Fursa iliyotengeneza mabilionea kwenye karne ya 21


 

Madalali ni watu ambao wamekuwepo kwa siku nyingi sasa. Kazi yao kubwa imekuwa ni kuunganisha eneo moja lenye bidhaa na jingine lenye uhitaji.

Kama una uhitaji wa chumba cha kupanga unamwona dalali anayekuunganisha kilipo.

Kiufupi wenyewe wamekuwa wanaingia katikati ya mlaji na mzalishaji.

Kwenye karne ya 21 udalali ndio umetengeneza mabilionea kwa wingi. Mtandao wa amazon na alibaba ni ya kidalali inayounganisha  kati ya wazalishaji na walaji wa mwisho wa bidhaa.

Mtandao wa Uber ni wa kidalali pia. Unaunganisha kati ya wenye teksi na wasafiri.

Google pia ni mtandao wa kidalali, unaunganisha mwenye taarifa na mwenye uhitaji nazo.

Ukiangalia mitandao yote hiyo imetengeneza mabilionea wakubwa. Hivyo, kwenye karne hii ya 21 ukitaka kuwa bilionea, basi kuwa dalali wa kidigitali. Unganisha watu na huduma wanayoihitaji.

Kila la kheri.

Umeshapata kitabu cha MAiSHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE

Kama bado fanya hivi, tuma elfu sita (6,000/-) kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA Sasa ili upate kitabu hiki cha kipekee sana.


One response to “Fursa iliyotengeneza mabilionea kwenye karne ya 21”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X