Maswali Muhimu Unayopaswa Kujiuliza Kabla Ya Kuachana Na Ndoto Yako


Rafiki yangu hongera sana kwa siku hii ya kipekee sana. Jana nilikuwa naongea na rafiki yangu ambaye amekuwa na ndoto kubwa ya kuandika tamthiliya, hata hivyo, amekuwa akihairisha zoezi kwa miaka mingi ni jana tu baada ya kusoma kitabu changu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO alimua kuchukua hatua, akanunua daftari na kuanza moja kwa moja kuandika tamhiliya yake. 

Pengine na wewe inawezekana umekuwa na ndoto kubwa kwa siku nyingi sana ila ndoto hizo hujazifanyia kazi, kwa kughairisha kuwa ndoto hiyo utaifanyia kazi siku nyingine, kitu ambacho kinafanya siku zinazidi kusogea bila ya wewe kufanya kazi yoyote ile kwenye ndoto yako. Au hata inawezekana umeanza kufanyia kazi ndoto yako ila humu katikati ukakutana na changamoto ambazo sasa zimekuzuia kuendelea mbele na kukata tamaa kufanyia kazi ndoto zako. yafuatayo ni maswali muhimu ambayo unapaswa kujiuliza kabla hujafikia uamuzi wa mwisho wa kuachana na ndoto yako.

1. kwa nini uliamua kufanyia kazi hiyo ndoto

Hili ni swali muhumu sana ambalo unapaswa kujiuliza na kuhakikisha umepata majibu yake. Ni kitu gani haswa kilikusukuma hapo mwanzoni ili kuanza kuifanyia kazi hiyo ndoto. Na je, hiki kitu kimeenda wapi? Kwa kujiuliza swali hili inakuwa na sawa na mtu ambaye anajiurudisha kwenye asili yake ya kwanza kabisa na hivyo kupata sababu ya kuweza kuendelea mbele kuifanyia kazi ndoto yako.

2. Je, nikiulizwa kwa nini nimeacha kuifanyia kazi ndoto nitawaambiaje wanaoniuliza?

Hili ni swali jingine ambalo unapaswa kujiuliza. Hivi kwa mfano leo hii ukiacha kufanyia kazi ndoto yako na miaka 10 au 20 ijayo ukaulizwa na mwanao au mjukuu wako, utamwambia ni kitu gani kilikusuma wewe kuachana na ndoto yako. Utatoa sababu gani kwake ili aweze kukuelewa.

Hili ni swali jingine muhimu ambalo litakukakudisha kwenye mtsari na kukufanya uendelee kuifanyia kazi ndoto yako. Kwa kawaida huwa naona kila mzazi anapenda kuonekana shujaa mbele ya watoto na wajukuu wake. ndiyo maana,kila mzazi huwa anapenda kutamba kwamba alikuwa kinara darasani hata kama alikuwa kilaza. Mzazi mwingine atataka kuonesha watoto wake na wajukuu wake kuwa alikuwa kinara kwenye mpira wa miguu miaka kadhaa iliyopita n.k.

Sasa wewe utapenda kuonekana kwamba ulikuwa kinara wa kuanzisha vitu na kuishia njiani. Sidhani kama wewe ungependa kuwa mmoja wao? Pengine labda wewe ndiye utakuwa wa kwanza kuwahadithia wanao na wajukuu wako kuwa ulikuwa kilaza na mtu wa kukata tamaa.

3. Je, ni kitu gani kibaya kinaweza kukutokea endapo utaacha kuifanyia kazi ndoto yako?

Hili ni swali jingine muhimu ambalo unapaswa kujiuliza, tena mara nyingi tu. angalia kama kuna kitu kibaya ambacho kinaweza kutokea endapo hutafanyia kazi ndoto yako.

Mara nyingi utagundua kwamba hakuna kitu kibaya ambacho kinaenda kutokea isipokuwa labda tu unaweza kuwa na uoga. Unaogopa watu watakuchukuliaje endapo utashindwa. Lakini kitu muhimu sana kwako ni kwamba unapaswa kuogopa kutoifanyia kazi ndoto yako.

4. Je, kuna uwezekano wowote kwamba maisha yako yatakuwa bora zaidi endapo utaacha kuifanyia kazi ndoto yako?

Hili ni swali jingine muhimu sana ambalo unapaswa kulijua. Sasa hivi unaweza kuwa unaona kwamba maisha ni magumu na mabovu kutokana na changamoto ambayo unakutana nayo kwenye ndoto yako. Lakini endapo utaacha kuifanyia kazi ndoto yako, utakuta kwamba maisha yako ndiyo yamekuwa mabovu zaidi. sasa swali la kujiuliza ni je, maisha yako yatakuwa bora endapo wewe utaacha kuifanyia kazi ndoto yako?

5. Ni kitu gani haswa kimefikia hatua ya kukufanya uache kuifanyia kazi ndoto yako? 

Ni muhimu kwako kufahamu kitu cha aina hii hapa. unaweza kukuta umekutana na changamoto kubwa ambayo kwa sasa hivi unaona kama haitatuliwi, ila ukiitafakari changamoto hii utapata jibu na kujua namna ya kuitatua. Kingine ni kwamba endapo utaacha changamoto hii bila ya kutatuliwa, unaweza kujikuta kuwa miaka 20 ijayo unaagalia nyuma kwa nini uliamua kuacha, unajiulaumu. Hivyo, kijue kitu hiki, kama ni changamoto itatue. Kama uamuzi huu ni wa kihisia zaidi basi jipe muda kwanza maana uamuzi unaotokana na hisia unaweza kukufanya ujute huko mbeleni

6. Je, kama wewe ndiyo ungekuwa unamshauri mtu kuhusu ndoto yake? Ungemwambiaje? Hivi ni kweli kwamba ungemwambia rafiki yako kwamba aikatie tamaa ndoto yake kwa sababu ya changamoto fulani ambayo anakutana nayo sasa hivi. Nina uhakika kabisa kwamba usingefanya hivyo. Pengine ungemwambia kwamba hiyo ni hali ya kawaida, hivyo avumilie. Au ungemwambia kwamba hali kama hiyo huwa inatokea, asikate tamaa. Sasa kwa nini wewe ukate tamaa? Na kuacha kuifanyia kazi hiyo ndoto yako

Rafiki yangu, hayo ndiyo maswali muhimu unayopaswa kujiuliza kuhusu ndoto yako.  Nimeandika kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO. ni kitabu ambacho kwa hakika kibadili maisha ya watu wanaokisoma. Nina uhakika na wewe ukikisoma kitabu hiki kinaenda kuleta mabadiliko makubwa sana kwenye maisha yako. Kitabu hiki kinapatikana kwa bei ya shilingi elfu 20 ila nimeona nikupe ofa wewe rafiki yangu. Utakipata kitabu hiki kwa elfu 17 tu kama utachukua hatua leo hii

Tuwasiliane sasa kwa 0755848391. Kitabu hiki kinapatikana kwenye mfumo wa nakala ngumu na kitatumwa popote pale ulipo Afrika Mashariki.

Karibu sana.

Umekuwa name

Godius Rweyongeza

www.songambeleblog.blogspot.com

http://jifunzeuandishi.wordpress.com/


One response to “Maswali Muhimu Unayopaswa Kujiuliza Kabla Ya Kuachana Na Ndoto Yako”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X