Vitu Kumi Na Tatu Vya Kufanya Kipindi Hiki Ambapo Gharama Za Miamala Ya Simu Imepanda Bei


Kusikiliza makala hii kwa sauti BONYEZA HAPA

Kuanzia juzi tarehe 15 julai, mitandao ya simu imepandisha gharama za kutuma na kutoa fedha ambapo kwa sasa kwa baadhi ya miamala gharama ya kutuma na kutoa fedha ni mara mbili ya ilivyokuwa hapo mwanzo. Kuna utani kuwa sasa hivi itakuwa bora kumtuma bodaboda fedha zako apeleke kwa mlengwa kuliko kutuma fedha kwa kutumia mtandao wa simu. Huku wengine wakisema kuwa hii sawa na kodi ya kichwa iliyotolewa miaka ya nyuma na sasa hivi imerudi kivingine. Sasa nimeona nikwambie ni mambo gani ambayo unaweza kufanya kwenye Kipindi hiki ili usije kuumizwa na kupanda kwa gharama hizi badala yake  uwe wa kufurahia

Kabla sijakwambia nini cha kufanya, nataka ujue kwamba MATAJIRI hawaathiriki na miamala hii. Hawaathiriki sana kwa sababu miamala yao mikubwa inafanyika kibenki na wengine ndiyo wanamiliki mitandao yenyewe tunayotumia kutuma na kupokea fedha.

Sasa wewe unadhani hawa wataathirika na kupanda au kushuka kwa miamala? Hapana
Ninataka na wewe uingie kwenye hili kundi la watu wasioathirika, yafuatayo ni mambo ambayo unaweza kufanya;

1. Ongeza kipato chako
Ongeza kipato chako. Ni wazi kuwa kipato chako kikiongezeka utakuwa umepunguza makali ya miamala na pengine katika harakati za kuongeza kipato chako kuna chanzo ambacho kinaweza  kuwa kinakupa  utakuwa  keshi mkononi badala ya kulipwa kwa miamala.
Lakini pia hiki ni kitu cha kwanza ambacho unapaswa kupambania maana kama kipato chako kitakuwa chini, ukaongeza na makato yatakayofanyika ni wazi kuwa utaumia sana. Hivyo, ili usiumie. Ongeza kipato chako.
Naomba nimalizie pointi hii kwa kukumbushia wimbo wa 20% anaysema;
Tuliza moyo wako
Kubali mapungufu yako
Rahisisha mahitaji yako
Ongeza kipato chako
Chunga tamaa mbaya *4

2. Ongeza thamani yako
Kama huwezi kuwapiga ungana nao. Huu ni usemi ambao unapaswa kuanza kuuishi. Ni wazi kuwa huwezi kubadili hili la kupanda kwa miamala kwa asilimia 💯. Kwa asilimia kubwa tu utaishia kulalamika, tena wakati mwingine mtandaoni huku maoni yako mazuri yakiwa hayafiki kwa walengwa. Hivyo basi,  cha kufanya ongeza thamanj yako zaidi ya ilivyokuwa mwazo.

Kama watu walikuwa wanakulipa elfu 20 ongeza thamani yako ili ulipwe mara mbili mpaka mara kumi zaidi hii itapunguza makali ya makato kwako.

Ebu tazama  video hii chini ujifunze jinsi ya kuongeza thamani yako

3. Fanya miamala michache 
Badala ya kuwa unafanya miamala mingi tena midogo midogo, fanya miamala michache mikubwa ili kupunguza kuongezeka kwa makato.

4. Wekeza kwenye haya makampuni
Japo asilimia kubwa ya tozo zilizoongezeka ni kodi ya serikali ila kwa ile fedha ambayo kampuni inapata na wewe unaweza kujiweka kwenye orodha ya watu wanayoinyakua kwa kuwa mmojawapo wa wamiliki wa kampuni hizo.

Unaweza kujiuliza nawezaje kuwa mmiliki wa kampuni za mitandao ya simu. Jibu ni kwamba kwa kampuni ambazo zipo kwenye soko la hisa unaweza kuwa mmojawapo wa watu wana wanaozimiliki kwa kununua hisa zake ili mwisho wa siku zikipata faida na wewe upate walau gawio hata Kama ni kidogo. Hii ni namna nyingine ya kutimiza ule usemi wa kama huwezi kuwapiga basi ungana nao. Kitabu Cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE pamoja na kitabu cha SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA vinaweza kuwa msaada mkubwa kwako kwenye hili. Kuvipata tuma rusha elfu nne (4,000/-) kwa namba 0755848391 ili utumiwe vitabu hivi.

5. Kama kuna uwezekano wa kumkabidhi mtu keshi, fanya hivyo.
Kama mtu unayepaswa kumtumia fedha hayuko mbali, fanya utaratibu wa kumkabidhi keshi badala ya kufanya muamala ambao wewe utakatwa kiwango kikubwa na yeye atakatwa kiwango kikubwa tena (double taxation).

