KAMA UNAFIKIRI KILA KITU KILISHAANDIKWA, FIKIRI TENA (SABABU 18 Kwa Nini Tunaandika Vitabu na Tutaendelea Kuandika Vitabu, Na Kwa Nini Wewe Unapaswa Kuandika Cha Kwako)


 

  Ok! Juzi kuna mtu alinifuata inbox kwangu na kuandika ujumbe mfupi unaosema kila kitu kilishaandikwa.

Nilishangaa kidogo kuuona ujumbe huu, ila baadaye nikakumbuka kuwa kwenye group mijawapo la whatsap Kuna mtu ambaye alikuwa ameuliza swali linalosema

Jamani habari za humu, 
Hivi mimi nitakuwa mwandishi kamili lini

Kujibu swali niliandika kwa kifupi mno nikisema,
Utakapoanza kuandika na kuonesha kazi zako.

Sasa kumbe mtu huyuhuyu ndiye aliyenifuata inbox kwangu kwa muda wake na kuniachia ujumbe unaosema, kila kitu kilishaandikwa.

Nilimjibu kwa kuuliza unamaanisha nini? Na Sasa namjibu tena kwa kirefu kwa kumwambia, kama UNAFIKIRI KILA KITU kilishaandikwa basi fikiri tena.

Siyo kweli kwamba kila kitu kilishaandikwa kama ambavyo unaenda kuona hapa chini lakini hata vile ambavyo vimewahi kuandikwa vinaweza kurudiwa kuandikwa upya katika namna nyingine kutokana na sababu kadhaa. Sasa ili kujibu hoja ya rafiki yangu anayesema kila kitu kilishaandikwa kwenye andiko hili nitajikita zaidi kwenye sababu zinazotusukuma kuandika vitabu. Bila kuongeza cha zaidi naomba nianze Kwa kusema tunaandika vitabu kwa sababu.

1. KUNA TAFITI NA GUNDUZI MPYA ZINAZOFANYIKA KILA MARA

Kuna GUNDUZI na tafiti  mbalimbali ambazo zinafanyika mara kwa mara. Ili gunduzi hizi na tafiti hizi ziweze kuwafikia watu vizuri lazima ziandikwe. Na njia mijawapo ya kuandika tafiti hizi pamoja na guduzi hizi ni kupitia vitabu pamoja na majarida. Ukisema vitabu visiandikwe maana yake hata hizi gunduzi zisiandikwe wala kutafsriwa kwa watu.

Ebu fikiria labda daktari ambaye amegundua dawa ya ugonjwa fulani, asiandike kitu kuhusu ugunduzi wake? Hayo matumizi ya hiyo dawa na yenyewe yalishaandikwa SI ndio? Kumbe kama UNAFIKIRI KILA KITU kilishaandikwa basi fikiri tena.

2. MAARIFA MAPYA
Ebu kwa mfano tuseme kwamba, mwisho wa kuandika vitabu ungekuwa mwaka 1999. Hii ilikuwa kabla intaneti haijashamiri, Facebook na mitandao yote ya kijamii ilikuwa Bado. Google yenyewe ilikuwepo ila haikuwa kama ilivyo leo. Sasa je, haya mambo  yote ambayo yameongezeka yaachwe bila ya kuandikwa?

Sasa hivi kuna vitabu kuhusu Facebook, Instagram, whatsap, au Twitter. Vipo vinavyozungumzia madhara ya hii mitandao, lakini pia Vingine vinaeleza namna bora ya kuitumia hii mitandao kwa manufaa na
Vyote hivi vimeweza kuwepo kutokana na maarifa yaliyopo ambayo hayakuwepo kabla ya mwaka 1999. Tafuta popote, hutakuta kitabu kuhusu Facebook kilichoandikwa mwaka 1999.

