Faida Za Kuwa Blogu Ambazo Hakuna Mtu Amewahi Kukwambia


 

Siku ya leo nitakuwa nikijibu malalamiko yaliyotewa na mmoja wa wasomajj kwenye kundi la WhatsApp Talent School. 

Hili ni kundi maalumu kwa ajili ya watu wenye vipaji vyao na jinsi wanavyopaswa kuviendeleza. Huyu msomaji aliiandika ujumbe uliosomeka hivi:

Mwanzoni Madarasa yalikuwa yanatumwa tunasoma humu, nowadays ni Blogs tuu🤭

Kujibu malalamiko yake niliandika hivi

Mpaka sasa blogu imeonesha kuwa njia bora ya kushirikishana  maarifa kuliko njia nyingine za kutumia mitandao ya kijamii.

Nikikwambia hapa nitafutie makala niliyoandika 2017 kwenye hili kundi la WhatsApp Talent School, huwezi kuitafuta na kuipata. Ila nikikwambia ingia songambeleblog.blogspot.com na tatuta makala ya mwaka 2017 au ya kabla ya hapo. Utazipata zooote.

Maarifa haya tunayoshirikisha hapa yanahitajika kwa watu sasa hivi na baadaye pia.

Kuna mtu anaweza kuja mwaka 2024 anauliza swali ambalo ulishaliandikia mwaka 2019. Unachofanya unaingia kwenye blogu, unatafutia makala na kumpa asome wewe unaendelea na mambo mengine.

Kuna faida nyingi za blogu na nimekuwa naandika sana, sema wengi hawachangamki. Ukiwemo wewe😀😀

Blogu ni kama ATM. Inafanya kazi saa 24 siku 7 za wiki. Iwe umelala au upo macho.

Nashauri kila mtu awe na blogu yake. Ni sehemu nzuri pia ya kuongeza kipato.

Kwa atakayehitaji, aje inbox nimsaidie kutengeneza na kumwonesha njia za kuongeza kipato kwa blogu.

Malipo kidogo tu yatahusika😊😊 

Blogu pia ni sehemu ya wewe kuonesha kipaji na ujuzi wako. Zamani ilikuwa ili unoe kipaji chako ulipaswa kuwa chini ya mwalimu au kuwa kwenye nyumba za vipaji. Siku hizi unaweza kunoa kipaji chako na kujenga wafuasi wanaokufuatilia mapema tu unapogundua kipaji chako kupitia blogu au YouTube. Huhitaji kuanza kuwapigia watu magoti ili wakukubalie na kukupa nafasi. 

Ni sehemu ya kujenga ujuzi pia kama hauna. Mfano unataka kujifunza uandishi unaweza kuanzia kwenye blogu. Ukaandika makala na watu wakawa wanasona na kukupa mrejesho. Mrejesho ambao unakusaidia kuboresha uandishi wako.

Blogu inakusaidia kujua watu wako wanahitaji nini zaidi. Nikiandika makala na kuiweka hapa kundini, siwezi kupata uhakika wa watu wangapi wameisoma, ila kwenye blogu ninaona na makala ambazo zinapendwa na watu wengi zaidi ninaziona. Kitu kinachonisaidia kupaga namna nzuri za kuandika kuwalenga hao watu.

Kiufupi, zama zimebadilika, maisha nayo yamebadilika. Wewe tu ndio hujabadilika. Zamani aliyekuwa na kiwanda ndiye aliyekuwa na nafasi nzuri ya kutengeneza fedha na utajiri. Siku hizi huhitaji kumiliki kiwanda. Unahitaji kumiliki blogu au tovuti.

Blogu inakufanya uonekane mtaalamu. Ukienda sehemu unaongea na watu ukawaambia kuwa wewe una blogu, daah, asikwambie mtu, kila mtu ataanza kukuchukulia tofauti.

Blogu inakufanya upate fursa ambazo huwezi kuzipata kama hutakuwa na blogu. 

Siku hizi mtu akiwa na tatizo, sehemu ya kwanza kukimbilia ni google kutafuta kile kinachomtatiza. 

Na mtu anapotafuta matokeo yanayooneshwa pale kwa asilimia kubwa ni yale yaliyo kwenye blogu au tovuti na siyo kwenye whatsap. Kitu hiki kimefanya watu waingize fedha nyingi 

Kuna rafiki yangu namfahamu alikuwa na blogu inayohusu Mambo ya wanyama (wildlife). Siku moja watu wa nje ya nchi waliitembelea na kuiona. Walimtafuta na kutaka kuinunua hiyo blogu. Akakataa. 

Walipoona hataki wakaamua kufanya partnership naye. Chezea blogu wewe.

Shauri yako.

Wewe endelea kujiunga na kifurushi Cha whatsap tu ili fursa ziendelee kukupita.

NB.  Hili andiko ninaenda kuliweka kwenye blogu, ili miaka minne ijayo uweze kulisoma tena nina hakika hapa kwenye whatsap litakuwa limeshapotea kitambo.  😊😊

Kama utapenda kufungua  blogu tuwasiliane kwa 0755848391

Umekuwa nami,

GODIUS RWEYONGEZA

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

kila la kheri


One response to “Faida Za Kuwa Blogu Ambazo Hakuna Mtu Amewahi Kukwambia”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X