Jinsi Ya Kubadili Mwelekeo Wa Kile Umachofanya Bila Kuathiri Matokeo (True Story)


Leo nimeikumbuka stori ya Sixto Rodriguez. Huyu ni mwanamziki wa kimarekani ambaye mwaka 1967 alirekodi wimbo wake wa kwanza. Na miaka mitatu baadaye ilikuja kurekodi albamu ambayo ilikuwa inajulikana kwa jina la cold fact.

Mwaka mmoja baadaye alirekodi albamu nyingine ambayo ilikuwa ikijulikana kama coming from reality. Hata hivyo, hizi albamu zake hazikufanya vizuri sana kiasi kwamba ile label yake iliyokuwa imemsajiri iliamua kuachana naye. Kipindi hicho alikuwa katika harakati za kurekodi albamu nyingine na alikuwa tayari amerekodi nyimbo tatu. 

Kwa hiyo hicho kitu kilimfanya aachane na muziki huku akianza kujishughulisha na kazi nyingine za kawaida nyumbani kwao. Taratibu alipotea kwenye chati ya mziki wa Marekani.

Ilitokea kwamba kulikuwa na binti ambaye alienda kumwona mchumba wake Afrika kusini. Akawa ameenda na albamu ya Rodriguez AFRKA KUSINI

Akiwa huko wakawa wanacheza nyimbo za Rodriguez na watu wakaanza kuzikubali. Ghafla albamu yake ilikuwa miongoni mwa albamu zenye  uhitaji mkubwa zaidi Afrika kusini. Hii ilitokana na ukweli kuwa miongoni mwa nyimbo zilizokuwa kwenye albamu ya Rodriguez zilikuwa za kiharakati, halafu kipindi hicho nchi ya Afrika kusini ndio ilikuwa kwenye harakati za ukombozi wa mtu mweusi.

Hivyo ilibidi shirika moja lianze kuchapa na kusambaza nyimbo  zake kulingana na uhitaji wake. Kutokana na umaarufu wa nyimbo zake watu waliamua kumtafuta mwanamziki huyo ili aweze kuja Afrika kusini kufanya show kwa mashabiki wake wa muziki. Hata hivyo hakuna mtu aliyekuwa anajua habari zake. Baadaye ilikuja kusambaa miongoni mwa watu kwamba mwanamziki huyu alijiua baada ya albamu zake kutofanya vizuri.

Lakini mwanahabari mmoja hakuamua kuchulia kitu hiki kama kilivyokuwa kinasambazwa na watu. Hivyo aliamua kuanzisha tovuti ambayo lengo lake lilikuwa ni kumtafuta mwanamziki huyu tu. Siku moja mtoto wa Rodriguez akiwa anapita mtandaoni aliona hiyo tovuti ambayo ilikuwa imelenga kumtafuta mwanamziki huyo. Aliandika pale kwenye ile tovuti kwamba Rodriguez ni baba yangu, na ninamaanisha hilo. Akawa ameacha mawasiliano yake. Baadaye alipigiwa simu na mipango ya Rodriguez kwenda Afrika kusini ilifanyika. 

Habari zilisambaa sana kwamba legendari wa mziki alikuwa hai na alikuwa anakuja Afrika kusini. Watoto wa Rodriguez walikuja na baba yao ila hakuna mtu hata mmoja aliyekuwa anatazamia kukutana na watu wengi kwenye hiyo show. Sio hata Rodriguez mwenyewe.

Ila cha kushangaza walipofika Afrika kusini walishangaa kukuta watu 5000 na tiketi zilikuwa zimeuzwa zote na kuisha. Rodriguez aliposimama kwenye jukwaa alishangiliwa na watu waliokuwepo kwa dakika 10 mfululizo (10 minutes standing ovation).

Kumbe umaarufu wake Afriks Kusini ulikuwa ni mkubwa sana kuliko mtu msanii mwingine nchini Marekani. Na alikuwa tayari ameuza nakala za albamu yake kuliko wasanii maarufu wa kipindi hicho kama Bob Dylan na Cat Stevens.

Nyimbo za Rodriguez zinatupa picha ya jinsi kitu kinaweza kukataliwa nyumbani, lakini kikaja kukubalika ugenini, kisipokubalika leo hii basi kinakuja kukubalika kesho. Lakini ili kiweze kukubaliwa utapaswa kuhakikisha umekifanya na kukimaliza.

Lakini pia ni funzo kubwa kwamba usikate tamaa mapema. Kuna wakati unapaswa kubadili mwelekeo kwa sababu kule ulipokuwa umeleekeza mwanzoni siyo sehemu sahihi. 

Naipenda sana hii picha ya mvuvi. Huyu jamaa, baadaye anaweza kukata tamaa, lakini kumbe issue hapa siyo kukata tamaa, issue ni kubadili mwelekeo kidogo tu na mambo mengine yote yakakaa sawa.

Kwa Rodriguez muziki wake haukubalika nchini mwake. Lakini, kumbe kuna sehemu muziki wake ulikuwa unahitajika. Kazi yako kubwa ni wewe kujua wapi watu wanahitaji kazi zangu.

Kazi yako ni kusoma mazingira ili ukiweka chambo, samaki wanase.

Anyway, leo vipi? Angalia hii video yangu hapa youtube kisha usubscribe.

Mpaka wakati mwingine. Mimi ni Godius Rweyongeza kutoka SONGAMBELE

0755848391

Morogoro-Tz


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X