Month: May 2022

  • Audiobook ni nini?

    Audiobook ni kitabu kilichosomwa. Yaani, kitabu kilekile ambacho ungekaa chini na kukisoma kwa siku au wiki. Zamu hii kinakuwa kimesomwa na kuwekwa kwenye mfumo wa sauti. Hivyo, unaweza kukisikiliza popote pale ulipo. Muda mwingine unaweza kukuta majukumu yamekubana, hivyo ukasikiliza audiobook vizuri tu bila ya shida yoyote wakati unaendelea na majukumu yako mengine kama kufua,…

  • Huu Ndio Ulevi Pekee Ambao Unapaswa Kuwa Nao

    Rafiki yangu mpendwa, najua umekuwa unasikia kuwa ulevi ni noma! Ulevi ni hatari. Mimi mwenyewe siyo kwamba napinga hili. Hapana, nakubaliana nalo kwa asilimia zote, ukweli ni wamba ulevi ni hatari kwa afya yako. Watu wanajiiingiza kwenye aina mbalimbali za ulevi. Kuna ambao wanaingia kwenye ulevi wa pombe, wengine madawa ya kulevya, wengine mitandao ya…

  • Niweke Fedha zangu benki Kama akiba au niwekeze kwenye CRDB Mzigo Flexi?

    Juzi kuna mtu alinipigia simu. Alikuwa ameniakiliza kupitia TEMINO YA CLOUDS FM. Swali lake lilikuwa moja tu na hakuwa na kitu kingine cha ziada Alitaka kujua kipi ni Bora, Kati ya kuweka fedha yake benki au kuwekeza kwenye CRDB Mzigo flexi! Unajiuliza kwani CRDB MZIGO FLEXI ni nini? Huu ni aina ya uwekezaji ambapo unaikopesha…

  • Tofauti Ya Thamani Ya Hisa Na Bei Ya Hisa

    Habari ya leo. Siku ya leo ningependa kujibu swali la mtu mmoj amabye amesoma kitabu changu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE. Anauliza swali hivi, samahani kuna kitu sijakikujua hapo, tofauti kati thamani yahisa na bei ya hisa Kwa hiyo hapa kitu cha kujibu ni je, thamani ni nini? na bei ni…

  • Kama Wewe Ni Shabiki Wa Yanga au Simba Hakikisha Umesoma Hapa

    Jana ilikuwa ni mechi ya simba na Yanga. Ni moja ya mechi zinagusa watu wengi kwa hapa Tanzania. Kuna watu hawashabikii timu yoyote ile hapa duniani, isipokuwa simba au Yanga. Sasa leo nilikuwa nikifikiri kuhusu hili nikawakumbuka rafiki zangu ambao wanahangaika kuandika vitabu. Wanahangaika na hawajui kitu gani wanaweza kuandikia. Nikasema ngoja leo niwaambie kitu.…

  • Mtaka cha uvunguni

    Leo nimemkumbuka jamaa mmoja niliyesoma naye shule ya msingi na baadaye sekondari. Huyu jamaa alikuwa anapenda maisha mazuri sana, ila alikuwa hataki kufanya kazi ili kuyapata hayo maisha mazuri. Alikuwa anapenda kufanya kazi kwenye ofisi nzuri ila alikuwa hapendi kupitia kwenye ule mchakato wa kumfikisha kwenye hiyo ngazi. Hivi kweli kitu kama hiki kinawezekana kweli…

  • Hii ni kazi anbayo huwezi kuajiri mtu kuifanya kwa niaba yako

    Unaendeleaje rafiki yangu wa ukweli. bila shaka kila kitu kinaenda vizuri upande wa huko. Siku ya leo ningependa nikujuze kazi mbili ambazo huwezi kumwajiri mtu kuzifanya kwa niaba yako. Na kazi hizi siyo nyingine bali ni Moja kufikiri. Hiki ni kitu ambacho huwezi kumwajiri mtu ili akifanye kwa niaba yako. Badala yake ni kwamba unapaswa…

  • Mapambano yanaendelea!

