MAISHA NI WAJIBU WAKO


 Kuna watu wanashangaza kweli. Mwaka 2015 walikuwa wanasema maisha ni magumu, hawana mtaji, ajira hazipo n.k.

Mwaka 2020 bado walikuwa wanasema mambo yaleyale. 

Cha ajabu zaidi ni kwamba 2025 watakuwa watu walewale bado watakuwa wanasema yale ya 2015. 

Sasa kwa nini? Je. Wewe ni mmoja wao. Unapaswa kubadilika mara moja.

1. Fahamu kuwa maisha ni wajibu wako, ukishinda ni juu yako na ukishindwa ni juu yako. (Beba jukumu la maisha yako)

2. Anza leo kubadili hali ambayo huitaki. Usisubiri mtu mwingine aje kukusaidia.

3. Jifunze mara kwa mara kwa kusoma vitabu ili ujue mengi yatakayokusaidia kwenye safari yako. Unaweza hata kunitumia ujumbe nikupe kitabu cha MAAJABU YA KUSOMA VITABU bure! 

4. Anza kujiwekea akiba kwa ajili ya kesho yako.

5. Fahamu kuwa rasilimali muhimu za kukusaidia wewe kuanza unazo. Moja ni muda, pili ni akili, tatu ni nguvu zako, nne ni ujuzi au kipaji chako au vyote viwili.

Huna haja ya kuendelea kulalamika. Badilisha kile ambacho hukipendi, kisha songa mbele.

Umekuwa nami

Godius Rweyongeza

0755848391

www.songambeleblog.blogspot.com

MOROGORO-TZ


One response to “MAISHA NI WAJIBU WAKO”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X