Cha kufanya pale wenzako wanapokuzidi elimu, kipaji, ujuzi konekisheni n.k.


Kama unajua Kuna wenzako wanakuzidi, elimu, kipaji, ujuzi, konekisheni n.k. unapaswa kupiga kazi kwa bidii.

Yaani, wewe huna maarifa, ujuzi, kipaji halafu unabweteka. Inakuwa siyo poa hata kidogo.

Moja ya kitabu ambacho nimewahi Kusoma kikanifungua sana ni kitabu cha 50CENT na cha Kobe Bryant.

50CENT anasema hivi, unaweza kumzidi akili, unaweza kumzidi konekisheni, unaweza kumzidi kipaji na vitu vingine vyote, ila huwezi kumzidi kuchapa kazi kwa bidii.

Jamaa anasema anachapa kazi kwa bidii. Na kuchapa kazi kwa bidii kumemfanya kuwa alivyo. Ameeleza haya kwenye kitabu chake cha HUSTLE HARDER, HUSTLE SMARTER

Kobe Bryant mwenyewe kwenye kitabu chake cha THE MAMBA MENTALITY anasema alikuwa anaamka asubuhi na mapema kwa ajili ya kufanya mazoezi. Hapa alikuwa anaamka asubuhi na mapema kabla ya mchezaji mwingine yeyote.
Na alikuwa anafanya mazoezi usiku wakati wenzake wote wanaenda kulala.

Hii nayo naweza kuihusisha na Ile ya 50CENT ya kuchapa kazi kwa bidii.

Niliwahi kusikia eti  Mohammed Ali alikuwa hana utaratibu wa kuhesabu pushap anazopiga mpaka pale anapojisikia kuanza kuchoka.

Kama kweli unajijua kuna wenzako wamekuzidi kipaji, akili, konekisheni, uwezo, n.k chapa kazi kwa bidii. Mambo nengine yatajipanga

Naomba kuishia hapo.

Uchambuzi wa kitabu cha 50 CENT huu hapa

Tazama video hii

Ukitaka pia kujua uchambuzi wa kitabu cha Kobe Bryant basi utabonyeza hapa.

Tazama video hii ya Kobe Brayant

Asante.

Kila la kheri
Umekuwa nami .
Rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
0755848391
Morogoro-Tz

,

3 responses to “Cha kufanya pale wenzako wanapokuzidi elimu, kipaji, ujuzi konekisheni n.k.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X