MAiSHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE. Zipuuze Zikukikimbie



Hakuna fursa ambayo huwa inapotea. Usipotumia vizuri fursa inayokuja kwako, kuna mtu ambaye ataitumia. Asiyejulikana.

Huwezi kuongelea ulimwengu wa kompyuta na mapinduzi ya kompyuta kiujumla bila kumwongelea Gary Kildall. Huyu jamaa ndiye alipaswa kuwa Bill Gates wa nyakati zetu ila akachezea fursa..endelea kusoma ili ujue kilichotokea.

Mwaka 1977 kampuni ya apple ilitengeneza kompyuta yao ya kwanza iliyojulikan kama APPLE 1. Hapo ndipo vuguvugu la PERSONAL COMPUTERS lilipoanzia. Zilikuwa bado hazijawa za mpakato kama ilivyo sasa hivi, ila kampuni ya APPLE ilikuwa imeleta mapinduzi makubwa.

Kampuni ya IBM kwa kuona kuwa wanaachwa nyuma, walitengeneza timu ya dharula ya kushughulika na hili na suala. Lengo la hii timu ilikuwa ni kutengeneza PERSONAL COMPUTER haraka iwekezakavyo kabla hawakapoteza fursa ya kuwa sehemu ya mabadiliko.

Hiyo timu ilianza kazi na mwaka 1980 kazi upande wa HARDWARE ukawa umekamilika. Kilichobaki ulikuwa ni mfumo wa kuiendesha kompyuta (OPERATING SYSTEM) ambayo wataalamu wa IBM hawakuwa na uwezo nayo. 

Kutokana na uharaka ilibidi wamtafute Bill Gates awasaidie. Walipoenda kwa Bill Gates aliwapokea na kuwaelekeza kuwa kampuni yake haikuwa na mwelekeo wa kutengeneza mfumo huo (operating system) kwa siku za karibuni. Hivyo, aliwaelekeza kwa rafiki yake ambaye alikuwa tayari ametengeneza mfumo huo ambaye sasa ndiye Gary Kildall.

Gary Kindall alikuwa mmoja wa watu wa kwanza kabisa kuona uwezekano wa kutengeneza kompyuta  binafsi (PERSONAL COMPUTERS), kiasi alishaanzisha kampuni inayotengeneza operating system iliyokuwa inaitwa Digital Research Inc. 

Hivyo kumbe, Bill Gates alipowaelekeza watu wa IBM kwa huyu jamaa siyo kwamba alikuwa anatania, bali ulikuwa ukweli.

 Gary Kindall alipokea simu kutoka kwa Bill Gates ambaye alimwambia kuwa kuna watu wanakuja, hivyo atapaswa kuongea nao vizuri. Ila hakuambiwa ni watu gani? Garry Kindall akawa amechukulia poa hilo suala na hivyo akapanda ndege yake binafsi kwenda kwenye mishemishe nyingine.

Watu wa IBM walipofika hawakumkuta Gary Kindall, hivyo walilazimika kuongea na mke wake. Hata hivyo mazungumzo yao hayakwenda vizuri. Kitu kitu kikubwa kinachosemekana kilifanya mazungumzo yao yasiende sawa, maana mke wa Gary alishindwa kuchukua badhi ya maamuzi kutokana na mme wake kutokuwepo.

Hivyo watu wa IBM waliondoka kwa hasira bila mafanikio yoyote. Ilibidi wamrudie Bill Gates kumwomba msaada. Bill Gates kuona hiyo nafasi imerudi kwake mara ya 2, ikabidi aitumie.

Alichofanya alinunua kampuni ambayo kiuhalisia siyo kwamba ilikuwa imetengeneza operating system ya kwake, bali ilikuwa imeiga kutoka kwa akina Gary Kindall. Hivyo, alichofanya Bill Gates alichukua SOFTWARE hiyo, na kuwapa IBM. Huo ukawa mwanzo wa Bill Gates kuwa Bill Gates na Gary Kindall kupotea kwenye ramani….

Umejifunza nini hapa?

Hakikisha unapata kitabu cha MAISHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE

Lipia elfu 6 tu Leo uweze kupata kitabu. Ndiyo elfu sita (6,000). Changamka sasa

Tuma fedha kwa 

M-PESA 0755848391 au

Airtel money: 0684 408 755

 jina ni GODIUS RWEYONGEZA

Siku njema

Godius Rweyongeza

+255755848391

Morogoro-Tz

www.songambeleblog.blogspot.com


One response to “MAiSHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE. Zipuuze Zikukikimbie”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X