Njia Mpya Ya Kujenga Tabia Kwa Haraka


Leo nataka nikwambie kitu kikubwa ambacho kitakusaidia wewe kuweza kujenga tabia mpya kwa haraka. Ebu fikiria tabia yoyote ile ambayo ungegependa kujenga miashani mwako. Ni tabia gani nzuri ambayo kwa siku umekuwa unatamani kuwa nayo?

Je, ni kusoma vitabu?

Je, ni kuandika

Je, ni kufanya mazoezi?

Au kuweka akiba?

Ni kitu gani haswa unataka uwe nacho ila sasa umekuwa unashindwa?

Je, ni kuboresha na kujenga mahusiano mazuri na mwenza wako?

Leo nataka nikwambie hivi. unaweza kujenga tabia mpya au kufanya kitu chochote kile ulichokuwa unatamani kufanya maishani mwako kwa kutumia kanuni ndogo tu ya dakika mbili.

Na dakika mbili siyo dakika nyingi sana rafiki yangu.

Ebu kwa mfano sasa hivi unavyosoma hapa. chagua kitu kimoja ambacho ungependa kufanyia kazi kisha kifanyie kazi sasa hivi unavyosoma hapa. acha kwanza kusoma hapa kifanyie kazi kisha urudi kumalizia.

Unaona eeh.

Badala ya kubaki na ndoto kubwa ya kuwa mwandishi na kuendelea kutamani kuwa mwandishi, kaa chini uandike ndani ya dakika mbili. ukiandika sentensi mbili. zinatosha na ni za kwako. Kesho utaongeza nyingine mbili na kesho kutwa utaongeza nyingine mbili. ukiweza kuandika kwa mwaka mzima, siyo siri hizi dakika mbili zitakusaidia hata kuandika kitabu kikubwa tu.

Bado unabisha tu. Ebu fanyia kazi hii kanuni ya dakika mbili kwa mwezi huu mmoja tu halafu utanipa mrejesho.

Kama ni mazoezi badala ya kusubiri upate masaa mawili ya kufanya mazoezi. Amka sasa hivi nenda hapo mbele ya uwanj na ufanye mazoezi ndani ya dakika mbili tu. au unaweza kufanyia hata hapo chumbani kwako kwa dakika mbili tu. dakika mbili siyo nyingi na wewe huwezi kushindwa kufanyia kazi kitu kwa dakika mbili tu.

Kama ni kuboreshamahusiano yako, tumia kanuni hii hii ya dakika mbili. tumia dakika mbili kuandika vitu viwili unavyopenda kwa mwenza wako. Kushukuru kwa kizuri alichokufanyia na hata kuongea naye.

Unaona eeh. Dakika mbii siyo nyingi sana, na zinaweza kukusadia wewe kufanya makubwa.

Ikitokea umepanga kufanyia kazi kitu fulani ila mzuka ukapanda ukakifanya kwa dakika zaidi ya hapo, basi. Ila hata mzuka usipopanda ukitumia hizo dakika mbili tu. inatosha.

Nadhani hata hii makala umeisoma kwa dakika mbili. kama siyo basi, maana mwenyewe nilidhamiria uisome kwa dakika mbili tu.

Tukutane wakati mwingine

Ni mimi

Morogoro-Tz

0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X