Hii Ndiyo Maana Halisi Ya Nidhamu


Hivi ukisikia mtu anasema mtu fulani ana nidhamu au hana nidhamu anakuwa anamaanisha nini? Je, wewe una una nidhamu? Au ndio ulishasahau mambo ya kuwa na nidhamu tangu ulipohitimu shule? Siku ya leo naomba ufahamu kwamba nidhamu, ni pale unapoamua kufanya kitu kwa utaratibu fulani na ukakifanya bila kuacha.

Umeamua kuwa kila siku utaamka alfajiri saa 11, na unahakikisha unafanya hivyo bila kujali siku hiyo inanyesha au ni jua kali, hiyo ndiyo nidhamu.

Umepanga kuweka akiba ya kiasi fulani cha fedha kila unapopata mshahara, unakiweka bila kujali mwezi huo una matumizi na mambo mengi yanayohitaji fedha au la!

Umeamua kufanya mazoezi kwa dakika kadhaa kila siku au kila wikendi, unafanya hivyo bila kujali siku hiyo una wageni au upo ugenini.

Orodha inayoonesha vitu vya aina hii inaweza kuwa nyingi sana ila walau msingi mkubwa wa nidhanu ndiyo huo.

Nikukumbusha tena; nidhamu, ni pale unapoamua kufanya kitu kwa utaratibu fulani na ukakifanya bila kuacha bila kujali kitu gani kinatokea au kimetokea.

Kazi ya kufanya siku ya leo.
Chagua kitu kimoja hata kama ni kidogo sana (hata kama ni kuweka akiba ya shilingi 100 kola siku). Kisha azimia kukifanya kila siku au kila wiki bila kuacha. Na ukifanye kweli kwa mwaka mmoja ujao.

Nakutakia kila la kheri.

SOMA ZAIDI:

Viashiria Vitano (05) Vitakavyokufanya Uendelee Kuwa Maskini Maisha Yako Yote

 NI MARUFUKU KUKATA TAMAA

Nakushukuru Sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri



One response to “Hii Ndiyo Maana Halisi Ya Nidhamu”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X