Watu wengi wanadhani kuwa ukiweka malengo tu basi kinachofuata inakuwa ni tiketi ya wewe kuyafanikisha. Siyo hivyo. Kuna vitu vinahitajika ili kukusaidia wewe kufanikisha malengo yako. Na kwa leo nitakushirikisha aina tano za ujuzi unaouhitaji ili uweze kufikia malengo yako.
1. Unahitaji ujuzi wa kuweka malengo sahihi. Siyo kila lengo ni sahihi kwako. Na siyo kila njia unayoitumia kuweka malengo ni sawa. Malengo mazuri yanapaswa kueleweka.
Yanapaswa kuwa yanapimika
Yanapaswa kuwa yanafikika
Yanapaswa kuwa yanaendana na ndoto au kusudi lako la maisha.
Yanapaswa kuwa na ukomo au muda ambapo yatakamilika.
2. Unahitaji ujuzi wa kuchukua hatua.
Baada ya kuweka malengo haitoshi tu wewe kuendelea kushikilia kuwa una malengo badala yake unapaswa kuchukua hatua ili uweze kuyafikia hayo malengo yako.
3. Unahitaji ujuzi wa kuyaandika malengo yako kila siku. Kila siku na kila Mara jikumbushe malengo yako, Kisha tafuta namna ambavyo utafanya kitu kuhakikisha lengo au malengo uliyoweka, unayafikia.
4. Unahitaji ujuzi wa kuwashawishi watu washirikiane na wewe au wakusaidie kufanikisha lengo lako. Ni wazi kuwa katika safari ya kufanikisha malengo yako, huwezi kutembea peke yako, unahitaji watu na hapo ndipo unahitaji kuwa na ujuzi wa kuwashawishi watu ili waweze kukusaidia kwenye Safari yako.
5. Unahitaji ujuzi wa kunga’ang’ania kile unachofanya mpaka pale utakapokikamilisha au kukipata.
Kila la kheri.
Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza
Hakikisha Umesuscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA
Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA
Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA
Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391
kila la kheri
4 responses to “Aina Tano Za Ujuzi Unaouhitaji Ili Uweze Kufikia Malengo Yako”
Kazi nzuri Mr Godius
KARIBU SANA, WASAMBAZIE WENGINE ILI NAO WANUFAIKE
[…] Aina Tano Za Ujuzi Unaouhitaji Ili Uweze Kufikia Malengo Yako […]
I need more knowledge