Kwa nini unapaswa kuanzisha biashara


1 zama zimebadilika

Mambo yanabadilika aisee! Zamani ulikuwa hivi, ulitakiwa kwenda shule, kusoma kwa bidii ma baadaye ulikuwa na uhakika wa kupata ajira. Siku hizi mambo yamekuwa tofauti. Kuna watu wengi ambao wamehitimu na wapo mtaani ila kazi hawana. Kwa hiyo je, tuendelee kuwambia wanetu na washikaji zetu kuwa waende shule wasome kwa bidii ili waje wapate ajira. Inabidi tuseme ukweli kuwa ajira hakuna. Ila kuna njia mpya ya kuishi hapa mjini na njia hiyo ni kuanzisha biashara

Iko hivi, biashara ndio njia pekee ya kufika mbali iliyobaki kwenye zama hizi.

Kama unataka kufika mbali. Anzisha biashara.

2. Hakuna ukomo wa kipato.

Unapoajiriwa kuna na kiasi cha mshahara ambacho unapaswa kukipokea kila mwezi. Na kiasi hiki kinakuwa fixed. Kama ikitokea mshahara ukapandishwa basi ni baada ya muda mrefu wa wewe kuwa umefanya kazi.

Siku hizi hata ule ushauri wa kwamba ukiongeza elimu utaongezewa mshahara haufanyi kazi tena.

Ila kwenye biashara hakuna ukomo wa kipato hata kidogo, unaweza kuanzisha biashara na kuikuza biashara hiyo.

Kadiri itakavyokua ndivyo utapata kipato zaidi. Hapo Sasa ndipo unapaswa kuhakikisha una biashara.

3. Utajifunza mengi

Biashara inakufundisha mengi. Ukiwa kweye biashara unalazimika kujua mambo mengi Kama mauzo, masoko, namna ya kuajiri, na mengineyo. Kiukweli kwenye biashara unapata kujifunza mengi, Mambo ambayo usingeweza kujifunza kama ungekuwa umeajiriwa.

Maana ukiwa umeajiriwa  Mwajiriwa wako atakutaka ufanye kitu kimoja tu ambacho akiwa amelenga umletee matokeo fulani..

4. Utafanya unachopenda

Kazini utafanya kazi yoyote unayopangiwa. Ila biashara utafanya unayoipenda na hivyo muda wote na mara zote utakuwa unafanya unachopenda Unapokuwa kwenye biashara.

Kuna tafiti zimeripoti watu wengi kuaga dunia siku ya jumatatu kwa sababu tu wanafanya kitu ambacho wao hawapendi.

Tafitikama hizi hazipo kwa wafanya biasahra maana wengi wanafanya vitu ambavyo wao wenyewe wanapenda kufanya.

5. Utakuwa mchango mkubwa kwa jamii

Biashara yako itatatua matatizo ambayo yanawakumba watu, hivyo wewe utakuwa umewasaidia watu kupata suluhisho la tatizo lililokuwa linawasumbua.

Ebu fikiria mtu kama Steve Jobs aliyegundua simujanja. Alitatua matatizo ya watu wengi wengi Sana.

Leo hii tunaweza kuwasiliana na watu wa nje ya nchi bila tatizo au shida yoyote.

Na ukiangalia biashara zote kubwa zinatatua tatizo fulani ambalo linawakumba watu.

Google wanachofanya ni kutatua tatizo la watu kupata taarifa kwa wakati.

Facebook wanachofanya ni kuunganisha watu


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X