Maana Ya Mafanikio Unaitoa Wewe Mwenyewe. Na Hivi Hapa Ndivyo Unavyoitoa


Kufanikiwa  kwako kupo mikononi mwako. Na maana halisi ya mafanikio yako unaitoa wewe mwenyewe. Kwa hiyo ukitaka kupata matokeo bora unapaswa kutoa maana bora ya mafanikio na jinsi ambavyo utayapata.

 

Ili unielewe vizuri hapa naomba nitolee mfano wa mtu ambaye kwake kufanikiwa ni mpaka pale unapokuwa na elimu ya chuo. Kwake bila ya elimu ya chuo hakuna mafanikio.kwa hiyo kinachoeonda kutoka kwa mtu kama huyu hapa ni kwamba atajituma na kujisukuma maishani , lakini kwa sababu anaamini kwamba bila elimu ya chuo hawezi kufanikiwa basi hali yake ya masha itaendelea kuwa hivyo.

 

Kuna mtu mwingine anaamini kwamba watu wa aina fulani ndio wanaweza kufanikiwa. Hivyo mtu huyu hata pale ambapo yeye atakuwa anajituma kufanya kazi lakini hali ambayo atakuwa anakutana nayo ni kwamba WATU WALE AMBAO ANAAMINI KWAMBA WAO NDIO WAMEZALIWA KUFANIKIWA NDIO ATAKUWA ANAONA WANAFANIKIWA HUKU YEYE AKIWA NA MAISHA YA KAWAIDA.

 

Kuna mtu anaamini fedha zinapatikana kwa uhaba. Hivyo atakachokutana nacho kila mara ni UHABA. Kwa sababu hicho kitu ndicho ameweka kwenye akili yake na anakiamini kwelikweli. Rafiki yangu, naomba nikuelekeze kitu kimoja muhimu sana. na kitu hiki hapa ni kwamba wewe ndiye unatengeneza mafanikio na maana ya mafanikio unitoa wewe.

Ukijiondolea vikwazo ambavyo umejiwekea kwa imani ambazo unazo sasa hivi. Au kwa hizo kauli ambazo umekuwa unajiambia mara kwa mara, ujue kwamba unaenda kupasua na kufanya makubwa zaidi. Rafiki yangu

 

Kumbuka kawamba chochote kile ambacho akili yako inaaweza kushikilia na kukimini kuwa ni kweli, LAZIMA TU ITAKiPATA

,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X