UMUHIMU WA ENEO KWENYE BIASHARA


 

 

https://www.getvalue.co/home/product_details/mambo_55_ya_kuzingatia_kabla_ya_kuanzisha_biashara
pata nakala ya kitabu hiki kwa kuboonyeza HAPA

Moja ya kitu muhimu kwenye biashara ni eneo. Yaani, unaweza kuwa na biashara nzuri lakini kama hutaiweka eneo zuri basi ni wazi kuwa utakuwa umekosea sana. Ebu chukulia mtu anafanya biashara ya kuuza magari na biashara yake akaiweka kijijini kabisa. japo biashara ni nzuri lakini kwa sababu ya eneo ambapo mtu huyu ameweka biashara yake, ni wazi kuwa ule ujio wa wateja ni kidogo sana au pengine hamna kabisa.

 

Kwenye zama tunazoishi sasa hivi, kila kitu sasa kinapaswa kuhakikisha kimepata eneo zuri ambapo kinaweza kuoneshwa kwa walengwa. Kipaji chako kinapaswa kuoneshwa kwa watu sahihi ili kuonekana. Uwezo wako au ujuzi wako unapaswa kuoneshwa kwa watu sahihi ili uweze kuonekana. Na hili pia linahitaji eneo zuri. Kwa hiyo siku ya leo ningependa kuongelea suala la eneo kiundani. Na leo hii tunaenda kuongelea aina mbili za maeneo ambapo unaweza kuweka kipaji chako.

 

ENEO LA KWANZA NI MITANDAONI

Kiufupi ni kuwa bishara zote kwenye zama hizi zinapaswa kuwa na eneo mtandaoni. Na hili eneo ni kuwa na blogu au tovuti yako ambayo umeitengeneza kitaalamu. Ni kwenye blogu ambapo watu wanaweza kukukuta na kujifunza mambo mengi kuhusu kile ambacho unafanya.

Pengine unaweza kujiuliza; kwani kuna ulazima wa kuwa na blogu? Kwa nini tu nisiwe na ukurasa wa facebook au instagram tu. au kwa nini nisiwe na kundi la whatsap peke yake.

Sawa, nimekuelewa, ila hapa ninachopenda kukwammbia ni kuwa ni muhimu sana kwako kuwa na blogu kuliko hata kuwa na kundi la whatsap au ukurasa wa facenbook. Blogu inapaswa kuwa eneo mama kwako kwenye mtandao, halafu haya maeneno mengine utayatumia tu kama majukwaa ya kukusaidia wewe kuwasiliana na wateja wako kiurahisi.

 

Siku hizi mtu anapokuwa na shida, kitu cha kwanza anachofanya ni kuingia mtandaoni ili aweze kupata kutafuta kile anachotaka. Ni wazi kuwa kama umekuwa unaweka vitu vizuri kwenye whatsap hivyo vitu vyako kwenye whatsa mtu hawezi kuvitafuta google akaviona. Ni mpaka viwe kwenye blogu pia.

Kitu kingine ni kuwa mpangilio wa blogu unamwezesha msomaj wako kuweza kusoma na kusoma zaidi au kujifunza zaidi kutoka kwenye blogu yako. Hata hivyo, ukurasa wako wa facebooka haumwezeshi msomaji wako kufanya hivyo.

Kwa mfano unaweza kuandika kitu kizuri na kukiweka kwenye mtandao wa whatsap leo hii, baada ya wiki msomaji wako akashindwa kukipata tena hicho kitu kama anataka kurejea ili ajifunze zaidi au kama kuna kitu amesahau. Hivyo, unakuwa unamkosesha uhondo wa kujifunza mara kwa mara kupitia kazi yako.

Lakini kibaya zaidi ni kuwa wewe mwenyewe unaweza kupoteza kila kitu ambacho umekuwa unaweka whatsap. Sasa hiki ni kitu ambacho hupaswi kukifanya wakati kuna uwezo wa wewe kutumia mbinu za kisasa kama hiii ya kuwa na blogu.

Usikwame. Fungua blogu yako leo hii. Kama ungependa kupata msasa wa kufungua blogu yako leo hii kwa bei ya elfu 10 tu badala ya elfu 30  fedha sasa kwenda 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA. Nitakutengenezea blogu yako kufikia jioni itakuwa tayari. Kuanzia kesho mapema na wewe utakuwa na blogu yako inayoeleweka.

 

JIFUNZE KWA KUBONYEZA HAPA: Maeneo muhimu unapoweza kuweka nyaraka zako mtandaoni kiusalama zaidi

 

ENEO LA PILI NI LINAOONEKANA AU KUSHIKIKA

Hili ni eneo ambalo tumezoea siku zote. Aina hii ya eneo pia linapaswa kuwa ambapo kuna walengwa wako wa biashara. Kwa mfano huwezi kuweka biashara ya kuuza nguo za kike kwenye bweni la wanaume ukitegemea wanunua. Vivyohivyo kwa nguo za kiume, huwezi kuziweka kwenye hosteli za wanawake, ukitgemea wanunue. Ni lazima tu uhakikishe kuwa umechagua eneo zuri kwa ajili ya biashara yako kulingana na watu ambao wewe mwenyewe umewalenga. Nimeeleza zaidi kwenye kitabu changu cha MAMBO 55 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZISHA BIASHARA. Jipatie nakala ya leo kwa kubonyeza HAPA

UMEKUWA NAMI

Godius Rweyongeza

Mwandishi, mjasiliamali na mhamasishaji.

0755848391

Kupata vitabu vyangu vyote bonyeza hapa

SUBSCRIBE kwenye YOUTUBE channel yangu kwa kubonyeza Hapa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X