Month: March 2022

  • Jinsi Ya kupakua vitabu bure mtandaoni

    Mara kwa Mara nwatu wamekuwa wakiniuliza mi kwa jinsi gani wanaweza kupakua vitabu mtandaoni. Wengine huwa wananiomba niwattumie vitabu fulanifulani. Binafsi huwa sipendi kumtumia mtu kitabu wakati najua anaweza kukipata mwenyewe. Ni mpaka pale ninapokuwa Nina uhakika kuwa huyu mtu hawezi kukipata kitabu fulani ndio namtumia. Kwa leo sasa ningependa wewe ujue namna unavyoweza kupakua…

  • Kitu kimoja kinachounganisha washindi wote

    Kama una ndoto za kuwa mshindi na kufanya makubwa unapaswa kufahamu kitu hiki kimoja ambacho kinaunganisha washindi wote na watu wote ambao wanafanya makubwa. Kitu hiki ni kuwa na ndoto kubwa. Na siyo ndoto kubwa tu, bali ndoto kubwa ambazo wapo tayari kuzifanyia kazi mpaka zikatimia. Bila ya kuwa na ndoto kubwa utakosa msukumo wa…

  • AMRI KUMI ZA MAISHA

    Huwa likitajwa neno Amri mara nyingi huwa linahusishwa na Amri za Mungu ambazo ndizo amri maarufu. Leo nataka nikwambie pia amri za maisha. Hizi amri hizi hakuna mtu yeyote ambaye anakubembeleza kuzifuata au kuzivunja. Ni au unazifuata kwa faida yako au unazivunja kwa hasara yako. Kama umewahi kusikia usemi kwamba malipo ni hapahapa duniani. Ukizifuata …

  • Kitu muhimu unachopaswa kufahamu kabla ya kuajiri

    Ukiingia kwenye ujasiriamali ni wazi kuwa itafikia hatua ambapo utahitaji kuajiri. Iwe Ni msaidizi wa kaziMtu wa masokoMtu wa mauzoAu yeyote yule.. Kwa vyovyote vile utapaswa kuajiri… Sasa kabla ya kuajiri jiulize je, kuna mashine au kitu ambacho kinaweza kufanya hii kazi? Kama hiki kitu kitumie kwanza badala ya kuajiri. Kama hakuna mashine wala kifaa…

  • Hata kama itatokea ukasahau vyote maishani, Ila hakikisha hausahau kufanya hivi vitu

    1. Usisahau kuweka AKIBA. Kwa kila kipato chako unacjopata weka akiba ya asilimia 10. 2. Usitumie fedha zaidi ya unavyoingiza. 3. Usifanye vitu kuwaridhisha watu. 4. Usitegemee chanzo kimoja cha kipato na hasa mshahara. 5.  Mara zote kuwa na kitabu na soma vitabu. 6. Hakikisha unakuwa na malengo na unayafanyia kazi. 7. Ukitaka kuibadili dunia.…

  • Jinsi ya kuandika KITABU kikubwa kwa namna ya kawaida

    Mwaka juzi nilitoa Kitabu CHANGU cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. Kwenye Kitabu HIKI nimeeleza hatua kwa hatua jinsi ambavyo unaweza kufikia malengo na ndoto kubwa kwenye maisha. Mmoja wa wasomaji wa Kitabu hicho alinipigia simu baada ya kuwa anlmekisona na kuniambia kuwa ana ndoto ya kuandika tamthiliya. Niliongeaa Naye na kumtakia kila la kheri.…

  • Kitu kikubwa na muhimu kwenye ujasiriamali siyo kujua kutengeneza bidhaa

    Kitu kikubwa na muhimu kwenye ujasiriamali siyo kujua kutengeneza bidhaa. Siyo kabisa! Ingekuwa hicho ndio kitu kikubwa basi wengi wangekuwa wametoboa. Hiyo ni sehemu ndogo tu… Juzi tu hapa nilikuwa naongea ndugu mmoja ambaye anakaribia kuhitimu chuo. Kama ilivyo kawaida yangu nilimwuliza una mpango gani na maisha baada ya chuo…! Hili ni swali ambalo nimewauliza…

  • Kitu gani unaenda kufanya wiki hii ili kujisogeza karibu na malengo yako?

