Ufanyeje unapokuwa unasoma vitabu huku unasahau?


Unaendeleaje rafiki yangu, juzi kuna mtu aliniambia kwamba anapenda kusoma vitabu, ila sasa tatizo lake ni kwamba akisoma anasahau alichosoma kwenye kitabu na hata kabla ya kumaliza kusoma kitabu husika.

Kitu hiki ndicho kimeniweka hewani siku ya leo nili niweze kukiandikia maana najua kuna watu wengi pia ambao wanapata shida hii.

Kwanza ninachopenda kusema ni kwamba kama unasoma na unasahau, usiache kusoma vitabu. Endelea hivyo hivyo bila kuacha.

Usitake kuona matokeo kwa siku moja. kuna kitu kinaitwa riba mkusanyiko. Yaani, vitu vidogovidogo vinakusanyika kutengeneza kitu kimoja kikubwa. Unaweza leo hii usione matokeo ya kile unachosoma, ila kumbe yanakusanyika na siku moja katika hali ambayo hutegemei, ukapata matokeo ya tofauti.

Kwa hiyo, kama unasoma vitabu na unasahau, usiache kusoma endelea kusoma.

Kitu cha pili, baada ya kuwa umesoma kitabu, jiulize ni kitu gani kimoja ambacho nimetoka nacho kwenye hiki kitabu? Ni kitu gani kimoja? Usitaka kuondoka na kila kitu kwenye kitabu. Wewe ukipata kitu kimoja tu kutoka kwenye kitabu na hicho kitu ukakifanyia kazi. inatosha.

Kwa mfano, ukisoma kitabu kuhusu fedha na uwekezaji. Toka na kitu kimoja kama kuweka akiba kila unapopokea mshahara wako. Hicho kitu kifanyie kazi. raha ya vitabu ipo kwenye kufanyia kazi kile ulichojifunza na siyo kwenye kusoma tu.

Kwa sasa hivi sina la ziada

Mimi naitwa Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE

Tuwasiliane kwa 0755848391

Baruapepe yangu ni GodiusRweyongeza1@gmail.com

NB. Kama umependa makala hii, utapenda makala zangu za kipekee ninazotuma kwa njia ya barua pepe. WEKA JINA LAKO Na BARUA PEPE YAKO hapa chini ili niweze kukutumia taarifa zako.


One response to “Ufanyeje unapokuwa unasoma vitabu huku unasahau?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X