Je, Kuna Namna Na Kutengeneza Fedha Kupitia Affiliate Marketing Ukiwa Nchini Tanzania?


Habari ya huko upande wa pili. Mimi kutokea hapa mkoani Morogoro naendelea vizuri tu.

Siku ya leo napenda kujibu swali la mmoja wetu hapa kwenye jukwaa ambaye ameniuliza kama kuna namna ya kutengeneza fedha kupitia affiliate marketing ukiwa hapa nchini Tanzania.

Na mimi kwa ufupi napenda kusema kwamba INAWEZEKANA.

Ila naomba usome ujumbe huu mpaka mwisho, ili uweze kuelewa hii dhana ya affiliate marketing kwa undani.

Kwanza kabisa tujibu swali la inawezekanaje?

Kwa hiyo kama kozi inauzwa kwa gharama ya laki moja. Punde tu baada ya hiyo ebook kununuliwa kwenye akaunti yako utaingiziwa elfu kumi ambayo unaweza kuitoa hapohapo au ukasubiri iongezeke pale watu watakaponunua kozi au ebooks zaidi kupitia kwako .

Kwa hiyo kama wewe ukiitangaza na mtu akainunua kupitia link maalumu ya affiliate marketing ambayo ni ya kwako. kikiuzwa tu, unapata elfu moja hapohapo bila ya kuchelewa.

Kadiri utakavyouza kitabu kwa watu wengi zaidi ndivyo utakavyopata kiasi kikubwa zaidi…

Nadhani upande huo umeisha…

Ukitaka kujua namna ya kutengeneza akaunti ya affiliate marketing, unaweza kuangalia video hii hapa chini

Sasa hapa nataka niongee kitu, ambacho ni zaidi ya kutengeneza akaunti.

Mpaka hapa umeshajua kwamba inawezekana wewe kutengeneza akaunti ya affiliate marketing, na umeshajua kwamba unaweza kupata hela kwa njia hii.

Sasa kifuatacho nataka nikwambie kwamba, unapaswa kukifanya kwa uendelevu. Kwa miaka ambayo nimekuwa naandika na kuuza vitabu, nimegundua kwamba huwezi kumwambia mtu mara mmoja kwamba una kitabu akanunua, kuna watu ni wagumu kununua. Na hili siyo kwenye vitabu tu, lakini pia kwenye karibia kila bidhaa kutoka kwenye kila sekta. Ndio maana kampuni za magari zinajitangaza kila siku. Ndio maana kampuni za simu zinajitangaza kila siku pia. Kwa sababu kuna watu hawachukui hatua mara moja.

Hivyo, basi, kama unategemea kuingiza kipato kwa hii njia, hakikisha kwamba, unatangaza na kuwakumbusha watu wako mara kwa mara ili waweze kununua na hatimaye wewe uweze kuingiza kipato kizuri tu.

Pili ni kwamba, tangaza bidhaa ambazo ni nzuri kwa watu wako, ili wakinunua hizi bidhaa, mwisho wa siku waweze kurejea kwako kujua bidhaa gani zaidi wanaweza kununua, na hivyo uendelee kutengeneza pesa kupitia hao watu kwa mara nyingine.

Tatu, weka mpaka utaratibu wa kuwaelimisha watu wako. Ili kupitia elimu unayotoa, watu wahamasike na waweze kuchukua hatua, kitu kitakachopelekea wewe kupata kiasi fulani cha fedha.

Mpaka wakati mwingine, mimi sina la ziada


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X