Nguvu Tatu (03) Kubwa Zitakazokusaidia Kufanikisha Malengo Yako


 

Rafiki yangu bila shaka siku ya leo imekuwa ni siku bora sana kwako. Leo hii ningependa nilete kwako nguvu tatu kubwa ambazo zitakusaidia wewe kuweza kutimiza malengo yako.

 

NGUVU YA KWANZA NI NGUVU YA KUANDIKA MALENGO YAKO

Hii ni nguvu muhimu sana ambayo inakufanya uandike malengo yako na kuwa unayapitia kila mara. Nguvu hii inatokana na ukweli kwamba kile kitu ambacho unakuwa umeandika unakuwa umekidhamiria kweli kuhakikisha kwamba unakifikia.

 

NGUVU YA PILI NI NGUVU YA KUSOMA MALENGO YAKO

Nguvu hii inakusaidia kuhakikisha kwamba ubongo wako unaweka nguvu kwenye malengo machache ambayo utayafanikisha. Nguvu inaendana na ukweli kwamba kile ambacho ubongo wako unaweza kushikilia na kukiamini basi lazima utakifikia. Hivyo nguvu hii inakuwezesha wewe kufikiria zaidi kuhusu malengo zaidi kuliko kufikiria kitu kingine chochote kile.

 

SOMA ZAIDI: RAS

NGUVU YA TATU NI NGUVU YA KUFANIKISHA MALENGO MADOGO

Kwa kutumia nguvu hii utatakiwa kuweka nguvu yako katika kuhakikisha kwamba unatimiza malengo madogo kwanza kisha unayatumia kama motisha ya kufanikisha malengo  makubwa zaidi.

Kwa mfano unaweza ukawa una lengo kubwa ambalo unapaswa kufanyia kazi mwaka huu. Ila sasa ukaamua kwamba lengo hili unaenda kuligawa kwenye malengo madogo madogo mengi ambayo unayafanyia kazi moja baada jingine, kila unapotimiza malengo haya madogo inakuwa ni motisha yako katika kuhakikisha kwamba unasonga mbele na unafanikisha malengo mkubwa zaidi.

 

Na ili uanze kufanyia kazi kitu hiki ambacho umejifunza hapa, ebu tulia kidogo kisha andika chini malenngo yako ya wiki hiii.  Ni kitu gani kikubwa ambacho ungependa kukamilisha wiki hii hapa. ukishajua ni kitu gani ambacho unataka kutimiza ndani ya wiki, basi nenda hatua ya ziada katika kuhakikisha kwamba unagawa lengo lako kubwa la wiki hii kwenye vipengele vidogo vidogo ambavyo utavifanyia kazi kila siku ili vikuwezeshe kufanikisha lengo la wiki hii nzima.

Kwa kutumia mfumo huu, nenda hatua ya ziada tengeneza malengo ya mwaka yagawe kwa malengo ya mwezi, kisha malengo ya mwezi yagawe kwa malengo ya wiki, na kisha malengo ya wiki yagawe kwenye malengo ya siku. Malengo ya siku yagawe kwenye malengo ya masaa na kuendelea.

 

Rafiki yangu hizo hapo ndizo nguvu tatu kubwa ambazo unaweza kutumia katika kuhakikisha kwamba unatimiza malengo yako ambayo umejiwekea.

 

Mimi nakutakia kila la kheri. Umekuwa name rafiki wako wa ukweli

Godius  Rweyongeza


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X