6. Kama kuna watu wawili wapo karibu watumie muamala mmoja
Badala ya kufanya miamala miwili tofauti ambayo itakugharimu sana, unaweza kufanya muamala mmoja, kama watu wako karibu na mmoja akapokea fedha ya kwake na nyingine akampa aliyebaki.

7. Ongeza mzunguko wa fedha kwenye biashara yako au huduma unayotoa.
Huu sasa ni muda wa wewe kutafuta wateja zaidi ya ilivyokuwa hapo awali. Badala ya kuridhika na wateja wachache, ongeza idadi ya wateja ili uongeze kipato chako zaidi.

8. Washawishi wateja wako walipe kwa cash badala ya kutuma kwa simu. Hii itakuondolea makato kwa asilimia 100.

9. Waambie watume na ya kutolea. Kama ulikuwa unatoa huduma ambayo Watu wanapaswa kulipia kwa simu, unaweza kuwaambia watu wawe wanatuma na ya kutolea. Jambo Hili litakufanya wewe usibebe mzigo mkubwa wa kukatwa fedha yako unapoenda kutoa.

10. Waambie wakutumie fedha benki
Kwa kuwa makato ya benki bado ni mazuri basi tuhamie benki. Ebu nenda ufungue akaunti benki, kisha waambie watu wawe wanakutumia fedha benki badala ya kutuma kwa simu. Makato ya benki ni ya kawaida.
Kwa upande wangu ukitaka kulipia kitabu changu chochote kwa njia benki basi fanya hivyo kupitia huyo wakala wa NMB aliye karibu nawe kwa akaunti namba 22110047274 jina ni GODIUS RWEYONGEZA. Utatuma risti na kuniambia kitabu gani unataka ili nikutumie. Ebu nenda ujaribu kutuma kwa benki leo na ulipie kitabu cha MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA, HATIFUNGANI NA VIPANDE uone nitkavyokutumia kitabu punde tu baada ya kuona risti yako. Nenda sasa.

11. Waanzishie ndugu zako mradi
Hiki ni kitu kingine muhimu sana ambacho unahitaji kuzingatia. Kama ulikuwa unalazimika kutuma fedha kwa ndugu kila mara, sasa unaweza kuwaanzishia mradi ambao utakuwa unawaingizia fedha hukohuko walipo na hivyo kukupunguzia adha ya kutuma fedha kila wakati.

12. Kuwa na laini sawa na walipaji wako.
Gharama za miamala zimeongezeka, lakini pia gharama za kutuma mitandao mingine ni kubwa zaidi. Ni bora watu wawe wanakutumia fedha ndani ya mtandao husika badala ya kutuma mitandao mingine ili kupunguza makali. Hivyo, kuwa na laini tofauti tofauti za simu ili watu wachague wenyewe ipi itawafaa zaidi.

13. Punguza matumizi yako
Hiki ni kipindi ambapo wewe unapaswa kupunguza matumizi yako, maana fedha yako yenyewe tu ni ya mawazo halafu wewe unaiponda kama vile utaishi milele, utaendelea kunyongwa na haki yako hutapewa. Hivyo basi, badala ya kusubiri upewe haki yako, itafute mwenyewe kwa nguvu zote. Anza kubana matumizi ili fedha ya ziada inayopatikana uiwekeze na kukuza uchumi wako binafsi.

Unachopaswa kufahamu ni kuwa, ukiendelea kuwa mnyonge hakuna atayekuvumilia. Badala yake utanyongwa zaidi ili utoweke. Na hayo siyo kwamba ninayasema mimi, iko hivyo.

Kanuni ya Darwin inaonesha kuwa vitu vinyonge ndio huwa vinatoweka kwanza kabla ya vyenye nguvu. Shauri yako wewe ukiendelea kujiita mnyonge…

Hayo ndiyo mambo 13 unayoweza kufanya kipindi hiki ambapo miamala ya simu imeongezeka.

TAARIFA MUHIMU: Napenda ufahamu kuwa ile ofa ya kupata vitabu vinne kwa shilingi elfu nne tu bado inaendelea. Hakikisha haukosi fursa hii ya kipekee sana. Maana dirisha zamu hii likifungwa ndio litakuwa limefungwa. Kwa hiyo basi hakikisha unakuwa miongoni mwa watu wanaopata vitabu hivi kwa hiyo bei ya vocha.
Rusha elfu nne (4,000/) kupitia
Mpesa 0755848391
Airtel money: 0684408755
NMB: 22110047274
Kote jina ni GODIUS RWEYONGEZA.
Baada ya kutuma, nitaarifu ili nikutumie vitabu hivi vya kipekee.

Fanya hivyo maana ofa hii haitadumu kwa muda mrefu.

Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesuscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

kila la kheri


One response to “Vitu Kumi Na Tatu Vya Kufanya Kipindi Hiki Ambapo Gharama Za Miamala Ya Simu Imepanda Bei”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X