Jinsi ya kupata chochote unachotaka


Rafiki yangu habari ya leo. Bila shaka unaendelea vyema kabisa. Zig Ziglar aliwahi kunukuliwa akisema kuwa unaweza kupata chochote unachotaka kama utawasaidia watu kupata kile wanachotaka. Yaani, kauli hii fupi laiti ingefahamika kwa watu vizuri basi kila mtu alipaswa kufurahi maana kauli hii imebeba siri kubwa.

Kama hujajua siri iliyobebwa kwenye kauli hii naomba utulie ili mimi leo hii nifanye tu kukudavulia na kikuwekea mezani kila kitu.

Labda kwanza nikuulize ni kitu gani unataka? Ni vigumu kupata kitu ambacho wewe mwenyewe hujui. Unapaswa kwanza kufahamu kitu unachotaka kwanza, ndio ukipate.

Kinachowafanya watu wengi waishi maisha ya kawaida Ni kwa sababu tu wanaishi maisha hovyo have hovyo tu bila ya kuwa mpangilio.

Kama kuna njia ya wewe kupoteza maisha yako bila kupata chochote cha maana, Ni wewe kuishi bila hata kujua kitu gani unataka.

Unawezaje Sasa kupata chochote unachotaka?
Kwa hiyo kwanza kabisa jua kitu chenyewe unachotaka. Na hiki linawezekana kupitia kuweka malengo. Kuweka malengo ni hatua ya kwanza ya kubadili yasiyoonekana kuwa yanayoonekana.

Anza leo kwa kuweka malengo? Unajiuliza namna gani unaweza kuweka malengo?

Pili ni kutoa thamani kwa watu.
Watu wanatafuta na kupata fedha kwa taabu . Na hawapo tayari kuitumia hiyo fedha yao kwa mambo ambayo siyo ya muhimu sana. Au yale ambayo wanaona wazi kuwa hayawezi kuwa na thamani kwao.

Kwa hiyo unapaswa kuwa tayari kutengeneza vitu ambavyo vina thamani na ambavyo watu wakinunua kwa hela yao, hasi waone wazi kuwa kweli fedha yao haikwenda bure.

Tatu, tatua matatizo yao.

Hakuna mtu AMBAYE anapenda kukaa na kusumbuliwa na matatizo. Hiki ni kitu kingine ambacho unapaswa kukifahamu. Ukiweza kutatua matatizo ya watu, watu watakuwa tayari kukulipa. Ni hivyo utakuwa na uwezo wa kupata chochote unachotaka.

Je, una maswali au maoni?
Tuandikie: godiusrweyongeza1@gmail.com
Au WhatsApp: 0755848391

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz


One response to “Jinsi ya kupata chochote unachotaka”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X