Karibu Kwenye Darasa Rasmi La Uandishi Mwaka 2022


Tangu mwaka 2019 nimekuwa naendesha darasa la uandishi ambapo huwa ninakaa na watu watano na kuwafundisha uandishi kwa kina. Darasa hili la kipekee ambalo huwa naliendesha kwa watu wachache tu, huwa linafanyika kwa njia ya mtandao, huku nikiwa na lengo la kuwafundisha na kuwanoa hao watu wachache na kuwafanya waandishi wabobevu.

Kila mwaka darasa hili limekuwa linafanyika kwa mafanikio makubwa, huku wahusika wake wakiwa wanatoka wamenolewa na kupata ujuzi kamili wa kiuandishi. Ndio maana mwaka huu kwa mara nyingine nimeamua kuliandaa darasa hili. Hivyo, kitu cha kwanza kabisa, ningependa kutangaza kuwa darasa hili litaanza rasmi tarehe 16.3.2022 na usajili kwenye darasa hili hapa umefunguliwa tayari.

Darasa hili la uandishi linafundisha nini haswa?

Kwenye darasa hili la kipekee sana unaenda kujifunza kwa kina kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi wa vitabu na makala. Kiufupi ahadi yangu kubwa ni kuwa hata kama hujawahi kuandika kitu chochote, kwenye darasa hili hapa unaenda kuandika na mwisho wa siku unaenda kuibuka kama mbobezi.

Nasema hivyo, kwa sababu kwa siku zote za darasa utapata nafasi ya kipekee sana ya kuwa karibu na mimi. Nitakupa masomo, nitakufuatilia kuona mwenendo wako, utauliza maswali kuhusu uandishi nami nitakujibu, utaandika makala nami, makala hizo nitazipitia na mwisho wa siku nitakupa mrejesho kuhusiana na makala hizo ulizoandika na kila siku nitahakikisha kwamba unapata somo moja la ukweli litakalokueleza kuhusu masuala ya uandishi. Hivyo, ndivyo tunaenda kutumia siku zetu.

Kama una ndoto ya kuandika kitabu, hili darasa linakuhusu sana. Utapata mbinu za kukusaidia kuandika kitabu chako kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Tunaenda kutumia mbinu 10:4:2 kwa wale wote watakaokuwa wanaandika vitabu.

Na kama hujui pa kuanzia kwenye kuandika kitabu chako au kwenye uandishi basi darasa hili linakufaa sana. Kama umeanza kuandika ila ukaishia njiani na umekwama hujui unawezaje kuendelea basi jiandikishe kwenye darasa hili.

Pia kwenye darasa hili utajifunza namna ambavyo unaweza kuanza kuandika. Hiki ni kitu ambacho kimekuwa kinawazuia watu wengi. kati ya watu wengi ambao nimefanya nao kazi, basi huwa naona sehemu ya kwanza kabisa ambapo wanakwama ni kuanza.

Mtu anajiuliza hivi naanza, anzaje. Naandika nini na nani atasoma kazi zangu. wengi wanakuwa na hofu ya kuanza kuandika. Mimi ninachopenda kukwambia ni kwamba ingia kwenye hili darasa, kwa mara ya kwanza kwenye maisha yako, utaweza kuanza kuandika na hata utaweza kumaliza darasa hili ukiwa tayari na kitabu chako.

Ndio namaanisha kuwa mwisho wa darasa hili hapa, utaweza kukamililsha kitabu chako.

Utajifunza namna bora ya kupata wazo la kuandika. Kama kuna swali ambalo watu huwa wanauliza, ni mbinu gani ambazo watu huwa wanatumia kupata wazo la kuandika.

Kuna watu huwa wanajiona kama vile hawawezi kuwa na wazo la kuandika, hivyo kwenye darasa hili utajifunza njia mbalimbali za kukupa mawazo ya kuandika, kiasi kwamba hutakaukiwa kwenye uandishi wako.

Utajifunza njia bora za kuhariri kitabu chako. Kwenye darasa hili hapa unaenda kujifunza namna za kuhariri kazi zako za uandishi

Utafundishwa hatua utakazopaswa kufuata kuanzia unapoandika mpaka unapochapa kitabu chako. Kumekuwepo na nadharia nyingi kuhusiana na masuala ya uchapaji wa vitabu. kwenye darasa hili hapa unaenda kupata mwongozo sahihi wa kufuata mpaka pale unapokuwa na kitabu chako mkononi.

Sambamba na hayo yote utajifunza mambo mengine mengi sana.

Kwani uandishi unafundishwa ?

Kuna hoja ambayo nimekuwa nakutana nayo ambayo ni je, uandishi kama uandishi unafundishwa? Tena wengine wamekuwa wanasema kwamba uandishi ni kipaji ambacho mtu anazaliwa nacho, hivyo haupaswi kufundishwa?

Ninachotaka kukwambia ni kuwa ni kweli uandishi unafundishwa. Hakuna mtu hata mmoja anazaliwa akiwa amebobea kwenye suala zima la uandishi, hivyo, ni mpaka pale utakaponolewa na kufunzwa vizuri ndipo utaweza kubobea na kuimarisha zaidi misuli yako ya uandishi na kuwa bora zaidi.

