Kinachokwamisha wewe kufika mbali.


Umekuwa unakwama kufika mbali kwenye maisha na kushindwa kufikia ndoto zako kwa sababu tu hujawa na ndoto  kubwa kiasi cha kutosha. Maneno ya busara yanasema hivi,

unapaswa kulenga kuifikia nyota kiasi kwamba hata ukishindwa uufikie mwezi.

Sasa ebu fikiria hili, wewe ndoto yako siyo kubwa kiasi cha kulenga kuifikia nyota badala yake umelenga kufika kileleni mwa mti, unadhani ukishindwa utaangukia wapi? Si utaangukia baharini?

Kuanzia Leo hii weka ndoto  zako kubwa Kisha anza kuzipambania.

Lakini pia labda niseme ndoto kubwa ndio njia pekee iliyobaki ya kuweza kuishi vizuri hapa duniani. Ndio hakuna njia nyingine .

Kama kikiwekwa chakula mezani na chakula kikawa ni kidogo, viumbe wenye nguvu ndio watakula na wale ambao hawana nguvu wataishia kujilamba midomo tu. Hali hiyo ikiendelea kwa muda mrefu ndio sasa unakuta viumbe ambao hawana nguvu wanakufa, wanabaki wale wenye nguvu tu.

Kwenye zama za sasa kuwa na ndoto kubwa limebaki kuwa ni hitaji la lazima (basic need).

Kwa nini? Kwa sababu ndoto kubwa ndiyo njia pekee ya wewe kuendelea kuishi kwenye ULIMWENGU wa leo.

Ebu wewe chukulia watu wote ambao unawafahamu wamefanya makubwa kwenye zama za sasa. Orodhesha hata watu 10 unaowafahamu. Hakuna hata mmoja mwenye ndoto ndogo au ndoto za kawaida. Wote wana ndoto kubwa.

Chukulia mtu kama,
Elon Musk na ndoto yake kubwa ya kwenda sayari za mbali.

Kwenye ulimwengu wa sasa kama unataka kufanya makubwa na basi kuwa na ndoto kubwa, Kisha zipambanie kila kukicha.

Kuwa na ndoto za  kuufikia uhuru wa kifedha
Kuwa na ndoto za kukuza kipaji chako kimataifa
Kuwa na ndoto kubwa haswa; Kisha Anza kuzifanyia kazi.

Rafiki yangu, kiufupi kuwa na ndoto kubwa.

Nakumbuka kuna mtu aliwahi kusema kuwa rafiki zangu ni watu wenye ndoto kubwa. Siwapendi wenye ndoto ndogo. Binafsi na mimi siwapendi wenye ndoto ndogo. Kama wewe una ndoto ndogo, bora tu usiwe rafiki yangu maana hata utanikwamisha mimi.

Utatoa nguvu hasi kwangu. Mimi nataka marafiki wenye ndoto kubwa na ambao wameamua kuwa watazifanyia kazi ndoto zao kubwa au la watakufa wakiwa wanazipambania.

Kina kila kitu, unachohitaji kujua kuhusu ndoto zako. Leo hii lipia 19800 upate nakala ngumu au elfu 10 upate softcopy.

Changamka sasa.


One response to “Kinachokwamisha wewe kufika mbali.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X