Mambo 13 Ya Kufanya Kila Siku Ili Kufikia Mafanikio Ambayo Umedhamiria


 

Rafiki ni wazi kwamba kwamba mpaka sasa hivi umeshajitoa kuhakikisha kwamba unafikia malengo yako makubwa maishani. Umeshaamua kwamba hata iweje, lazima nifanyie kazi malengo yangu na kuyafikia. Na malengo yako yanaweza kuwa ni ya kifedha (kuufikia uhuru wa kifedha, au kuwa tajiri), yanaweza kuwa ni ya kiroho, kiakili, kimahusiano n.k.

 

Sasa ukizingatia kwamba malengo mengine hayafikiwi ndani ya siku moja,nimeona nikuweke wazi kwa kukwambia baadhi ya vitu ambavyo utatakiwa kufanya kila siku ili kufikia malengo na ndoto yako. Hii safari sio safari ya siku moja. Inachukua miaka na miaka. Kuna vitu ambavyo kama hutavijua, basi kwako itakuwa vigumu sana kutoboa. Naweza kusema kwamba huu mchezo hauhitaji hasira, ila ukifanya haya mambo 12 lazima tu mafanikio yako yatakuja

 

1. Kula vizuri. Afya yako ni kitu muhimu sana. kama afya yako haiko vizuri ni wazi kuwa hayo malengo yako yataishia kuwa matamanio. Huwezi kufikia malengo yako wakati umelala kitandani, hivyo kila siku hakikisha unakula vizuri ili kuiweka afya yako katika hali ya usalama.

SOMA ZAIDI: Je, Wewe Una Matamanio Au Una Ndoto

 

2. Fanya  mazoezi. Kwa kawaida sisi binadamu ni viumbe ambao tunapaswa kuwa kwenye mwendo. Ila kwenye zama za sasa hivi, mwendo umepungua sana. Hii ni kutokana na ukweli kwamba asilimia kubwa ya kazi zinafanyiwa ofisini ambapo mtu anakuwa amekaa muda mrefu au zinafanyiwa nyumbani kabisa. hii ni tofauti na mababu zetu ambao kazi zao zilikuwa ni kuwinda au kulima. Kwa hali ya kazi ya mababu zetu ilivyokuwa hakukuwa na mtu ambaye angeweza kuwaaambia kwamba fanya mazoezi, maana kazi zenyewe zilikuwa ni mazoezi tosha. Ila sasa sisi, asilimia kubwa ya kazi zetu ni za kutulia. Kitu hiki kinafanya mwili usichangamke au kuwa kwenye mwendo kama ambavyo inapaswa kuwa. Hivyo, ndio maana nakwambia hakikisha kwamba kila siku unatenga muda wa kufanya mazoezi (KUUWEKA MWILI KWENYE MWENDO).

SOMA ZAIDI: Huyu Ndiye Arnold Shwarzenegger Na Mambo MatanoYa Kujifunza Kutoka Kwake

Hivi Ndivyo Mazoezi Yanaweza Kukufanya Ule Meza Moja Na Mfalme

3. Hakikisha kwamba unakuwa na muda wa kutafakari, sala au swala kulingana na imani yako. Ujue binadamu ana afya nne ambazo yote zinapaswa kwenda kwa usawa. Afya ya mwili, afya ya roho, afya ya akili na afya ya hisia. Afya hizi zote zinategemeana. Inapotokea kwamba afya moja umeikuza zaidi kuliko nyingine basi unakuwa umehamisha mzani na kufanya eneo moja liwe juu kuliko jingine. Hivyo hakikisha kwamba afya zako zote zinaenda sawa kila wakati.

S0MA ZAIDI: Vitu Vitatu Ambavyo Vinahitaji Kuboreshwa Kila Siku

 

4. hakikisha kwamba unakuwa na malengo ambayo yameandikwa chini. Watu wengi hawapati wanachotaka kwa sababu hata hawajui kitu ambacho wanataka. Hivyo wanakuwa tu wanaamka, wanazunguka huku na huko na jioni wanarudi nyumbani kulala. Kitu hiki ni kibaya sana. unapaswa kuwa na melengo ambayo yanakuongoza kufanya maamuzi yako ya kimaisha. Usiishi tu kubahatisha, kuwa na kitu ambacho ungependa kufikia.

 

5. soma malengo yako kwa kurudiarudia kila siku. Ni wazi kwamba kila siku unakuwa na vitu vingi vya kufanya, kama hutajipa nafasi ya kusoma na kurudia malengo yako kila siku. Itafikia hatu ambapo utayasahau kabisa malengo yako.Ndio maana inatakiwa kila siku uyasome.

