Niweke Fedha zangu benki Kama akiba au niwekeze kwenye CRDB Mzigo Flexi?


Juzi kuna mtu alinipigia simu. Alikuwa ameniakiliza kupitia TEMINO YA CLOUDS FM. Swali lake lilikuwa moja tu na hakuwa na kitu kingine cha ziada

Alitaka kujua kipi ni Bora, Kati ya kuweka fedha yake benki au kuwekeza kwenye CRDB Mzigo flexi!

Unajiuliza kwani CRDB MZIGO FLEXI ni nini?

Huu ni aina ya uwekezaji ambapo unaikopesha benki ya CRDB fedha, halafu yenyewe inawekeza kwenye miradi mbalimbali baadaye inakupa faida ya asilimia 9. Kwa mwezi, baada ya miezi mitatu, sita au kwa mwaka.

Haya ni makubaliano ambayo mnaingia Kati yako wewe na CRDB, kwa hiyo fedha yako unapoiweka huku inakuwa salama na wanapaswa kukulipa wewe kiasi cha fedha mlichokubaliana.

Kama umesoma kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE utagundua Kuwa Hii Ni aina ya HATIFUNGANI.

Kama hujasoma kitabu changu hiki cha kipekee ngoja nukupitishe tu kwa haraka.

Kuna aina mbili za hatifungani:

Hatifungani za serikali (ambapo wewe unaweza kuikopesha serikali hela yako kwa makubaliano ya kuwa ikurudishie hela yako pamoja na hiyo faida ya kila baada ya muda fulani ambapo mara nyingi huwa ni kuanzia miezi sita, miaka mitatu, kumi na hata ishirini au ishirini na tano.

Hatifungani za serikali huwa zinatolewa na benki kuu ya taifa (BOT).

Pia Kuna hatifungani za makampuni ambapo unaweza kuikopesha kampuni fedha zako kwa makubaliano hayohayo Kama unayoyafanya kwa serikali.

Sasa CRDB mzigo Flexi. Nadhani itakuwa flexible Ila wamefupisha 😂😂 ni hatifungani ila za kampuni.

Tofauti kati ya hisa hatifungani

Jamani jamani! Ambao hamjasoma kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE mnakosaa mengi. Niseme nisiseme!

Tofauti kubwa iliyopo Kati ya hisa na hatifungani ni kwamba ukinunua hisa za kampuni fulani, wewe unakuwa ni sehemu ya mmiliki wa kampuni husika.

Lakini ukinunua hatifungani, unaikopesha kampuni. Kuna tofauti kubwa hapo.

Hiki kitu kinamaanisha kuwa endapo kampuni itafilisika Kama wewe ni mmiliki wa hisa kwenye Kampuni, hutapata chochote maana wewe mwenyewe ni mmiliki wa ile kampuni iliyopata hasara.

Ila kama umeikopesha kampuni (umenunua hatifungani), hiyo ni stori nyingine kabisa.

Yaani, kampuni itakazimika kuuza rasilimali zake zitakazokuwa zimebaki Kama majengo na uwekezaji mwingine ili kukulipa wewe.

Any way, sasa baada ya kueleza hayo yote kwa kina ndio sasa nataka nikueleze nilivyomjibu yule mtu wangu wa juzi.

Kumbuka aliuliza

Niweke Fedha zangu benki Kama akiba au niwekeze kwenye CRDB Mzigo Flexi ?
Yule mama aliendelea kuniambia kuwa alikuwa na milioni kama tatu hivi na ile fedha alikuwa anaiweka kwa ajili ya mwanae ambaye yupo darasa la saba sasa.

Nilimwambia hivi, kulinganisha na riba inayotolewa kwenye akaunti za benki, hata kama ni akaunti ya mtoto, ni vigumu sana kupata riba ya asilimia 9 kwa mwaka. Ikizidi sana, sana, itakuwa asilimia nne. Hapo imezidi.

Ila kwa riba ya asilimia 9 ukilinganisha na akaunti ya kawaida ya benki Ni Bora tu kuweka fedha zako huku utakapopata riba ya asilimia 9.

Nikaweka kituo. Nikamwambia achukue kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Baada ya dakika tano tu, nikaona Mpesa inasoma hivi

9ES67XC1Z imethibitishwa mnamo tarehe 27/5/22 1:23 PM, toa 30,000 kutoka kwa…

Alikuwa ametuma fedha kwa ajili ya vitabu viwili. Kwanza ni kitabu Cha NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA na
ebook ya MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE pamoja na nauli ya kumtumia kitabu.

Sasa hivi anaendelea kusoma vitabu vyake.

Ebu na wewe hakikisha unapata nakala laini ya kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE kwa 5,000/- tu. Tuma fedha kwa 0755858391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

Kumbuka hiki ni kitabu pekee kitakachokufundisha wewe uwekezaji kwenye HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE kwa namna ambayo hujawahi kujifunza.

Naamimi sasa umeelewa CRDB mzigo Flexi ni Nini na tofauti take na akiba ya kawaida.

Pata nakala yako, wasiliana na 0755848391


One response to “Niweke Fedha zangu benki Kama akiba au niwekeze kwenye CRDB Mzigo Flexi?”

  1. Ama kweli wewe Godius Rweyongeza msimulizi mzuri. Nimetoka kusoma makala yako hadi mwisho bila kigugumizi. Big up!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X