Kitu hiki tu kinakwamisha watu wengi Sana


Moja ya kitu ambacho kinakwamisha watu wengi kwenye kufanyia kazi malengo ni kutojiwekea viwango.

Unapaswa kuishi kwa viwango.

Kampuni huwa zinajiwekea viwango vya uzalishaji wa bidhaa zake. Na muda mwingine viwango hivi huwa vinaangaliwa na watu wa ndani ya kampuni na nje ya kampuni.

Kwenye kampuni unakuta kuna mkurugenzi anayehakikisha bidhaa zinazozalishwa ni bora. Wengine watamwita quality manager au majina mengine ila kazi ni yake ni kuhakikisha kazi ya mwisho inayozalishwa ni kazi ya viwango.

Huyu ni lazima tu atahakikisha kweli kila kitu kinazalishwa kwa ubora kwa sababu kuu zifuatazo.

Moja, bidhaa ikizalishwa kawaida, bosi wake akaigundua anaweza kumwachisha kazi.

Au la bidhaa imezalishwa kwa viwango vya kawaida imeenda kwa walaji wakalalamika, bosi atafuatilia na akagundua kuna uzembe ulifanyika, atamwachisha kazi.

Kwa hiyo huyu mkurugenzi lazima awe makini mara zote kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa ni za viwango Kama inavyotakiwa.

Na kitu kingine kinachoongeza umakini kwenye kazi hasa ni pale ambapo kunakuwa na wakaguzi kutoka nje.

Hiki Kitu kinamsukuma zaidi mkurugenzi husika na kampuni nzima kiujumla kuhakikisha kwamba wanazalisha bidhaa za viwango.

Wewe pia unapaswa kujiwekea viwango.

Unaweza usiwe na mkurugenzi wa kukufuatilia kuona kama viwango vimefikiwa au la! Ila sasa hiyo kazi unapaswa kujipa mwenyewe. Wewe mwenyewe unapaswa kuwa mkurugenzi wa ubora (quality manager) wa maisha yako.

Jiwekee viwango, kisha vifuate. Kama huwezi, tafufa mtu wa kukushikiria. Ambaye utaripoti kwake mara kwa mara, na yeye atakusaidia kuona Kama kweli umeweza kukidhi viwango au la!

Mimi naweza kukusaidia kwenye hilo.

Siku siyo nyingi nilijiwekea viwango vya kuandika makala mbili kila siku. Na viwango hivi nimeshaanza kuvifanyia kazi kwa zaidi ya wiki na nusu na nitaendelea kuvifanyia kazi kila iitwayo leo bila kuchoka.

Ila sasa nimekaa chini na kugundua kuwa napaswa kujiwekea viwango vipya na vya juu kuliko nilivyozoea kwenye kila eneo la maisha. Hivyo, leo nimejiwekwa viwango vingine kwenye maeneo mengine.

Nakusihi na wewe ujifanyie tathimini na kujiwekea viwango utakavyokuwa unafuata.

Unaenda kujiwekea viwango kwenye eneo gani la maisha?

Tutawasiliana
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz


3 responses to “Kitu hiki tu kinakwamisha watu wengi Sana”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X