    Kwenye kitabu changu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI, nimeeleza kwamba kadiri unavyokuwa unafanyia malengo yako, yenyewe yanakuwa yanasogea karibu pia. Hivyo, Kuna sehemu mtakutana ambayo ndiyo pointi ya wewe kufikia melengo yako. Sasa wiki mpya tayari imeanza, ni kitu gani unaenda kufanya wiki hii ili usogee karibu na malengo yako? Hakikisha unafanya kitu. Bila kufanya…

  • Namna ya kufanya usomaji wa vitabu uwe sehemu ya pili ya maisha yako

    Kusoma ni tabia. Na tabia yoyote hujengwa.  Kuna tabia ambazo unazo sasa hivi unazifanya ila hujiulizi mara mbili kama uzifanye au uache. Kwa mfano kila siku unapiga mswaki ila hujiulizi mara mbili kwamba upige au usipige leo utapiga mswaki kesho. Yaani, kupiga mswaki kumeshakuwa tabia yako ya pili. Sasa hata kusoma kunapaswa kuwa tabia yako…

  • Zama Zimebadilika (Part 1)

    UTANGULIZI Dunia tunamoishi sasa imepitia katika nyakati mbali mbali kwa vipindi mbali mbali. Dunia hii imekumbana na vitu mbali mbali ambavyo vimekuwa vikiiweka hii katika vipindi kadha wa kadha ambavyo tunaviita zama. Zama ni nini? Kamusi ya Kiswahili sanifu inazizungumzia zama kama nyakati. Kwa hiyo tungeweza kusema kwamba nyakati sasa zimebadilika badala ya kusema kwamba…

  • KUTOKA KWENYE AJIRA MPAKA KUJIAJIRI

    Nakumbuka juzi nilikushirikisha safari ambayo unapaswa kuifuata ili uweze kujiajiri kama umeajiriwa kwa sasa. leo hii naomba kuendelea tena kwa kukushirikisha vitu zaidi kwenye suala zima la ujasiriamali na kujiajiri.  Na leo ninakushirikisha machache niliyopata kutoka kwenye kitabu cha Employee To Entrepreneur Moja ya ushauri ambao umekuwa unatolewa kwa watu wengi ni ushauri wa kwamba…

  • Ushauri Mzuri Ambao Nimewahi Kupokea Maishani Mwangu

    Nakumbuka mwaka 2016 hivi wakati naendelea na masomo yangu ya chuo. Nilikuwa njia panda nikifikiria niache chuo niendelee na biashara na uandishi au nifanyeje? Uamuzi wangu ulikuwa kuacha chuo… Baadaye katika kuwashirikisha watu wangu wa karibu; mmoja wao aliniambia hivi; Godius fanya vyote, endelea na kusoma, andika na fanya biashara. Ukifanikisha vyote vitatu utaonekana shujaa…

  • Nguvu Ya Kuwa Na Ratiba Na Mambo Matano Ya Kujifunza Kutoka Kwa Benjamin FranklinKila Mara nimekuwa

    Kila mara nimekuwa nikisisitiza juu ya umuhimu wa kuwa na ratiba. Ukiamka asubuhi pangilia siku yako kwa namna ambavyo ungependa iwe. Andika vitu ambavyo utafanya na hata vile ambavyo hutafanya. Lakini pia kuna vitu ambavyo vinajirudia kila siku katika ratiba yako. Na hapo ndipo unapaswa kuwa na mfumo fulani ambao unaufuata. Mfumo huu utakuwezesha wewe…

