Kinachokukwamisha Wewe Kuandika Kitabu Chako Ni Hiki..


Kama Kuna kitu watu wamekuwa wanasema kwamba halijakaa sawa ni mfumo wa elimu. Umekuwa unalalamikiwa kwa
Kukaririsha watu vitu
Kutokujjenga watu wenye ujuzi
Kutokuwaandaa wahitimu kwa ajili ya maisha baada ya chuo n.k.

Kwenye hili naweza kusema kuwa Kuna kitu kimoja watu huwa wanakisahau. Kitu hiki ni namna mfumo wa elimu unavyozuia watu kutumia uwezo wao mkubwa wa kuandika.

Unaweza kukuta mtu alikuwa na ndoto kubwa kwenye maisha ya kuandika vitabu ila baada ya chuo hatamani kuandika tena

Kwa Nini?
Moja ya kitu ambacho mwanachuo anapaswa kufanya anapokuwa chuoni ni utafiti. Na utafiti huu huwa unapaswa kuwasilishwa kwa njia ya maandishi.

Sasa elimu yetu unakuta kwamba kabla ya kukamilisha andiko lako lako la utafiti, unabinywa kwelikweli. Unazungushwa huku na kule na mpaka mtu anamaliza kuandaa andiko lake, anakuwa amehenyeka sana.

Kitu hicho kinawafanya wengi wakose hamu ya kuandika baada ya chuo. Nadhani na wewe utakuwa mmoja wao.

Ila kikwazo kama hiki kinaondoleka.
Ili kukusaidia kuondoa kikwazo hicho nimeandaa darasa rasmi la uandishi ambapo Mimi ninaenda kukusimamia na mwanzo mpaka mwisho kuwa mwandishi MBOBEVU.

Darasa hili litakalofanyika kwa njia ya mtandao, linaenda kuwa la kipekee sana. Utavunja hiyo hali inayokuzuia wewe kuandika kuandika. Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yako utaaandika na kukamilisha kitabu chako.

Kama umependa hicho kitu ebu rusha mikono juu kidogo kushangilia ushindi huo….

Shangilia ushindi huo maana ni uhakika kuwa ukijiunga na kozi hii, ushindi huo unaupata tu.

Sambamba na hilo kwenye kozi hii:

👉Nitakusimamia na kusoma kazi zako unazoandika kila siku na kukuelekeza namna bora ya kuziboresha

👉Nitakufungulia blogu ya bure.
👉Utajifunza mengi kutokana na yale wanayoandika wenzako na maoni nitakayokuwa natoa kuhusu kazi za wenzako.
👉Utapata kitabu Cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 bure.
👉Utapata jarida lenye hatua 15 za kufuata ili kuandika magazetini.
👉Utapata mafunzo ya audio zaidi ya 10. Yakiwemo mahojiano na waandishi wakubwa hapa nchini.

👉Utaungana na waandishi wengine wanaoandika na kujifunza mengi kutoka kwao.

Nafasi kwenye darasa hili ni 10 tu. Hivyo, kama unataka kuhudhuria darasa hili, sharti uwahi kujihakikishia nafasi yako kabla hazijaisha. Na gharama ya kozi hii ni laki mbili (200,000)

jihakikishie nafasi yako sasa hivi kwa kuwasiliana nami kwa 0755848391



One response to “Kinachokukwamisha Wewe Kuandika Kitabu Chako Ni Hiki..”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X