Uandishi ni kama kipaji cha kucheza mpira wa miguu au kikapu. Kwenye mpira miguu kuna wachezaji ambao wana vipaji ila bado wananonelewa chini ya watu waiobobea ili waweze kubobea na kuwa imara zaidi.

Na uandishi upo hivyo, bila kujali una kipaji au la, utapaswa kuingia darasani na kuanza kujifunza kwa kina kuhusu uandishi na leo hii nimetangaza rasmi nafasi za kujifunza uandishi kwa mwaka 2022. Hakikisha hukosi nafasi hii

Darasa hili litadumu kwa muda gani ?

Darasa hili la kipekee sana linaenda kudumu kwa kipindi cha siku 30 tu. Ndani ya kipindi hiki hapa unaenda kujifunza kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi kutoka kwa mwandishi mbobezi. Sambamba na vitu vyote ambavyo nimesema hapo mwanzo utakavyojifunza.

👉Utapata kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30 bure.

👉Utapata ripoti maalumu yenye HATUA 15 ZA KUFUATA ILI KUANDIKA MAGAZETINI

👉Utapata audio zenye mafunzo kuhusu uandishi zaidi 10

👉Utapata nafasi ya kunipigia simu na kuniuliza swali lolote kuhusu uandishi, muda wowote ule utakapokuwa na swali katika kipindi chote cha uandishi.

👉Nitapitia kazi zako na kukupa mrejesho wa kitalaamu na

👉Utaungana na watu wengine kama wewe na utapata kujifunza kutokana na makosa yao au yale wanayofanya vizuri. Kama kuna ktu ambacho wanafunzi wangu huwa wananufaika nacho kwa sana ni hiki hapa. kwenye darasa hili hapa wanafunzi wangu huwa wanaufaika sana na maoni ambayo huwa natoa kwenye kazi zao na za watu wengine. Kila siku huwa napitia kazi ya mtu mmoja baada ya mwingine na kumpa mrejesho wa kuhusiana na kazi yake. Kitu hiki huwa kinawafanya wanafunzi wangu wajifunze kwa kina na kuelewa vizuri dhana nzima ya uandishi kiundani.

👉 Utafunguliwa blogu ya bure kabisa.

Wanahitajika watu wangapi ili kukamilisha darasa hili?

Kwa kawaida darasa hili huwa naliendesha nikiwa na watu watano. Ila zamu hii wanahitajika watu kumi tu. Ndio ni watu kumi na siyo zaidi ya hapo. Ninafanya hivyo ili niweze kupata muda wa kunitosha kupitia kazi za waandishi watakaojiunga na darasa husika na kuwafuatilia kwa umakini, na watu watano ndio idadi ambayo naweza kuifuatilia kwa ukaribu. Hivyo, naweza kusema kwamba hili darasa ni la PRIVATE. Na kila anayejiunga na darasa hili ni V.V.I.P.

Nafanyaje ili kujiunga ?

Ili kujiunga na darasa hili hapa utapaswa kulipia laki mbili (200,000/-) kama gharama ya darasa hili la kipekee. Thamani ya darasa hili ni kubwa sana kwa kiwango ambacho haiwezi kununulika kwa gharama za kawaida, ila sasa unaenda kuipata kwa laki mbili tu.

Kikawaida watu wengine huwa wanalipia laki saba na nusu (750,000), kuingia kwenye darasa hili hapa ila zamu hii unaenda kujiunga na darasa hili kwa bei ndogo ya laki mbili tu.

Kama utapenda kujiunga na darasa hili, wasiliana nami kwa 0755848391. Usianze kutuma fedha, wasiliana nami kwanza ili nikuhakikishie kuwa nafasi bado zipo ndipo utume fedha.

Nakukumbusha tu kuwa kwenye darasa hili unaenda;

👉kujifunza kwa kina kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uandishi wa vitabu na makala

👉Namna ambavyo unaweza kuanza kuandika, kuhariri, kuchapa mpaka kutoa kazi zako. na hapa unaenda kujifunza haya kutoka kwa mwandishi mbobevu.

👉 Mbinu bora za kupata wazo la kuandika, kuhariri na hata kuchapa kitabu chako.

👉 Kikubwa kwenye darasa hili ni kuwa utapata konekisheni zote unazohitaji. Utaunganishwa na wachapaji wazuri, utaunganishwa na wauzaji na wasambazaji wa vitabu na hata utapewa maelezo sahihi ya kupata dhana muhimu za kitabu chako kama ISBN na bar code.

👉Na kikubwa zaidi ni kuwa utapewa kipaumbele kwenye semina ya LIVE (ana kwa ana) itakayofanyika mwishoni mwa mwezi wa nne (tarehe 30), hapa Morogoro.

Kiufupi mambo ni mengi kwenye darasa hili hapa.

Kama kuna uamuzi bora ambao unaweza kufanya kwa ajili yako au kwa ajili ya ndugu yako basi ni kulipia au kumlipia gharama za darasa hili hapa.

Jiwekee nafasi yako sasa kwa kuwasiliana nami kwa 0755848391 kisha utalipia gharama za darasa ambazo ni laki mbili (200,000). Tuwasiliane sasa kwa 0755848391

PATA KITABU CHA BURE

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli

Godius Rweyongeza

+255755848391/ Morogoro-Tanzania


3 responses to “Karibu Kwenye Darasa Rasmi La Uandishi Mwaka 2022”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X