Lakini hata vingine vilivyoandikwa miaka hiyo, unakuta sasa hivi vinaboreshwa kutokana na ongezeko la maarifa au maarifa mengine kupitwa na wakati. Mfano kitabu kilichoandikwa mwaka 1999 kuhusu ugonjwa wa kansa, NI wazi kuwa kufikia mwaka huu kiwe kimefanyiwa marekebisho au kiwe kinafanyiwa marekebisho maana Kuna maarifa mengi sana yameongezeka kwenye hiki kipindi tangu kitabu kiandikwe.

Ebu fikiria pia kitabu kuhusu kompyuta kilichoandikwa mwaka 1999 siyo kitabu cha kompyuta kinachoandikwa leo. Kompyuta zenyewe zimebadilika. Matumizi ya kompyuta yameongezeka, watumiaji pia wameongezeka.
Kuna vitu vingi sana tunavyo kwenye kompyuta za leo ambavyo havikuwepo kwenye kompyuta za 1999. Hivyo, leo hii huwezi kuniambia eti kila kitu kilishaandikwa wakati mabadiliko Kama hayo yanatokea kila mara.

Mwaka 1960 walikuwa wanakula wali, pialau, maharage, karanga, nazi na vyakula vinginevyo. Ila hawakuwa na maarifa ya kutosha kuhusu hivi vitu kama ilivyo leo. Sisi leo tunakula vyakula hivi tukiwa tunajua mpaka sayansi yake. Inawezekena kipindi hicho walikuwa wanaweka chumvi kwenye chakula kwa ajili ya ladha, ila leo hii tunajua kuwa chumvi kwenye chakula nI zaidi ya ladha. Tunajua mpaka manufaa yake. Tunajua ikizidi inakuwaje na ikipungja inakuwaje. Haya yote mi maarifa MAPYA yanayopaswa kuandikiwa vitabuni.  Hivyo, kama UNAFIKIRI KILA KITU kilishaandikwa basi fikiri tena.

3. MATATIZO MAPYA
Kama wewe ni mkulima na ulikuwa ukilima tangu miaka ya 90 utakubaliana nami kuwa  kuna mabadiliko mengi ambayo yametokea kwenye sekta hii na mengine yanaendelea kutokea. Miaka hiyo watumiaji wa mbolea na viwatilifu walikuwa wachache sana, na hata waliokuwa wanavitumia vitu hivi walikuwa hawavitumii kitaalamu. Udongo ulikuwa rutuba, na visumbufu walikuwa wachache.  Lakini sasa mimea inashambuliwa  na magonjwa ambayo hayakuwepo miaka hiyo , wadudu nao hawapo nyuma,

MATATIZO haya yanafanya zifanyike taratibu za kuokoa sekta ya kilimo. Suluhiso linapopatikana, linapaswa kuandikwa kwenye vitabu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Hivyo, MATATIZO kama haya mwisho wa siku yanapelekea vitabu viandikwe ili kuujuza umma kuhusu tatizo lililopo na suluhisho lake lililopatikana hata kama ni la muda mfupi.

Ebu kwa mfano fikiria kuhusu janga la korona ambalo limetikisa dunia na linaendelea kutikisa dunia. Kuna njia zilizotumika kujikinga na ugonjwa huu. Kuna juhudi nyingi zilizofanyika kuokoa maisha n.k.
Haya yote yanapaswa kuandikwa, ugonjwa kama huu unaweza kutokea pengine miaka 100 baadaye. Mimi na wewe tutakuwa tumekufa ila maarifa yatakayokusaidia vitabuni, yatawasaidia sana watu wa kipindi hicho kukikinga na kupata sehemu ya kuanzia katika kutafuta suluhisho zuri zaidi.  Na hata usipotokea (na sisi tunaomba iwe hivyo) Bado wanaweza kusoma na kujua kuwa miaka ya 2020 na 2021 ilitokea Korona. Nina uhakika wapo watakaofurahia hazina kumbukizi Kama hiyo. Kama mpaka Sasa hivi unaendelea kufikiri kuwa kila kitu kilishaandikwa basi fikiri tena.