    Kwenye Moira wa MIGUU, timu huwa haishindi wa kufunga goli dakika ya kwanza. Hata timu ukifunga goli dakika ya kwanza. Bado huwa haitangazwi Kuwa imeshinda. Badala yake Ni mchezo huwa unaendelea mpaka dakika ya 90. Na wewe fahamu kuwa mapambano yanaendelea. Hujafaulu kwa sababu ushindi wa muda mfupi uliopata. Huu ushindi huo wa muda ukupe…

  • Kiongozi ni mtu wa aina gani?

    Kwa watu wengi akitajwa kiongozi au mtu yeyote yule anayeitwa kiongozi basi wanafikiria kwamba kiongozi ni mtu mwenye cheo. Kama rais, waziri, mkurugenzi au cheo chochote kikubwa. Kama hauna cheo wewe siyo kiongozi. Ninachoweza kusema hapa ni kwamba watu wanachanganya kati ya cheo na uongozi. unaweza ukawa na cheo ila ukawa siyo kiongozi. Na unaweza…

  • Uchambuzi wa kitabu cha Think And Grow Rich (Mambo 50 Ya Kujifunza)

    Kitabu: THINK AND GROW RICHMwandishi: Napoleon HillMchambuzi: Hillary Mrosso Whatever your mind can conceive and believe it can achieve. Mafanikio yote yanaanzia kwenye mawazo, na ukiyaamini mawazo yako na kuyafanyia kazi utayaona mafanikio yako. Mafanikio mara zote yanakuja kwa wale wanaofikiria mafanikio kwenye fikra zao au mawazo yao. Mwandishi wa kitabu hiki ni Napoleon, ambaye…

  • Jinsi Ya Kufanikisha Ndoto Zinazohitaji Fedha Nyingi

    Kwenye video ya leo kupitia channel yetu ya YouTube nimeeleza kwa kina ni namna gani unaweza unaweza kupata na kutunza fedha ya kukusaidia Kufanikisha ndoto yako kubwa. Je, upo tayari kwa ajili ya hiki? Ebu tazama video yenyewe hapa Hakikisha umejiunga na mfumo wetu wa kupokea makala maalumu kikashani mwako kwa kujaza taarifa zako hapa…

  • Huu ndio utaratibu mzuri ambao unapaswa kuujenga kuanzia mwezi huu

    Moja ya sifa ya watu wanaofanya makubwa kwenye hii dunia ni tabia ya kujifunza. Hii ni tabia moja muhimu ambayo inaweza kukusaidia wewe kufanikisha mambo makubwa kwenye hii dunia. Kama bado unajiuliza ni kwa jinsi gani kusoma kunaweza kukusaidia wewe, chukua hatua. Utoe mwaka mmoja ambapo utajifunza kila siku. Kisha linganisha huo mwaka na miaka…

  • Sababu Moja Kwa Nini unapaswa kuandika kitabu chako Leo

    Rafiki yangu wa ukweli Karibu kwenye makala ya jumapili ya leo. Leo ninataka nikwambie kwa nini unapaswa kuandika kitabu chako kuanzia leo hii. Naikumbuka siku za nyuma niliwahi kuandika (SABABU 18 Kwa Nini Tunaandika Vitabu na Tutaendelea Kuandika Vitabu, Na Kwa Nini Wewe Unapaswa Kuandika Cha Kwako) Ninachofanya leo ni kukuongezea nyama kwenye kile ambacho…

  • Baadaye siku ya leo, nitakuwa CLOUDS FM nikiongelea Gharama za Kulipa ili kufikia ndoto zako

