

Ukiingia kwenye daladala unakuta mtu anatumia simu, unaweza kupanda kituo kimoja na kushuka kituo kingine, mtu asijue kama ulikuwa umekaa pembeni yake. Watu wanasahau mpaka kushuka kwenye vituo vyao kisa wanatumia smartphone zao. Kuna mpaka mtu anakwambia kwamba maisha bila ya smartphone ni magumu sana. kwani unadhani uongo? Watu wa aina hiyo unao hapo mtaani, mtu ambaye akipotelewa simu yake anaomboleza mpaka kila mtu anajua…mtu ambaye akikosa kifurushi cha kuingia mtandaoni siku hiyo anakonda ghafla.

Hayo ndiyo maisha ya sasa.

Imenibidi nieleze hayo yote kwanza, ili mwisho wa siku tuweze kujua umuhimu wa simujanja au smatphone kwenye maisha ya sasa hivi, na kwa mfanyabiashara.

Kama mtu anashinda na simu yake kwa kutwa nzima, si fursa hiyo? Na siyo tu kwamba anashinda nayo, bali tafiti zinaonesha kwamba mtu wa kawaida anaiangalia simu yake mara 2617 kwa siku. Wakati wale watumiaji konki wanagusa simu zao  mara 5427.

Ona,

 • Mtu akiamka asubuhi kitu cha kwanza anagusa simu yake kabla hata ya sala.
 • Chakula siku hizi tunaagiza kwa simu
 • Pesa tunatuma kwa simu
 • Wapendwa wetu tunawasiliana nao kwa simu
 • Usafiri siku hizi tunauita kwa simu. Hatuna tena muda wa kujipanga eti unasubiri boda au teksi.
 • Mpaka biashara zenyewe zinasimwamiwa kwa simu. Kama wewe hujaanza umechelewa.

Kwenye biashara lengo la biashara yoyote ile ni kupata wateja. Au kwa lugha nyingine, watu wa kununua bidhaa kutoka kwenye biashara husika na hivyo kuleta faida. Sasa kama watu unaowahitaji wewe kwenye biashara yako, wanatumia simu muda wote unafanyaje? Hapo sasa ndipo unapaswa kufunguka..

Zama za sasa hivi zimebadilika sana…

Kwa hiyo, mfanyabiashara kwenye ulimwengu wa leo, huna budi kuhakikisha kwamba biashara yako, unaiweka kwenye mazingira ya kuonekana kwa watu hawa wanaoshinda wanatumia simujanja zao.

Hii ndio kusema kwamba kama watu  wanashinda facebook, basi wewe biashara yako inapaswa kuwepo facebook.

Kama watu wanashinda instagram wewe pia biashara yako inapaswa kuwepo huko.

Mfanyabishara yeyote makini, anapaswa kuona fursa kubwa kwenye matumizi ya simu janja na hivyo atumie hii fursa.

Kwa hiyo kama wewe ni mfanyabiashara hakikisha kwamba

 BIASHARA YAKO UMEIWEKA MTANDAONI.

Si unajua ee, siku hizi mtu akiwa na tatizo, sehemu ya kwanza kabisa anapokimbilia ni mtandaoni. Anaperuzi ili aweze kupata suluhisho lake. Hii ndiyo kusema kwamba, kama leo hii unamiliki biashara na hujaiweka mtandaoni, kuna watu wanakosa huduma yako kwa sababu tu hujaweka biashara yako mtandaoni. Maana yake ni kwamba, kama wewe biashara yako inahusiana na sabuni na mtu akiwa na shida akaingia mtandaoni na kutafuta kitu kinachoendana na sabuni. Atakikosa kwa sababu, wewe hujaingia mtandaoni kumwekea kitu cha aina hiyo, na kwa jinsi hii utakuwa umepishana na gari la mshahara…

Siku hizi biashara zinafanyika mtandaoni aisee….

Wateja wako wanapaswa kukuta wewe mtandaoni.

Yaani, mteja akiwa ana tatizo, akitafuta kitu, moja kwa moja google imlete kwako. kama wewe unafuga mbuzi au kuku, ikitokea tu mtu akatafuta kitu kinachohusiana na mbuzi au kuku, basi moja kwa moja aletwe kwako…

SASA WANAKUKUTAJE MTANDAONI

Ndio kama ambavyo nimeshaeleza hapo mwanzoni. Tengeneza kurasa za mitandao ya kijamii. Lakini kikubwa zaidi, na hapa nasema kikubwa zaidi ni wewe kuhakikisha kwamba unakuwa na tovuti. Kwa mfanyabiashara yeyote yule ambaye yuko makini na angependa kunufaika na biashara yake mtandaoni, basi hakikisha una tovuti au blogu ya biasahra yako…

Mitandao ya kijamii kuna wakati huwa inapoteza baadhi ya vitu ambavyo umeweka. Ila tovuti, haipotezi kitu labda wewe uamue kukiondoa…

Na ubora ni kwamba tovuti unakuwa unaimiliki wewe mwenyewe kama ambavyo Zuckeberg anamiliki facebook. Na wewe tovuti yako, ni ya kwako tu na wala hakuna mtu wa kukuingilia kwenye hili eneo..

Kwa hiyo basi, nashauri sana sana, utengeneze tovuti au blogu.  Ukihitaji msaada kwenye hili, nicheki kwa 0755848391 ila kaa ukijua kwamba kuna gharama kidogo utapaswa kutoa, japo hizo gharama zisikuogopeshe kama kweli upo siriazi na biashara yako, maana zinaenda kujilipa ndani ya muda mfupi tu. Utapoteza kidogo sasa hivi, kwa ajili ya faida kubwa hapo baadaye.

Kuna mengi sana ya kusema kuhusu simu na mtandao wa intaneti ila kwa leo, nataka niishie hapa tu. Mjadala uendelee kwenye eneo la kutoa maoni hapa chini…

Na sasa leo hii napenda nikwambie kwamba, kama utaweka oda. Utapata pia ebook ya bure ya Maajabu ya mtandao wa intaneti. Ambapo ndani yake nimeeleza kwa kina

 • Umuhimu wa smartphone kwa mfanya biasahra
 • Namna ya kuutumia mtandao wa intaneti kwa manufaa
 • Jinsi ya kujiweka mtandaoni mapema kabla ya wateja wako
 • Mtandao wa intaneti kama sehemu ya kukuingizia kipato
 • Na mambo mengine mengi…

Weka oda yako leo hii kwa kuwasiliana nami kwa 0755848391. Au nitumie ujumbe tu wenye jina lako, namba yako ya simu na mahali unapoishi

Mfano

1.Godius Rweyongeza 0755848391 (Morogoro mjini, Morogoro).

2.

3.

4.

5.

Na wewe nitumie jina lako sasa.


2 responses to “Nini mchango wa smartphone kwa mfanyabiashara?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X