Waandishi Wa Vitabu: Igeni Kitu Hiki Kimoja Tu Kutoka Kwa Wasanii Muziki


 

Huwa napenda kusikiliza muziki wa bongo flava mara mojamoja ninapokuwa nimepumzika. Kama na wewe huwa unausikiliza walau hata mara moja moja nyoosha mkono juu tujuane.

Ukifuatilia muziki huu hata kwa dakika tano tu, Kuna kitu kimoja ambacho utakigundua kwa wasanii na hiki ndicho ninataka tujadiliane leo. Kitu hiki siyo kingine bali ni kushirikisha kwa baadhi ya wasanii kwenye tungo zao mbalimbali.

Utakuta msanii fulani ameshirikiana na msanii mwingine kutoa tungo fulani. Ni kitu ambacho ukikiangalia kwa juu juu unaweza kuona ni cha kawaida au hakina maana, ila ukikiangalia kwa jicho la kipekee utagundua kuna kitu Kikubwa cha kujifunza hasa kwa WAANDISHI.

Labda tujiulize kwa Nini wasanii wa muziki huwa wanashirikiana? Sababu kubwa ni kupeana konekisheni na mashabiki.

Unakuta msanii A ama wafuasi na mashabiki wake huku msanii B akiwa na wafuasi na mashabiki wake pia. Sasa wanapoungana kutengeneza wimbo mmoja kuna wafuasi na mashabiki wa msanii A wataanza pia kumfuata na kumsabikia msanii B na hivyohivyo kwa upande wa pili.

Hakuna msanii anaogopa kushirikisha na mwenzake kwa kuogopa kuwa mwenzake ataondoka na wafuasi wake wote, badala yake wanashirikiana kadiri wawezavyo.

SASA WAANDISHI TUNAWEZA KUITUMIAJE HII?

Looo! Nimekumbuka kwamba naongea na waandishi na siyo wasanii wa muziki, ngoja sasa niache kuongelea masuala ya wasanii bwana niongelee mambo ya kiuandishi?

Kwa Waandishi mnaweza kutumia hii njia kwa kushirikisha katika kuandika makala.
Kuandika kitabu
Kuatangaziana bidhaa au vitu vyenu.
Kupost vitu vya mwenzako na mwenzako kupost vya kwako (hapa tafuta mwandishi ambaye mpo kwenye level moja au mnazidiana kidogo)
Kukomenti kwenye maandiko ya mwandishi mwenzako kwa kuongezea pointi za maana zaidi. Hii pia inaweza kukuongezea idadi ya watu wanaofuatilia kazi zako.
Kushiriki kikamilifu kwenye kundi la mwenzako na kutoa mafunzo.
Kuweka Dibaji kwenye kitabu chako; Dibaji iwe imeandika na mtu ambaye ana jina kubwa kuliko wewe.
Kuwaomba  Waandishi wengine wakuandikie neno fupi kuhusu kitabu chako (review).

Na mengine mengi.

Kwa hayo naamimi walau umelata kitu ambacho kinaweza kukusaidia Kama mwandishi.

Kama wewe MWANDISHI ambaye uko siriazi na kuandika na unataka kwenda viwango vingine, Basi hakikisha umesoma kitabu cha JINSI YA KUWA MWANDISHI MBOBEVU NDANI YA SIKU 30.
Nakala laini (soft copy) inapatikana kwa 6500/- tu. Nakala ngumu kwa Sasa haipo. Tuwasiliane sasa kwa 0755848391 ili upate nakala yako


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X