Mafanikio ni nini?


Kwa mwanafunzi mafanikio yake ni kufaulu mtihani.
Kwa mwanachuo mafanikio yake yanaweza kuwa kupata kazi baada ya kuhitimu.
Kwa aliyepata ajira mafanikio kwake yanaweza kuwa ni  kupandishwa cheo au kuoa/ kuolewa au kuanzisha biashara au kujiajiri.

Hivyo, hakuna maana moja ya mafanikio ambayo inaweza kuwekwa kama maana ya kimataifa ya mafanikio

Maana ya mafanikio unajipa mwenyewe. Wewe mwenyewe unapaswaa kujipa maana ya mafanikio.

Jua ni kitu kipi ukikifanya au ukikikamilisha kinakuwa kinaashiria kuwa umefanikiwa?

Lakini pia kitu kingine unapaswa kujipa orodha ya vitu ambavyo utavifanya maishani.
Orodhesha vitu ambavyo unataka ufanikishe au ufikie.
Kwa mfano orodha yako inaweza kuwa na vitu kama
Gari utakalomiliki
Nyumba
Mwenza wako
Sehemu utazotembelea kabla ya kufa
Vitu utakavyofanyia kazi kabla ya kufa n.k.

Kwenye kitabu chake cha Who Will Cry When you Die, Robin Sharma anashauri uandike vitu 101 utakavyofanyia kazi kabla ya kifo chako. Na hivi ndivyo vitabeba maana yako ya mafanikio.

Hata hivyo hivi vitu visibebe furaha yako kwa kutaka kuvifanikisha. Bali wewe ufurahie ule mchakato wa kufanikiwa zaidi na kwa kuvifanyia kazi.

MAKALA NYINGINE ZINAZOENDANA NA HII:


2 responses to “Mafanikio ni nini?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X