  • TAARIFA: Masomo Na Uchambuzi Kuhusu Soko La Hisa Kwa Siku 30 Zijazo

    Leo rafiki yangu nina habari njema Sana. Unajua ni habari gani? Ewaaa! Ni kuhusu uwekezaji kwenye soko la hisa. Kwa siku 30 zijazo kuanzia tarehe tarehe 1 aprili nitafanya kimoja kati ya vifuatavyo.1. nitatoa uchambuzi Kuhusu mwenendo wa soko la hisa2. Nitatoa mafunzo kuhusu soko la hisa3. Nitajibu maswali yanayoulizwa kuhusu uwekezaji na soko la…

  • Kwa nini hufikii ndoto zako

    Umekuwa na ndoto kubwa Ila bado hazifanikiwi? Unajua kwa nini? Najua kwa asili sisi ni viumbe wenye ndoto kubwa. Ndio na hili naweza kuliona kwa watoto wadogo. Maana mtoto mdogo haogopi kusema waziwazi kuwa siku moja atakuwa daktari au kuwa siku moja atakuwa rubani. Mtoto akiona ndege anasema ni ya kwangu au ya baba yangu…

  • Kinachowatofautisha Wanaofikia Ndoto Zao Na Ambao Hawazifikii

    Kitu kimoja kikubwa ambacho kinawatofautisha wanaofikia ndoto zao na ambao hawazifikii ni vitendo. Wanaofikia ndoto kubwa ni watu wa vitendo. Siyo watu wa kukaa mtandaoni na kuanza kuzungumzia ndoto zao. Bali vitendo vyao ndivyo vinaongea. Wewe pia kama unataka kufikia ndoto zako. Tenda zaidi ya unavyoongea. Hivyo tu. Anza leo.

  • Ulipata kitabu cha bure?

    Rafiki yangu kwa siku Sasa nimekuwa natoa kitabu cha bure. Itasikitisha sana endapo hutachangamkia hii ofa na kuchukua hiki kitabu. Yaani, wewe ushindwe kupata kitabu cha kununua. Ushindwe hata kupata cha bure. Kweli? Ebu chukua hatua Sasa hivi…. Kipate hapa

  • Njia nzuri na ya pekee ya kupata matokeo yadumuyo

    Kama kuna mtu ambaye amekufikisha wewe juu, mtu huyohuyo anaweza kukuangusha chini. Kama umetumia njia ya mkato, njia hiyohiyo inaweza kukurudisha chini Njia nzuri na ya pekee ya kupata matokeo yadumuyo ni kufuata mchakato.Mchakato unakujenga.Hata ukianguka unaweza kusimama tena maana unakuwa unaujua mchakato. Rafiki yangu, kazana kuujua mchakato, kisha ufuate.

  • Mwongozo Sahihi Wa Kufikia Malengo Na Ndoto Zako

    Ebu kwa mfano fikiria hili Umezaliwa na kukua katika mazingira ambayo wewe mwenyewe kabisa unaona huyapendi. Baadaye unasikia kuwa ukitaka kufanikiwa unapaswa kuweka malengo. Unaweka malengo lakini bado huoni matokeo makubwa, badala yake ni kama umeamua kujifukia kwenye shimo. Habari za kuwa unapaswa kuwa mvumilivu zinakufikia. Unasema ngoja niwe mvumilivu kwanza.Lakini bado hola! Unafanyaje sasa?…

  • Wateja wako wasikusahau

    Hakikisha kila mara unawasiliana na wateja wako. Usipowasiliana na wateja wako mara kwa mara watakusahau na hata kushindwa kuja kununua kwako. Kitu hiki kinaweza kupekelekea wateja wako kwenda kununua kwa washindani wako. Weka utaratibu wa kuwasiliana na wateja wako kila mara. Tafuta sababu (excuse) nzuri ya kuwasiliana na wateja wako.Mfano siku ya kuzaliwa kwao wapigie…

X