4. HISTORIA INAZIDI KUANDIKWA

Bila Shaka umewahi kusoma au kusikia HISTORIA mbalimbali, labda historia ya vita ya kwanza na ya pili, jinsi nchi za Arrika zilivyopata Uhuru n.k.
Lakini wakati unasoma hiyo historia, Kuna historia nyingine zinazidi kuandikwa kila siku. Mfano tuseme historia ya Tanzania iandikwe kuishia 1999. Je, SI ukweli kuwa tutakuwa tumesahau Mambo ya kihistoria makubwa na muhimu ambayo yamefanyika na yamazidi kufanyika baada ya hapo? Hivyo, vitabu vinaandikwa na vitaendelea kuandikwa kwa sababu pia historia yenyewe inaendelea kuandikwa kila siku. Kama wewe bado unaendelea kufikiri kuwa kila kitu kilishaandikwa basi fikiri tena.

5. SIKU MOJA TUTAKUFA
Binafsi NI mpenzi sana wa vitabu vya wasifu, tawasifu au kumbukizi. Vitabu hivi hunizamisha ndani kuhusu mhusika, nikiyatafakari maisha yake na kuona jinsi ambavyo mtu aliishi na hivyo kunisaidia mimi kujifunza na kuchukua hatua zitakazokusaidia. Ebu fikiria Kama wewe babu yako angekuwa ameandika kitabu cha maisha yake si ungekisoma wewe? Sasa! Ebu na wewe andika cha maisha yako ili hata watoto na wajukuu zako wake wakisome siku moja. Waambie ulivyozaliwa, kukua, kupambana, kuanguka na kuinuka. Waambie Mambo uliyofanya vizuri na hata Yale uliyokosea, waambie misimamo yako na misingi yako. Waambie ulivyoso a shule ya msingi pengine hata mpaka chyo, uoivyompata mwenza wako, waambie ulivyokuwa unatoroka shuleni au uoivyokuwa unachapwa kwa sababu ya kutojua hesabu na mengine mengi.

Tukiacahana na hayo ni ukweli kwamba inawezekana kuna vitu unajua kuhusu kitu fulani. Wewe hutaishi milele yote kuendelea kutoa maarifa haya kwa vizazi vingine. Ila ukiyaandika yanakuwa ya manufaa hata ukishakufa. Bado watu wanaweza kunufaika na ujuzi wako na ukawasaidia katika vitu wafanyavyo. Kama bado UNAFIKIRI KILA KITU kilishaandikwa basi fikiri tena.

6. KUONGEZA MAARIFA
Hivi ninavyoaandika hapa nipo naendelea kusoma kitabu Cha BRAIN RULES FOR BABY Cha John Medina.

Mimi siyo daktari wa binadamu kusema kwamba najifunza kuhusu ubongo ili nifanye MATIBABU yangu vizuri. Wala siyo kwamba Mimi ni daktari wa wanayama na wala sikaribii kwenye kimojawapo. Lakini nipo hapa nyumbani kwangu nikiwa nasoma kitabu hiki kwa manufaa yangu mwenyewe. Kitabu hiki kimesheneni maarifa ya kutosha kuhusu ubongo wa mtoto kuanzia siku mimba inapotungwa mpaka mtoto anapokuwa na miaka mitano (japo maarifa haya unaweza kuyatumia hata mtoto akiwa ameshakuwa na zaidi ta miaka mitano).

