Una Uwezo Mkubwa Ndani Yako


Kwenye Biblia kuna hadithi ya watu watatu waliopewa talanta. Mmoja alipewa tano, wa pili alipewa mbili na mwingine alipewa talanta moja.

Aliyepewa talanta moja hakuithamini, na wala hakuitumia kufanya kitu chochote cha maana. Binafsi sipo hapa kukwambia hiyo stori, naamimi kuwa utakuwa unaijua vizuri tu, au la utaenda kuisoma baada ya hapa.

Kitu kikubwa ninachotaka kusema leo ni UKUBWA WA KILE AMBACHO KILA MTU ALIKUWA AMEPEWA. Na ukubwa wa kile ulichonacho wewe.

Ukijua ukubwa wa talanta moja, utagundua kwamba hata jamaa aliyepewa talanta moja alikuwa amepewa kitu kikubwa sana.

Kulingana na mtandao wa Wikipedia; talanta moja ni sawa na dola 4080 za Kimarekani ambapo zikiwekwa kwenye fedha za Tanzania ni sawa na shilingi milioni tisa na laki nne, sitini na nane elfu.

Kumbe talanta moja hakikuwa kitu kidogo, kama kinavyoelezwa…
Kama ni mtaji basi jamaa alikuwa amepewa mtaji mkubwa tu. Japo jamaa hakuitumia…..
Najaribu tu kufikiri, wewe ukipata hata hako ka talanta kamoja, yaani ukipewa shilingi milioni tisa keshi…Hivi wewe ninavyokujua kweli utatulia…..

Hiki kitu kitupe funzo kubwa kwenye maisha yetu ya kila siku.

Kuna uwezo mkubwa tulio nao ndani yetu, tuutumie vizuri.  Usipoutumia uwezo wako vizuri, utaishia kulalamika kuwa hukupewa kitu …

Kumbe huyu jamaa wa talanta moja alipewa kitu kikubwa ila sasa hakukitumia… Sawasawa na wewe, una kitu kikubwa ndani yako, swali je, unakitumia??

Kuna watu wengi ambao huwa nakutana nao wakilalamika kuhusu maisha. Mfano, unaweza kukuta mtu analalamika kuhusu mtaji, lakini ukifuatilia kiuhalisia huyu mtu shida yake siyo mtaji.

Shida yake ni kwamba hathamini like kidogo alichonacho. Haamini kwamba hicho kidogo, kinaweza kugeuzwa na kukuzwa mpaka kikawa kikubwa.

Ebu fikiria kitu kama mbegu ya mhindi. Najua nikisema hii mbegu watu wengi watanielewa kuliko nikisema mbegu ya haladali ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚…

Ukipanda mbegu moja ya mhindi. Ikiota haitoi tunda lenye mhindi mmoja. Inatoa gunzi lenye mahindi ya kutosha. Yale mahindi ukiyapanda, hayatoki yenyewe kama yenyewe yanatoka na mahindi mengine zaidi….

Kwa hiyo ukianza Januari mosi na mbegu moja. Ukaipanda ukaipalilia, na kuimwagilia na baadaye kuvuna…

Halafu ukapanda tena zile mbegu ulizovuna na kurudia mchakato.

Mpaka unafikia disemba 31… Mbegu moja, ina uwezo wa kuwa imezalisha magunia ya kutosha….

Lakini ukiidharau hiyo mbegu moja, yenyewe itaishia kuharibika…

Hiki kitu kihusishe na uwezo wako…
Uwezo wako unaweza kuwa unaudharau kuwa ni kidogo, ila ukianza kuutumia. Uwezo huu utashangaa kwamba uwezo huu unazidi kukua na kuongezeka na hata unakufikisha mbali…..

Wachungaji wakiwa wanahubiri, wakiongea pointi, huwa unasikia wanasema. Naamimi naongea na mtu hapa….

Sasa na mimi naamimi naongea na mtu ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

Mpaka wakati mwingine
Mimi ni Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE
0755748391
Morogoro-Tz


5 responses to “Una Uwezo Mkubwa Ndani Yako”

  1. Be blessed Mr Godius hakika kuna kitu unanifundisha mdogo mdogo maana sikuwa na tabia japo ya kusoma hata mstari mmoja but now days am able to read one page

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X