Asilimia 99 ya Maisha ya Watu Hujihusisha Na Vitu Hivi


Leo nimekuandalia vitu ambavyo huwa vinachukua muda wa watu japo huwa havina manufaa yoyote kwao. Ni jukumu lako kuvifahamu na Kisha kuamua kuachana navyo.

1. Watu wengi hupoteza muda mwingi wakihofu jinsi watu wengine wanavyowafikiria, wakati na wao wanahofu wanasemwaje.

2. Watu wengi huishi maisha kwa kutaka kuwaridhisha wengine; wakati mtu pekee wanayepaswa kumridhisha ni wao wenyewe.

3. Watu hutumia muda mwingi kwenye mahusiano yanayowaumiza wakitarajia  yatakuwa mazuri muda wowote.

4. Watu wengi hutumia mida mwingi kuongea umbea na kuwasema watu. Ukweli ni kwamba mtu anayemsema mwingine mbele yako. Atakusema na wewe mbele ya wengine.

5. Watu wengi hutumia muda mwingi wakijaribu kuishi aina fulani ya Maisha ili waendane na jamii husika. Kitu ambacho huwa kinawafanya wasiishi uwezo wao halisia.

6. Watu wanatumia muda mwingi kufanya kazi ambayo hawaipendi. Wakishindwa kutoa hata dakika kidogo tu za kufanya kitu wanachopenda.

7. Watu wengi wanatumia muda mwingi kutafuta fursa nzuri ya kufanyia kazi. Kitu ambacho huwa kinawafanya wakimbizane kutoka fursa moja kwenda nyingine.

Pata nakala ya kitabu cha MAiSHA NI FURSA: ZITUMIE ZIKUBEBE Leo kwa elfu sita (6,000/-)

Tuma sasa elfu 6 kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA.

KARIBU
NI MIMI
GODIUS RWEYONGEZA
+255755848391
MOROGORO-TZ


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X