Hii ndiyo kusema kuwa Kuna watu wanapenda kuongeza MAARIFA kuhusu mada fulani. Na njia nzuri ta kuongeza MAARIFA ni kupitia vitabu. Vitabu vinakuwa vimeambatanisha maarifa kuhusu mada husika kiundani kiasi kwamba mtu anapoamua kukisoma anajifunza mengi yanayomsaidia msomaji. Hivyo, vitabu vinaandikwa pia kwa ajili ya watu wa aina hii ambao wanapenda kuongeza MAARIFA

7. HATUTAKI KIZAZI CHA SASA WALA KIJACHO KIANGAMIE
Imeandikwa. Ndiyo, imeandikwa kuwa watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Sasa unajua maarifa haya ya kuwasaidia watu wasiangamie unayapata wapi? Yamo vitabuni. Kwa hiyo tunaandika vitabu ili kuwasaidia watu wasije wakaangamia.  Na hapa kuangamia ninakosema siyo tu kwa kuangamia kwa kuwa dhambi.
Bali kuangamia kwa kuangamia kwa kuingia kwenye madeni kwa sababu ya ukosefu wa maarifa sahihi ambayo ungeweza kuyapata kwa kusoma kitabu tu.
Au kuangamia kwa kushindwa kufanikisha malengo ma ndoto kwa sababu ya kukosa maarifa sahihi.

Charlie Munger amewahu kusema kwamba; ninataka kujua hatari ilipo ili niiepuke. Vitabu pia vinawaeousha watu na zilipo hatari. Hii ni kutokana na ukweli kuwa unaposoma kitabu unakuwa unakusanya maarifa, ujuzi na uzoefu ambao mtu ameukusanya kwa miaka mingi sana, ila wewe unaupata kwa wiki au mwezi tu. Hivyo, kwa jinsi hiyo unakuwa umeepuka hatari ambayo ingetokea bila ya wewe kuwa na maarifa husika. Unakuwa umeepuka kuangamia. Napenda kukwambia kuwa tutaendelea kuandika vitabu kwa sababu HATUTAKI KUONA WATU WANAANGAMIA na wewe kama bado  UNAFIKIRI KILA KITU kilishaandikwa basi fikiri tena.

8. UJUZI UZOEFU NA UBOBEVU WETU
Wewe umezaliwa katika mazingira tofauti na watu wengine, umesomea shule ya tofauti na walio wengi, umebobea kwenye kitu cha tofauti na wengine. Kipaji chako na ujuzi wako ni tofauti na wa mwingine. Hivi vitu kwa pamoja vinafanya kitabu utakachoandika kiwe cha tofauti.

Pengine umekuwa unafuga ng’ombe wa maziwa kwa miaka 5 na zaidi. Na sasa unajua kila kitu linapokuja suala zima la ufugaji wa ng’ombe wa maziwa. Wakati huohuo Kuna mtu ndiyo kwanza anataka aanze kufuga. Hajui hili wala lile. Wewe umelalia maarifa ambayo yangeweza kumsaidia huyu anayeanza. Sisi tunaandika vitabu kwa sababu HATUTAKI KULALIA MAARIFA wanayohitaji wengine. 

9. HATUKOMI KUJIFUNZA na TUNAPENDA KUJIFUNZA PIA
Sababu nyingine ya kwa nini vitabu vitaendelea kuandikwa ni KWA SABABU watu hatuachi kujifunza. Kitu hiki kinatufanya tuwe na maarifa ambayo pia yanahitaji kuandikiwa vitabu vyake.

Binafsi nimeandika andiko hiki kwa sababu ya kauli yako. Laiti Kama ningekuwa nimeitafsiri vibaya nisingeweza kuandika chochote. Ila kwa sababu nimejifunza kitu kutokana na kauli yako, ndiyo maana niemweza kuandika ujumbe huu.

Unaweza kushangaa kidogo hapa na unaweza kujiuliza pia. Kama mnaandika vitabu kwa sababu mnapenda kujifunza kwa nini msijikite tu kwenye kusoma vitabu ambavyo vimeandikwa. Ninasema hapana, tunaandika vitabu kwa sababu kwa TUNAPENDA KUJIFUNZA. Na hii inatokana na ukweli kuwa, unapoandika kitabu bila kujali wewe NI mtaalamu kiasi gani. Utahitaji Sana kujifunza zaidi, kusoma vitabu vingine na tafiti nyingine. Hivyo, kuandika kitabu tu kunakufanya ujifunze zaidi na usome vitabu zaidi.