 

6. Yagawe malengo yako kwenye vipengele vidogo. Hapa ninamaanisha hivi, kama una malengo makubwa ya mwaka, au miaka kumi anza kuyagawa chini kwenye lengo ya mwezi, kisha malengo ya mwezi yagawe kwenye malengo ya wiki na malengo ya wiki yagawe kwenye malengo ya siku. Kwa kufanya hivi kila wiki utakuwa unapima mwenendo wako kwa kuangalia kazi ambazo unafanya na wapi ambapo wewe mwenyewe umeweza kufika. Kitu hiki kitakufanya kila wakati uendee kuwa kwenye mwendo ukijua wapi unataka kufika

 

7. Fanyia kazi malengo yako kila siku. Kuna watu wanadhani wamba mafanikio makubwa yanaweza kufika ndani ya siku moja tu, yaani tarehe 1 disemba (mwisho wa mwaka) hata hivyo kitu hiki hapa sio kweli. Mafanikio ni muunganiko wa vitu vidogo ambavyo vinafanywa kwa kipindi kirefu. Sasa muunganiko wa hivi vitu vidogo  kwa pamoja ndivyo huleta mafaniaakio makubwa.

 

Unaweza kuwa unaona kwamba vitu vidogo, havina maana ila kama kila siku unafanya vitu vitatu mpaka vitano. Kufikia mwishoni mwa mwaka ni lazima tu utakuwa umeweza kufikia malengo makubwa kwa viwango ambavyo wewe hukutegemea kufikia. Hivyo jenga utaratibu wa kufanyia malengo yako kwa kuafanya vitu vidogo vidogo kila siku ili uweze kufikia malengo yako

SOMA ZAIDI: Kosa Kuu Ambalo Watu Hufanya Kwenye KuwekaMalengo

8. Soma vitabu

Huhitaji kuanza kufanya kila kitu kwa kubahatisha. Kuna watu ambao walishafanya vitu hivi na kuandika kwenye vitabu. Hivyo ni suala la wewe tu kujifunza kutoka kwenye hivi vitabu na kuyaweka uliyojifunza kwenye matendo.   Vitabu ni kama jicho la kukusaidia wewe kuona yale ambayo wengine hawaoni. Nimeandika makala nyingi sana kuhusu umuhimu wa vitabu, kwa leo ningependa

Usome makala hii hapa; TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOYEA-128,Tatizo Hujajua Umuhimu Wa Kusoma Vitabu

au hii hapa MAKALAM AALUMU KWA WATU MAALUMU: Kwa nini kusomavitabu

Kisha nitaenda kukutumia kitabu bure cha kusoma le leo. Bonyeza hapa ili ukipate

 

9. Jifunze ujuzi unaoendana na lengo.

Kama kufikia lengo lako kunahitaji muunganiko wa ujuzi mbali mbali, basi usisite kujifunza ujuzi ambao unahitajika. Kwa mfano mimi mafanikio yangu makubwa kwenye uandishi yanahitaji niwe na ujuzi  kucharaza vizuri kwenye kibodi. Hiki ni kitu ambacho huwa nakifanyia kazi mara kwa mara kuhakikisha kwamba ninaweza kucharaza kwa kasi kuliko mtu yeyote. Na mpaka sasa hivi najifahamu kuwa huwa ninacharaza kwa kasi sana kuliko mtu  mwingine ambaye nimewahi kukutana naye.  Na wewe kama ujuzi wa aina hii ambao unapaswa kujifunza, basi usisite kutafuta maarifa sahihi ili yaweze kukusaidia. Siku hizi mitandao imerahisisha sana, kiasi kwamba hata kama unapenda kujifunza lugha unaweza kujifunza ukiwa nyumbani kwako. na kama unapenda kujifunza biashara au fedha, inawezekana pia ukiwa hapo hapo nyumbani kwako. kwa hiyo rafiki yangu, nikushihi sana ujue ujuzi muhimu ambao wewe unauhitaji ili kufikia malengo yako na uhakikishe kamba unaufanyia kazi.

 

SOMA ZAIDI: HIVI NDIVYO UNAWEZA KUJIFUNZA LUGHA MPYA 2020 (UkiamuaKuitumia Vyema Njia Hii Mwakani Watakusikia Ukinena Kwa Lugha Nyingine)

10. Tengeneza mzunguko wa watu ambao wanakufanya usongembele.

 Huwa ninapenda kusema kwamba huwezi kuwa komando kwa kufanya mazoezi ya mgambo. Vivyo hivyo huwezi kufanikiwa kwa kuungana na watu ambao wanakurudisha chini. Tafuta mzunguko wa watu sahihi ambao  muda wote watakusaidia wewe kuweza kufikia malengo yako.

