Kwa Nini Watu Wengi Na Hasa Vijana Wanashindwa Kuzifikia Ndoto Zao


 

Juzi niliomba watu wapendekeze mada ambazo nitaandikia kwenye blogu yangu kupitia status yangu ya whatsap. Nilipokea maombi kadha wa kadha ambayo nitakuwa nayafanyia kazi moja baada ya jingine. Ombi mojawapo lilikuwa ni kuandika makala maalumu kueleza kwa nini watu wanashindwa kufikia NDOTO zao.

Kabla sijaenda mbali nataka ufahamu kuwa tayari nimeandaa makala nyingi kuhusu ndoto na jinsi unavyoweza kufikia NDOTO zako. Makala zote hizo nitajidi kuzihusisha kwenye makala ya leo ili uweze kurejea na kuzisoma.

Lakini pia nimeandika kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Unaweza kupata kitabu hiki kwa kuwasiliana na 0755848391 utatumiwa popote ulipo duniani.
Natamani sana siku moja nikuone ukiwa umeweza KUFIKIA NDOTO ZAKO KUBWA

kupata kitabu hiki wasiliana na 0755848391. Utatumiwa popote ulipo duniani

1. KINACHOKUKWAMISHA kufikia ndoto zako ni kuchelewa kuchukua baadhi ya hatua.

Ulipaswa kuwa umechukua hatua fulani ila sasa unachelewa aidha kwa kutoelewa au kwa kuelewa na kupuuza, au kwa uoga.

Mfano, kwenye ulimwengu wa sasa ulipaswa kuwa umeweka biashara yako au kipaji chako mtandaoni, ila hujafanya hivyo.

Na haikugharimu chochote. Kwa bando lako tu unafungua na kuendesha blogu yako, unatengeneza akaunti za biashara kwenye mitandao ya kijamii na mengine mengi.

Ulipaswa kuwa unatunza kumbukumbu za hesabu za mapato na matumizi ya biashara yako, ila hufanyi hivyo, halafu ukija unasema kwamba biashara ni mbaya.
Kwani inakugharimu wewe shilingi ngapi kufanya kitu kama hiki.

Kuna baadhi ya hatua unachelewa kuzichukua, na hapo unakuwa unakwama kufikia ndoto zako.

2. Kutaka kuishi maisha kama ya wengine wakati una ndoto kubwa

Unapokuwa na ndoto kubwa matumizi yako, mwenendo wako, ulaji wako na mambo mengine yote yanabadilika.

Huwezi kuwa na ndoto ya kuwa mkimbiaji wa Marathon ukawa hufanyi mazoezi huku ukila chipsi kila siku. Vitendo vyako vinapaswa kuendana na ndoto yako.

Kuna vitu bila kulazimishwa wala kuambiwa na mtu yeyote utapaswa kuachana navyo, sio kwa sababu ni vibaya ila tu kwa sababu havieneani na ndoto zako kubwa.

Huwezi kuwa na ndoto za kuwa bilionea huku ukiwa unataka kumhonga kila binti anayepita mbele yako.


3. Hujafanya uamuzi wa dhati wa kuzifikia NDOTO ZAKO.

Ngoja nikwambie kitu, kuna uamuzi unapaswa kuufanya kwenye maisha yako. Na uamuzi huu ni au utazifikia ndoto zako au utakufa ukiwa ukiwa unazipambania au hutazifanyia kazi kabisa ndoto zako.

Hapo unapaswa KUCHAGUA maana maisha ni kuchagua.
Ukichagua kuzifanyia kazi ndoto, fahamu kuwa umechagua kitu kigumu ila kinachowezekana.

Kama ndoto ingekuwa ni barabara basi ni sawa na kuchagua barabara mbaya, yenye makorongo ila inayokufikisha ikulu.
Nadhani umewahi kusikia kuwa mlango wa kuingia mbinguni ni mwembamba, hivyohivyo mlango wa kufikia ndoto zako. Haupitiki mara kwa mara ndio maana watu wengi kwenye jamii yako wameamua kuishi maisha ya kawaida.

Mwaka 1968 kwenye mbio za marathon; mshiriki mmojawapo alikuwa ni Mtanzania John Stephen Akhwari

Mtanzania John Stephen Akhwari kwenye mbio za marathon mwaka 1968.

Mtanzania huyu naweza kusema siku hiyo alikuwa miongoni mwa watu waliotegemewa kushinda. Hii ni kutokana na rekodi yake ya mashindano ya nyuma likiwemo moja la olimpiki na jingine la jumuia ya madola ambayo alikuwa amefanya vizuri sana.

Sijui kama kubeti kulokuwepo miaka hiyo, ila kama vijana wa siku hizo wangekuwa wa kubeti, basi siku hiyo wangempa ushindi wote JOHN STEPHEN AKHWARI.

Alianza mbio kama ambavyo watu wengine walikuwa wameanza. Baada ya kufikia kilomita kama thelathini hivi, aliumia na kupata maumivu ambayo kwa mtu wa kawaida yalitosha tu kumfanya asiendelee na mbio. Ila hali haikuwa hivyo kwa Bwana John Stephen Akhwari.

Alitulia pembeni kwanza. Alipewa huduma ya kwanza, kisha baada ya hapo akaendelea kusonga mbele. Zamu hii akiwa anajikongoja. Gari la kumbeba lililetwa ila alikataa kulipanda.

Wale ambao hawakuumia walimaliza mbio mapema na Mwethiopia siku hiyo ndiye alishindwa

Saa moja baada ya mashindano kuwa yamekamilika na watu wameanza kuondoka uwanjani pale, ndipo vyombo vya habari vilipata taarifa kuwa kuna mtu bado anakimbia.

KUMBUKA hapa watazamaji wengine wameshaondoka uwanjani na tuzo zilishatolewa. John Stephen Akhwari ambaye aliumia ndipo alikuwa anaingia.

Vyombo vya habari vilituma watu wao ili warekodi kinachoendelea. Walimwona John Stephen Akhwari alivyokuwa anachechemea ila akipambama kumaliza mbio. Na mwisho alimaliza huku akipigiwa makofi ma watazamaji wachache waliokuwepo pale uwanjani.

Alipoulizwa kwa nini uliendelea kukimbia wakati ulikuwa umeumia, alisema. Nchi yangu haikunituma maili elfu tano ili nianze mbio bali nimalize mbio.
Tokea hapo kauli hiyo imekuwa kauli inayotumika sana kwenye ulimwengu wa michezo kuwahamasisha wachezaji.

Ninachotaka utoke nacho hapa Ni kwamba, unapaswa kuamua kwa DHATI kuifanyia kazi ndoto yako au kutoifanyoa kazi kabisa. Ila hakuna kitu cha katikati

Kwa Leo naishia hapo. Kuna makala nyingi za nyuma ambazo nimewahi kuandika kuhusu mada hii. Nimeziunganisha kwenye makala ya leo. Naomba UBONYEZE viunzi husika ili uweze kuzisoma.

Mimi naitwa
GODIUS RWEYONGEZA
0755848391
MOROGORO

 

[block rendering halted]


One response to “Kwa Nini Watu Wengi Na Hasa Vijana Wanashindwa Kuzifikia Ndoto Zao”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X