10  HATUNA MUDA WA KUTOSHA KUZUNGUKA KILA SEHEMU
Ebu fikiria wewe mtaalamu katika eneo fulani na watu wanahitaji maarifa yako kwa sana. Huwezi kuwa unakutana na kila mtu kwa muda wake na kuanza kuongea naye kumweleza kila kitu unachojua na kisha kwenda kwa mtu mwingine. Muda wetu NI saa 24 tu kwa siku na tuna mambo mengi ya kufanya.

Lakini kitabu kina nguvu ya kukufanya uwafikie watu Wengi kwa wakati mmoja. Hata Kama wako mbali na mahali ulipo. Kumbe kitabu kinakusaidia kuwafikia wengi huku ukiendelea kufanya kazi zako.

Kama we’re NI mchungaji, mhubiri, askofu, padre n.k. unaweza kuhubiri watu wengi hata wa mbali kupitia kitabu chako hata kama hao watu hawaji kanisani kwako moja kwa moja.

Kama wewe NI daktari unaweza kuponya wengi kwa kitabu chako hata Kama watu hao hawaji hospitalini kwako Moja kwa moja.

Kama wewe mtaalamu katika kitu fulani, utalaamu wako unaweza kusaidia Wengi kupitia kitabu hata Kama watu hao hujaonana nao Moja kwa moja.

Kitabu kinaokoa muda wa wewe kuongea na hawa watu. Chenyewe kinaongea nao huku kikisimama kwa ajili yako. Hivyo na wewe andika kimoja, Kama bado utaendelea kufikiri kuwa kila kitu kilishaandikwa basi fikiri tena.

11. KWA SABABU VITABU VILIVYOTANGULIA HAVIKUANDIKA KILA KITU
Kwenye pointi ya sita nimekudokeza kuhusu kitabu Cha The Brain Rules For Baby  ninachosoma. Kitabu ambacho kimezungumzia kuhusu ubongo hasa kwa upande wa mtoto na jinsi unavyoweza kutumia maarifa yakiyo kitabuni kumlea mwanao. Hata hivyo, kitabu hiki siyo mwanzo na mwisho kwenye suala zima la ubongo. Hivyo, uwepo wa kitabu hiki haumzuii mtu mwingine kuandika kitabu kingine kuhusu ubongo. Ndiyo maana Kuna kitabu kingine kama Cha Ben Carson kinachoitwa You Have The Brain (Nina mpango wa kukisoma pia nikimaliza hiki).

Hali kama hii pia ndiyo inatufanya tuandike vitabu vingine. Maana hakuna kitabu kimoja kilichoandikwa mambo yote duniani. Kila kitabu kinachagua mada moja na kuizungumzia kwa kina na hivyo kuwaachia uwanja wengine uwanja mwingine wa kuandika.

Ukisema watu wasiandike ni sawa na kusema watu wasifanye tafiti zaidi maana zilishafanyika huko nyuma.

Lakini tunachoona kwenye ulimwengu wa sayansi na tafiti uwepo wa kitu fulani unasasaidia ujio wa kitu kingine. Utafiti fulani unaweza kuwa chanzo cha utafiti mwingine. Au unaweza kusema mtafiti mmoja anachokoza wengine kufanya utafiti zaidi juu ya hicho kitu au kinachohusiana na hicho.

Hakuna mwanasayansi anakaa ofisini au kijiweni na kusema hakuna jipya sasa. Kila wakati Kuna tatizo ambalo linatafutiwa suluhisho bora zaidi  hivyohivyo kwenye uandishi, kila mara kunahutajika uandishi wa vitabu zaidi.