Jana nilisoma historia ya  mtu ambaye alilalizimika kulipa dola laki 6 na nusu ili kula mlo mmoja tu na warren buffet ili ajifunze siri zake za uwekezaji. Sasa hiki kitu kinaweza kuonekana kama kitu cha kijinga kwa baadhi ya watu, au kinaweza kuonekana ni kitu cha kupoteza fedha ila ni kitu muhimu sana maana kukutana watu waliofanikiwa kunakupa mwanga wa kuiona dunia katika namna ambavyo ulikuwa hujawahi kufikiri. Unaweza kujifunza kitu kipya ambacho kinaweza ambacho kinaweza kuwa msaada maisha yako yote. Na hata kukuletea utajiri ambao unataka.

 

11. Shangilia mafanikio madogo.

Unaweza kujikuta kwamba unakimbizana na mafanikio kiasi kwamba hata vitu vidogo ambavyo unafikia unavisahau. Ni muhimu sana kushangilia mafanikio madogo pale yanapopatikana. hii pia inakupa nguvu ya kufikia nguvu ya kufikia mafanikio makubwa zaidi maana unakuwa unajenga mafanikio juu ya mafanikaio. Yaani unakuwa umejenga msingi kwamba kama nimeweza kufikia mafanikio madogo, basi siwezi kushindwa kufikia mafaniakio makubwa.

SOMA ZAIDI: Kama Sio Wewe Nani? Kama Sio Sasa Lini?

 

12. Pata muda wa kulala wa kutosha kulingana na mwili wako. Wataalamu wanapendekeza kila mtu kulala masaa nane kwa siku. Hata hivyo, miili yetu sisi binadamu inatofautiana. Kuna wanaohitaji masaa nane kweli, wengine wanahitaji masaa saba na wengine zaidi ya masaa nane au pungufu ya saba.

Kwa hiyo ni vizuri wewe mwenyewe kuujua mwili wako. Jua ukiunyima usingizi huwa unakuwaje, hivyo lala masaa yanayostahili.

Siku si nyingi nilikuwa nasoma historia Albert Einstein, nikagundua kwamba alikuwa analala masaa 10. Lakini Thomas Edison alikuwa analala masaa matatu na yeye alipoulizwa kwa nini unalala masaa machache alisema,kitu kikubwa sio wingi wa masaaa ambayo mtu analala. Isipokuwa ubora wa usingizi.

Sasa ni juu yako wewe pia rafiki kuhakikisha kwamba unapata muda ambao unakufaa kulingana na mwili wako.  Japo kwa upande wangu ushauri wa Benjamin Franklin  huwa naukubali sana. anasema hivi, kulala mapema, kuamka mapema kunamfanya mtu anakuwa na afya njema, tajiri na mwenye busara.

 

SOMA ZAIDI: JE, UNAAMKA SAA NGAPI? UNAFANYA NINI BAADA YA KUAMKA? Mbinu Mpya Na Zilizothibitishwa Zitakazokuwezesha Kuamka Asubuhi Na Mapema

 

13. Usijihusishe na mabishano kwa aina yoyote. Watu wakianza kubishana, wewe ondoka eneo hilo hapo maana utapoteza nguvu zako bure kabisa. mabishano mara nyingi huwa hayambadilishi mtu. Kila mtu huwa anaendela na msimamo wake hata baada ya mabishano kuisha. Hivyo njia bora ya kumbadili mtu au kumwelimisha mtu sio kupitia mabishano. Kama unaona kuna ujumbe ambao unapenda kuuwasilisha kwa mtu basi tafuta njia nyingine ila sio mabishano.

Rafiki yangu,hayo ndi mambo 13 ambayo nimeona nikushirikishe siku ya leo ili uweze kuyahusisha kwenye maisha yako ya kila siku na uweze kufikia mafanikio makubwa.

Kama ambavyo nimekwambia hapo awali, hii safari ni ndefu na haiitaji hasira. Hivyo huu unapaswa kuwa mwongozo wako wa kukupeleka kule ambapo unataka. Binafsi nakupenda sana rafiki yangu na nikutakie kila la kheri.

Usisahau kujiunga na mfumo wetu wa kupokea makala maalumu kwa kubonyeza HAPA

 

MAKALA NYINGINE ZINAZOENDANA NA HII:

Toa Uso wako Facebook Na Uweke Kwenye Kitabu

 Ni mimi anayejali mafanikio yako,

GODIUS RWEYONGEZA

KUWA MIONGONI MWA WATU AMBAO WANAPOKEA MAKALA MAALUMU KWA WATU MAALUMU KWA KUBONYEZA HAPA

SUBSCRIBE KWENYE CHANNEL YANGU YA YOUTUBE HAPA


JIUNGE NAMI KWENYE NURU ANGAZA


2 responses to “Mambo 13 Ya Kufanya Kila Siku Ili Kufikia Mafanikio Ambayo Umedhamiria”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X