Kitu hiki lazima tu kitokee maishani mwako


 

Kuna vitu katika maisha lazima tu vitokee. Vinatokea uwe unavipenda au huvipendi. Vyenyewe vinatokea tu.


Jua linachomoza na kuzama, bila kujali unapenda au hupendi.
Dunia inajizungusha kwenye mhimili wake, bila kujali una chuki nayo au unaipenda.
Ukiruka juu, sharti utarudi chini bila kujali unapenda au hupendi.

Mojawapo ya kitu kingine ambacho lazima kitokee kwenye maisha ni mabadiliko. Uwe unapenda au hupendi mabadiliko lazima tu yatatokea.

Ndio maana unaona kila zama huwa zina matajiri ambao huwa wanatengeneza mabilioni ya fedha ya kutumia fursa ya mabadiliko fulani vizuri.

Mansa Musa alikuwa tajiri mkubwa kuwahi kutokea duniani kwa sababu alitumia fursa ya kuuza chumvi na dhahabu enzi zake vizuri. Unaweza kushangaa chumvi?!! Ilimtajirishaje mtu?? Ukweli ni kwamba kipindi chake chumvi ilikuwa dili kubwa Kama ambavyo miaka ya 1800 viwanda vilikuwa dili kubwa pia.

Kitu Kikubwa ninachotaka ni wewe kuhakikisha unasoma mabadiliko na kuyatumia kwa manufaa.

Ni hayo tu
NAKUKUMBUSHA TU. Kama hukupata nakala ya kitabu cha MAiSHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE kwa elfu sita tu (6,000/-) changamka utumie fursa hii leo hii. Kuanzia mwezi ujao kitabu kitarudi kwenye bei yake ya elfu kumi.

Hivyo kipate Leo kwa elfu sita tu. Cha kufanya Sasa. Tuma elfu sita (6,000/-) kwa MPESA 0755848391 au Airtel money 0684 408 755
Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

CHANGAMKA SASA.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X