Jinsi Ya Kuondokana Na Hofu Ya Kuongea Mbele Ya Watu (How To Overcome The Fear Of Public Speaking)


 

Hivi ni kitu gani ambacho wewe huwa unaogopa sana?  Watu wote huwa Wana kiwango fulani cha uoga kwenye vitu mbalimbali japo uoga hutofautiana.

Hata hivyo, kuna kitu kimoja ambacho kinaonekana Kuogopwa Na watu Wengi. Kitu hiki hapa ni kuongea mbele ya watu.

Huu ndio uoga unaowakumba watu wengi sana pengine na wewe ukiwa mmoja wao. Tafiti mbalimbali zinazoonesha kuwa asilimia 73-77% ya watu wana uoga huu wa kuongea mbele ya watu.  Hii ndiyo kusema kuwa kwenye kikundi cha watu 100, watu 73-77 wanaogopa kuongea mbele ya watu. Huku watu 23-27 tu wakiwa ndio hawaogopi. Hata  hivyo, ukweli ambao  unapaswa kuufahamu ni kuwa katika maisha yako kuna wakati utatakiwa kuongea mbele ya watu. Iwe ni kwenye kikao cha familia, kazini, kuomba kuongezewa mshahara kutoka kwa bosi wako au hata kuongea kwa ajili ya kulipwa. Hivyo, kutokana na ukweli huu huna budi kuhakikisha unaondoka na uoga huu wa kuongea mbele ya watu.

Dalili zinazoonesha kuwa unaogopa kuongea mbele ya watu

Moja, Kama kila ukipata fursa ya kuongea unaikimbia au unatafuta sababu ya kwa nini hutaweza, hata Kama sababu hiyo haina mashiko.

Pili, kutetemeka na kuongea kwa uoga pale unapopata fursa ta kuongea mbele ya watu.

Tatu, kutoa jasho au kutetemeka.

Nne, kuongea kaa kusitasita

Nawezaje kuondokana na hali hii?

Ili tuweze kwenda sawa hapa ninataka nikuibie siri kuhusu watu unaowaona wanaongea mbele ya watu. Siyo kwamba hawa hawana uoga, bali wao wameamua kuwa mbali ya kuwa wana uoga watasimama mbele ya watu na kuongea. Sasa zifuatazo ni mbinu unazoweza kutumia ili kuondokana na hali hii ya kuogopa kuongea mbele ta watu;

Kwanza ijue mada unayoenda kuongelea vizuri. Hapa utapaswa kuhakikisha unaisoma na  kiundani na kufuatilia vyanzo vyote muhimu ili upate taarifa kamili kuhusu hiyo mada. Unapoijua mada husika kiundani inakuwa rahisi kwako kuieleza bila kuteteleka na hata inakuwa rahisi kwako kujua maswali ambayo watu wanaweza kuuliza hivyo kuandaa majibu yake, lakini kikubwa zaidi ni kwamba hata ikitokea umekosea kidogo wakati unatoa mada, inakuwa rahisi kwako kurudi kwenye mstari na kuendelea kutoa mada husika kwa ustadi.

Pili, unapopata nafasi ya kuongea mbele ta watu hakikisha unajiandaa vya kutosha ili ukianza kuongea ujiamini. Hapa unapaswa kufanya mazoezi ya kutosha nje ya pazia ili ukionekana mbele ya watu uweze kuongea kama vile hujawahi kuogopa kuongea mbele ya watu. Unapaswa kufanya mazoezi kiasi kwamba ukianza kuongea watu waseme ni mnenaji kwa asili, kumbe wewe nyuma ya pazia unaweka nguvu kubwa sana.

Wakati wa kufanya mazoezi unaweza kuchagua watu wachache kama watano na kuongea mbele yao. Hawa wanaweza kuwa watu wako wa karibu au wanafamilia wako.

Lakini pia hata kama hauna watu unaweza kuongea mbele ya kioo na hivyo kujiangalia jinsi unayoongea, mwili wako unavyotoa ishara na mengine mengi.