12. KWA SABABU TUNA KITU NDANI YETU AMBACHO KINAPASWA KUANDIKWA
Siwezi kuwa na kitu fulani cha kuandika halafu nikaacha kukiandika kwa kuogopa eti kwa sababu kilishaandikwa. Hadithi yangu niliyotunga mwenyewe naanzaje kuacha kuiandika na kuiweka kwenye kitabu. Kama nina kitu ndani yangu ambacho ninaona KINAPASWA kuandika ni LAZIMA tu nitakiandika.

13. KWA SABABU KUNA VITABU AMBAVYO TUNGEPENDA KUSOMA ILA HATUVIONI.
Naupenda usemi wa mtu aliyesema; Kama Kuna kitabu ambacho ungependa kusoma ila hukioni basi kiandike.

Hivyo, muda mwingine tunaandika vitabu kwa sababu kuna aina fulani vitabu tungependa kusoma ila hatuvioni hivyo tunaamua kuviandika wenyewe.
Au kuna aina fulani ya uandishi tunaupenda ila hauonekani sokoni, hivyo tunaamua sisi wenyewe kuchukua usukani.

14. HATUTAKI VISINGIZIO Wala HATUOGOPI KITU
Kusema kila kitu kilishaandikwa NI kisingizio cha wazembe na watu ambao hawapendi kuchukua hatamu ya maisha yao. Watu wanaoogopa watachukuliwaje endapo wataandika na kuonesha kazi zao. Hata hivyo, sisi tunaandika kwa sababu HATUTAKI VISINGIZIO na Wala HATUOGOPI KITU.
Kama wewe ni mwoga na mtu ambaye hakosi VISINGIZIO NI lazima tu utaendelea kusema kila kitu kilishaandikwa.

15. NI NJIA MOJAWAPO YA KUELEZA HISIA ZETU
Ndiyo, uandishi NI NJIA MOJAWAPO pia ya kutuliza mawazo, kuondoa stress lakini pia KUELEZA HISIA. MWANDISHI kama binadamu, naye hupitia changamoto mbalimbali. Kuna wakati anakuwa na furaha, hasira, wivu, na mengine mengi.

Kuandika pia huwa kunasaidia kueleza hisia hizi na hivyo kupunguza stress.  

16. KUACHA ALAMA

Robin Sharma kwenye kitabu chake Cha Nani atalia utakapokuwa, ameandika kuwa Kuna vitu vitatu ambavyo unaweza kufanya ili kuacha ALAMA hapa Duniani.

Moja NI kuandika kitabu, pili kuoanda miti na kuzaa mtoto. Hivyo tunaandika vitabu ili kuacha alama pia. Hii inatokana na ukweli kuwa vitabu vina uwezo wa kudumu Karne nyingi Sana hata baada ya wewe kufa.  Hivyo, wewe utaendelea kuishi hata kwa miaka yote hiyo kupitia kitabu chako.

17. KWA SABABU TUNAPENDA KUANDIKA

Uandishi ni mchezo ambao tunaupenda na tumeamua kuucheza, kwa hiyo hatutarudi nyuma. 

18. KWA AJILI YA KUONGEZA KIPATO
Ok sawa, kuongeza kipato siyo sababu ya kwanza Wala ya pili ya kwa nini tunaandika vitabu ila mwisho wa siku na yenyewe inaingia japo haibebi uzito mkubwa kama hizo zilizotangulia.

Kama umesoma makala hio na ungependa kuandika kitabu chako, karibu nikusaidie. Nitakushika mkono kuanzia unapoanza kuandika mpaka kitakapoisha. Gharama yake NI 50,000/- tu. Tuwasiliane kwa 0755848391

Nakushukuru Sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri



3 responses to “KAMA UNAFIKIRI KILA KITU KILISHAANDIKWA, FIKIRI TENA (SABABU 18 Kwa Nini Tunaandika Vitabu na Tutaendelea Kuandika Vitabu, Na Kwa Nini Wewe Unapaswa Kuandika Cha Kwako)”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X