Kama kweli umejitoa na unataka kujifunza kwa kina kuhusu uandishi, BASI SOMA HAPA


Mwaka 2016 nilipoanza kuandika ulikuwa ni mwaka ambao niliamua na kujitoa kuwa ninaenda kujifunza kwa kina kabisa kuhusu uandishi. Tokea mwaka huo nimejifunza na kusoma vitabu vingi kuhusu uandishi. Nimesoma makala za kutosha kuhusu uandishi. Siyo hilo tu, nimefanyia kazi vitu vingi nilivyosoma na kuviweka katika matendo kwa kuandika vitabu 17 makala zaidi ya elfu mbili. nimeandika kwenye magazeti makubwa hapa nchini na mambo mengine mengi.

Nimeitumia kila nafasi niliyoipata kuhudhuria semina na kozi zote fupi na ndefu ili kujifunza mambo kadha wa kadha kuhusu uandishi.

Katika kufanya haya yote nimekusanya maarifa ambayo huwezi kuyapata sehemu nyingine yoyote kwa pamoja, ni maarifa ya kipekee ambayo siyo tu kwamba nimeyakusanya na kuyaweka sehemu, bali mimi mwenyewe nimeyafanyia kazi katika mchakato mzima wa kuandika na kuchapa vitabu vyangu.

Kila nilipochapa kitabu kimoja, nikawa najifunza na kusoma zaidi ili kujua namna ya kuboresha kitabu kitakachofuata. Kila niliochapa toleo la kwanza nikawa nazama tena ndani ili kujifunza namna nitakavyoboresha toleo la pili.

Kwa jinsi hiyo basi nimeweza kujifunza mambo mengi kwa kipindi hicho kuliko kawaida.

Na sasa nipo tayari kukushirikisha wewe maarifa haya kuhusu uandishi wa vitabu kwenye DARASA maalumu litakalofanyika mtandaoni kuanzia tarehe 16. Machi mwaka huu.

SOMA ZAIDI: Karibu Kwenye Darasa Rasmi La Uandishi Mwaka 2022

SOMA PIA: KWA NINI UNAPASWA KUHUDHURIA DARASA RASMI LA UANDISHI MWAKA 2022

Gharama ya kuhudhuria darasa hili hapa ni laki mbili (200,000) na hapa ninataka niseme kitu, maana kuna watu ambao wanafikiri kwamba nimeweka gharama kubwa sana, pengine na wewe unafikiri hivyo.

Binafsi nimekuwa nikiwekeza kwenye kujifunza uandishi kwa nguvu zote kama vile maisha yangu yote yanategemea uandishi. Sisemi hivyo ili ujue kwamba nimewekeza hela nyingi. Potelea mbali…

Kitu kikubwa ninachotaka ujue ni kwamba kuna madini ya pekee unayoenda kupata kwenye hii kozi kuliko ambavyo unaweza kupata kwenye kozi nyingine au kitabu kingine. Darasa hili ninalokwambia lina mkusanyiko na muunganiko wa maarifa ambayo nimeyakusanya kwa kipindi cha miaka mitano sasa.

Kwa hiyo unaenda kupata uzoefu wa miaka yote mitano ukiwa tayari umechakatwa na kuwekwa pamoja ndani ya siku 30 tu. Hiki ni kitu cha kipekee sana.

Naomba unisikilize mimi kwa kitu hiki, kama utaamua kuanzia leo hii kuanza kukusanya na kujifunza kitu kimoja baada ya kingine peke yako, maana yake itakuchukua wewe miaka mitano kujua haya yote ambayo ninaenda kukufundisha ndani ya siku 30 zijazo. Na hapa ni kama tu utaupa uandishi kipaumbele kama ambavyo huwa naupa kipaumbele.

Kuna watu huwa wanasema kwamba makala zako zinavutia na unajua kuzipangilia… nawakaribisha tukutane kwenye darasa hili hapa maana unaenda kujifunza siri zote za uandishi kwenye hili darasa

Kama sasa umeamua kwamba hili darasa sitaki linipite, njoo tufanye kazi uone jinsi utakavyojifunza mambo mengi na ya kipekee sana…

Ubora ni kwamba hauna kitu cha kupoteza. Ukilipia laki mbili (200,000) halafu katikati ya kujifunza au baada ya darasa kuisha ukaona fedha uliyotoa na kile ulichojifunza haviendani, utakuwa huru kuomba kurudishiwa fedha yako NA UTARUDISHIWA. Nasisitiza tena kwamba fedha yako yote utarudishiwa, tena bila kuulizwa maswali yoyote.

Kama kweli umejitoa na unataka kujifunza kwa kina kuhusu uandishi, basi tuwasiliane sasa kwa 0755848391.

Au bonyeza tu HAPA kuwasiliana nami kwa haraka zaidi.

Unaweza kuanza kulipia kidogokidogo kuanzia sasa hivi ila mwisho wa kulipia ni tarehe 10.3.2020.

Kama unahisi kabisa huwezi kulipia gharama za darasa hili au zimekuwa kubwa kupitiliza, basi utaniambia nitajua kitu gani cha kukusaidia.

Karibu

BONYEZA HAPA kuwasiliana na mimi kwa haraka. BONYEZA HAPA

SOMA ZAIDI: Karibu Kwenye Semina Rasmi Ya Uandishi Mwaka 2022

PATA KITABU CHA BURE

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli

Godius Rweyongeza

+255755848391/ Morogoro-Tanzania


One response to “Kama kweli umejitoa na unataka kujifunza kwa kina kuhusu uandishi, BASI SOMA HAPA”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X