    Helo upande wa huko. Godius Rweyongeza hapa na leo nina taarifa fupi tu kwako. Taarifa hii ni kwamba baadaye siku ya leo nitakuwa CLOUDS FM, Kwenye kipindi Cha TEMINO.Mada nitakayozungumzia Ni GHARAMA ZA KULIPA ILI KUFIKIA NDOTO ZAKO Kipindi hiki kinaendeshwa na Harris KAPIGA pamoja na adv. Henry Mwinuka. Muda wa kipindi ni saa 9…

  • Hii Ndio Aina Bora Uwekezaji Unayoweza Kufanya. Hakuna Uwekezaji Wenye Manufaa Kama Huu

    Moja ya kitu ambacho watu wanatafuta na wangependa kupata maishani mwao ni uwekezaji mzuri. Najua na wewe unasoma hapa kwa sababu unataka uwekeze fedha zako sehemu ambayo itakupa faida kubwa. Sasa siku ya leo nataka nikwambie eneo zuri ambalo wewe mwenyewe unaweza kuwekeza na kupata faida. Kwa siku sasa nimekuwa nikikwambia maeneo ya kuwekeza na…

  • Usifurahie kitu hiki kwenye maisha yako

    usifurahie kuitwa mnyonge. Hivi umewahi kujiuliza unyonge wako uko wapi? Sasa kwa nini watu wanakuita mnyonge na muda mwingine wanasema kwamba, wanakutetea wewe. Sikiliza, pambana kwa hali yoyote ile kuhakikisha kwamba wewe hauwi mnyonge. Kwa asili ni kwamba vitu vinyonge huwa havidumu. Sisi wenyewe hatupendi tukae na vitu vinyonge. Mfugaji wa ng’ombe hawezi kukaa na…

  • Leo ndiyo siku ya mwisho ya kupata kitabu cha jinsi ya kufikia ndoto zako kwa bei ya ODA

    Habari ya upande wa huko rafiki yangu. bila shaka unaendelea vyema kabisa. Nimekuwa nikikutaarifu kuwa leo ni siku ya uzinduzi wa kitabu cha jinsi ya kufikia ndoto zako. kitabu hiki cha kipekee kimeeleza kwa kina, jinsi gani unaweza kugundua ndoto zako na kuzifanyia kazi mpaka zikatimia. Hivi umeshajiuliza swali ee! Kwa nini natumia neno ndoto…

  • KUHUSU KITABU: NGUVU YA VITU VIDOGO KUELEKEA MAFANIKIO MAKUBWA

    Hivi umewahi kujiuliza kuwa vitu vidogo vinaweza kukusaidia kitu gani maishani mwako? Mara nyingi sana watu huwa wana ndoto kubwa na malengo makubwa ya kufikia kifedha, kimahusiano, kibiashara au kikazi. Lakini cha kushangaza ni kwamba huwa hawafanyii kazi hizo ndoto kubwa walizonazo bali huwa wanasubiri itokee siku moja ya muujiza ambapo ndoto yao itatimia kwa…

  • JINSI YA KUANZA UPYA BAADA YA KUANGUKA

    Huwa inatokea mtu anaanza kitu unakikuza lakini inafikia hatua ambapo unapata anguko na kurudi chini. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kuanguka, ikiwa ni pamoja na kupumzika kwa nguvu baada ya kuwa umefika juu. Au inaweza kutokana na sababu kuwa mwanzoni ulikuwa na lengo kubwa, ila baada ya kuwa umefikia juu au baada ya kuwa umefikia…

  • Unafanyaje ili kupata mbia sahihi wa biashara

    Leo nataka tuongeelee kuhusu ubia wa biashara. Ikiwa ni moja ya kitu muhimu sana kwenye biashara ambacho unakihitaji hasa kama umelenga kufika mbali. Ubia kwenye biashara unakutanisha watu wenye ujuzi, elimu na hata fedha ambapo wanaungana kutengeneza kitu kimoja. Kwenye biashara ubia ni muhimu sana hasa kama unataka kufika mbali. Kitu kikubwa unachohitaji kujua kuhusu…

X