Tatu,  pangilia vizuri pointi zako. Jua ni pointi gani utaanza nayo na pointi gani itafuata. Hi itakusaidia sana wakati unaongea na kutoa hoja yako mbele ya watu. Unaweza pia kurekodi au kuandika pointi zako kwenye karatasi au notebook utakayoutumia wakati unaongea. Japo binafsi huwa sipendelei kutumia notsi wakati wa nawasilisha mada yoyote. Kwangu huwa naiona kama ishara ya kutojiandaa vizuri na kutoijua mada husika kiundani. Kama umejiandaa vya kutosha na unaijua mada kiundani unaweza usihitaji hizi notsi.

Nne, jirekodi wakati unaongea. Hi itakusaidia wewe kujisikiliza na kujua mapungufu au ubora wako na wapi pa kuweka juhudi na nguvu zaidi. Utajua wapi huweki msisitizo wakati panaspaswa kuwa na msisitizo mkubwa, lakini pia uragundua wapi huweki msisitizo wakati panaspaswa kuwa na msisitizo mkubwa.

Tano, weka nguvu kubwa kwenye uwezo wako, kile ulichoandaa na uwezo wako, Wala siyo udhaifu wako. Unachopaswa kufahamu ni kuwa unaposimama kuongea mbele ya watu, fahamu kuwa wewe ndiye unakuwa unajua zaidi kuliko mtu yeyote anayekusikiliza. Hata Kama wapo watu unaowajua kuwa wao wanajua zaidi ya wewe, kitendo cha wewe kupewa nafasi ya kuongea mbele ya watu kwa muda huo kinakufanya wewe kuwa MASTER kwa muda huo. Hivyo, simama kuongea kama mtu anayejua zaidi kuliko wengine.

Sita, kunywa maji ya uvuguvugu na vuta pumzi kwa nguvu kabla ya kusimama mbele ya watu. Hiki kitu nilikisoma kwenye kitabu kimoja, japo sikumbuki ni kitabu gani ila huwa nakitumia. Kunywa maji ya uvuguvugu na kuvuta hewa kwa nguvu hufanya mwili uendelee na shughuli zake kwa ustadi bila kukwama wakati wewe unaendelea na shughuli yako ya kuongea mbele ya watu.

Saba, usiogope kutulia kidogo pale inapotokea kuwa umepoteza mwelekeo wa kile unachoongea. Hapa unaweza kuangalia sehemu ulipoorodhesha pointi zako ili ikusaidie kukupa mwanga wa kule unapoelekea. Lakini pia unaweza kuitumia nafasi hii kuomba swali au kudokeza hata kitu chochote ambacho kinaweza kuwafanya wasikilizaji wako wacheke kidogo huku wewe mwenyewe ukijipanga kuendelea kutoa hoja.

Nane, soma kitabu cha Presentation Secrets Of Steve Jobs.
Ni wazi kuwa kila mtu huwa ana shujaa wake kwenye Mambo mbalimbali. Binafsi linapokuja suala zima la unenaji basi Steve Jobs ni shujaa wangu. Mbinu zake za unenaji ni za nyakati zote, hazichuji na hata kwenye zama hizi za taarifa bado mbinu zake zina nguvu sana. Kama utapaswa kusoma kitabu kimoja kuhusu uneni (public speaking) Basi soma Presentation Secrets Of Steve Jobs. Kina kila kitu unachohitaji kujua kuhusu uneni. Unaweza kudhani nampendelea Steve Jobs. Lakini ebu kwanza jionee nwenyewe hotuba yake aliyotoa mwaka 2007 wakati wa uzinduzi wa iPhone ya kwanza (simu janja ya kwanza ya kupangusa). Hi ni hotuba ambayo  unaweza kujikuta umeifuatilua mpaka nwisho kwa shauku kubwa sana.

Au unaweza kuangalia hotuba yake ya 2005 aliyoitoa akiwa chuo kikuu Cha Stanford. Hii nayo ilikuwa ni hotuba ya viwango Vingine. Ebu ifuatilie hapa:

Ukisoma kitabu hiki mpaka mwisho na kufuata yakiyoandikwa humu, ni wazi kuwa utakuwa mneni Bora wa nyakati zetu.

Nakushukuru Sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X